Toyota harrier kwa bongo bei gani,nahitaji

Rutunga M

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2009
Posts
1,769
Reaction score
1,393
Nina mahitaji ya gari aina yaToyota harrier lakini kwa kuwa humu kuna wadau wa haya mambo na waliowahi kutumia wanisadie hasa kwa issue ya bei kwa tz sh,fuel consumption,kupatikna kwa vipuri nk,sitaki kuagiza gari nje,nimeishalizwa,nanunua hapa hapa.Najua ninaweza kutopata za rangi hizi lakini nataka aina hiyo,wauzaji kazi kwako.Bei isiwe katika USD iwe katika sh na specification zake

images

images
 
Rutunga M, usiogope, japo kuna vitu ambavyo inatakiwa ujiulize kabla ya uamuzi wa kununua gari, namna yako ya uendeshaji iKoje?, untaka gar ya kufanyia nn? Na soul connection na engines( tofauti tofauti ukoje), hii itasaidia to have a right choice of a car.

Sina cha kukushauri kwanza mpka maswali yangu ujibu
 
Ni gari nzuri mkuu,kwa model hiyo itakuwa ina VVTI ,na fuel consumption si kubwa kivile,ntingi ni cc 2400,haitishi sana,kwa model za kuanzia 2004 na kuendelea inabidi uwe na fundi hasa mtaalamu,maana magari ya miaka hizo yna hitaji utaalamu zaidi ikiwamo computer software kuyafanyia service na matengenezo.Hata hivyo ningekushauri uagize tu nnje itakuwa nafuu kuliko hapa.Vipuri si shida.bei unaweza kupata katika mitandao ya kuuza magari
Nina mahitaji ya gari aina yaToyota harrier lakini kwa kuwa humu kuna wadau wa haya mambo na waliowahi kutumia wanisadie hasa kwa issue ya bei kwa tz sh,fuel consumption,kupatikna kwa vipuri nk,sitaki kuagiza gari nje,nimeishalizwa,nanunua hapa hapa.Najua ninaweza kutopata za rangi hizi lakini nataka aina hiyo,wauzaji kazi kwako.Bei isiwe katika USD iwe katika sh na specification zake

images

images
 
Ila bodi zake huwa km ganda la yai, afu zinachoka haraka
 
Mie nmechukua juz M18 tu metalic colour,kikubwa n kuwa na middle man mwaminifu na mjuz wa magar
 
yap kwa wajuzi bei inacheza humo 15mn hadi 28mn, hiyo ni bei ya used car,

bei ni kulingana na condition ya huo u-used wa gari, au muuzaji ana shida,
 
Harrier kwa milioni 18, Itakuwa ya mwaka 96/98
 
Kweli mkuu. Harrier kama aliyoonyesha hauwezi kuipata hata kwa 20m. Anzia 28m na kuendelea. Kama utaikuta mtu anauza chini ya 20m basi hiyo ni ya miaka ya 90 na itakuwa imechoka sana. Ila hizo gari ni nzuri,uki drive ni kama ndege flani hivi!
 
Hiyo ya kwenye picha hata mil 28 hakuna. Ni kuanzia 40 mil. lakini yeye hajasema anataka kama hiyo. Yeye anataka harrier tu.
 
tatizo la wabongo wala hawajui namna ya kutumia mitandao kuuza vitu.mtu anasema 'mimi ninayo ni 18m' basi!

tunataka ubandike specifications zake nk,pia haya mambo ya kutaka kutumia chemba(PM) inaonesha mashaka fulan,njoo jamvini sema sifa za gari lako na bei,wadau au wajuzi wa haya magari watanisaidia kupitia coments.

mpaka sasa sijapata
 
mtu akihitaji um PM hujue huyo ni mbabaishaji tu, mjasiliamali wa ukweli huweka mambo hadharani.
 
tatizo la wabongo wala hawajui namna ya kutumia mitandao kuuza vitu.mtu anasema 'mimi ninayo ni 18m' basi!

tunataka ubandike specifications zake nk,pia haya mambo ya kutaka kutumia chemba(PM) inaonesha mashaka fulan,njoo jamvini sema sifa za gari lako na bei,wadau au wajuzi wa haya magari watanisaidia kupitia coments.

mpaka sasa sijapata

Na mimi nafatilia apa kwa ukaribu. Unaweza kupata a rough pic ya bei.mtandaoni pia

Ila kama walivosema wengine zinarange kuanzia huko 15m na28 kutegemea mwaka.na hali ya gari. But with 18m unaweza kupata nzuri hata kama ya miaka ya nyuma but ina hali nzuri na ni Harrier
 
Nina mahitaji ya gari aina yaToyota harrier lakini kwa kuwa humu kuna wadau wa haya mambo na waliowahi kutumia wanisadie hasa kwa issue ya bei kwa tz sh,fuel consumption,kupatikna kwa vipuri nk,sitaki kuagiza gari nje,nimeishalizwa,nanunua hapa hapa.Najua ninaweza kutopata za rangi hizi lakini nataka aina hiyo,wauzaji kazi kwako.Bei isiwe katika USD iwe katika sh na specification zake

images

images

Nitafute, Harrier ya mwaka 2001,Auto,CC 2390 Rangi ya Silver, Mileage 70,000kms, haijatumika bongo na inatoka bandarini kesho tar. 26 August. Bei Mil.21 kamili. If interested call 0658192116
 
Back
Top Bottom