Tovuti ya linki tanzania

Joined
Nov 2, 2006
Messages
4,235
Likes
38
Points
0

Yona F. Maro

R I P
Joined Nov 2, 2006
4,235 38 0
Kwahiyo umekuwa unahangaika kupata Linki za tovuti mbalimbali za kitanzania si ndio ? kama ni ndio jaribu kutembelea www.tzlinks.com ni moja ya tovuti yenye Linki nyingi kuliko zote mpaka sasa ambazo zina maelezo kidogo pamoja na mpangilio mzuri .

Kama nawe unatovuti yako unaweza kuisajili kwenye Database yao kwahiyo itaweza kuonwa na watu wengine hata kwenye search engine inaweza kuwa rahisi zaidi kuitafuta .

Kumbuka taarifa zilizokuwa humo ndani sio lazima ziwe asilimia 100 sahihi kwa sababu kuna baadhi ya linki na maelezo yamekosewa haswa kwenye blogu na forums Fulani Fulani lakini nimeshawaandikia wenyewe wataangalia suala hilo .

Pia kuna tatizo lingine la lugha inaonyesha hawajakipa Kiswahili kipaumbele katika utendaji wao nafikiri hili linaweza kuwa pigo kubwa la kibiashara kwao kama wasipokuwa makini haswa kwenye ushindani wa search engine kama google ambayo imeanza utumiaji wa Kiswahili kwenye bidhaa zake zingine .

Na kwenye linki ya top Hits hawajaandika wanatumia vigezo gani kuweza kutambua hizo top hits na ni hits kwa watembeleaji wa tovuti yao au wale wanaosearch sehemu zingine hichi pia inaweza kuleta utata kibiashara kwa tovuti zingine .

Pia unaweza kujisajili kwa ajili ya kuweka makala na maandiko yako mengine pamoja na huduma zingine nyingi Karibuni sana katika TZLINKS tembeleeni toeni mawazo ya kuboresha na maoni mengine ambayo yanaweza kusaidia katika kuendeleza Tovuti hiyo kwenda mbali zaidi .
 

Forum statistics

Threads 1,189,736
Members 450,798
Posts 27,645,707