Tottenham Hotspurs Thread

Huyu pochettino kosa kubwa atakalofanya ni kuhamia Man Utd akidhani ataweza kurudia mafanikio yake ya spurs huko.... Akumbuke Man united ni timu kubwa kihistoria hivyo ukifika pale wanakuwa na matarajio makubwa yaani ushinde champions league au ligi kuu tofauti na spurs ambao wakimaliza nafasi yoyote ndani ya top 4 bado anaonekana ni shujaa.

Pia kazoea kuongoza wachezaji wa bei rahisi wasio na complications tofauti na dressinh room ya Man Utd iliojaa mastaa wanaojiona miungu watu kina pogba n.k hapo lazima kocha kama poch ashindwe kuwahandle na akishindwa beba ligi anatimuliwa msimu huo huo kwa aibu

Hizi tamaa zilimponza David Moyes.... Naliona anguko kubwa sana la pochettino
 
Back
Top Bottom