mkuu chukua tu hiyo gari mimi mwenyewe walinitisha sana wadau wa humu jf lakini ubishi wangu ulinifanya niagize na huu ni mwaka unaenda wa tatu, nilikuwa natumia chevrolet suv nilinunua ughaibuni nimetumia kama miezi sita hapa bongo kwa safari za mjini na nyumbani lakini nikaona nalifanyia kazi gari kwani lilikuwa linakula sana mafuta,nikaamua niwe nalitumia kwa safari za mbali sana na nikanunua Duet, niliifanyia modifications kama kuinyanyua juu pamoja na kuifunga sports tires na rims za size kumi na nne,uwezi amini nasafiria Tanga kila week ends na gari iko stabble barabarani hata ukipishana na roli haiyumbi na ulaji wake wa mafuta ni mzuri sana,km 14 hadi 20 kwa lita moja, cha muhimu ni service tu na spare zake zinapatikana sana siku hizi tofauti na zamani.