Sasa wewe mkubwa unaposema;
"...napendekeza PGO iwekewe kipengere cha 'enhanced interrogation' na utaratibu uwekwe wazi..."
Wewe unaijua na umewahi kuisoma PGO achilia kwanza kuielewa...?
Wewe unadhani jambo hili muhimu na maelekezo yake ya namna ya kulitekeleza linaweza kukosekana kwenye utaratibu wa polisi wa kila siku wa kutekeleza majukumu yao as stipulated in the PGO...?
SIKILIZA NDUGU YANGU NA WENGINE WOTE MNAONISOMA HAPA;
##Tatizo hapa siyo PGO...
##Tatizo hapa siyo sheria zinazoongoza utendaji kazi wa jeshi la polisi....
##Tatizo hapa siyo Polisi mwenyewe kama watu...
å Tatizo letu hapa ni MFUMO MBAYA WA UTAWALA unaotoa IMPUNITY kwa viongozi (watawala) wasiowajibika kwa YEYOTE kwa maamuzi yao kiasi cha kujiona wako juu ya SHERIA...!!
##Na kwa kesi hii inayoendelea, tatizo siyo watuhumiwa kuteswa ili polisi kupata taarifa muhimu za kiusalama na upelelezi ili kuzuia maafa...
##Tatizo la polisi na waendesha mashitaka kwenye kesi hii ya Freeman Mbowe na wenzake ni msingi wa mashitaka yenyewe kuwa ni UONGO wenye HILA ndani yake kwa kuwa tu watawala wenye IMPUNITY wanataka kumtoa ktk picha mtu fulani aliye kikwazo cha maslahi yao binafsi...
Udhaifu huu wa polisi katika hoja ya hapo



juu ndiyo ambayo mawakili wa upande wa utetezi wanajaribu kuuweka wazi kwetu na kutufanya kuliona Jeshi la polisi ktk picha yake halisi...
Ndiyo maana, polisi wote (akiwemo RPC wa Kinondoni ACP Ramadhani Kingai kama mbeba mikoba wa kesi) waliokwisha kutoa ushahidi, wamedhihirisha wazi kuwa hawana uelewa na sheria, kanuni na miongozo ya utendaji kazi wao wa siku kwa siku unaojulikana kwa jina la "POLICE GENERAL ORDERS - PGO"...
##Kwa hiyo, kwa kuwa msingi wa kesi yenye ni UONGO, kamwe hawawezi kutumia njia halali mbele ya macho ya sheria kutafuta au kukusanya ushahidi wao...
##Kwa hiyo ndugu kama ni watuhumiwa kuteswa na kutwezwa utu wao kwa njia isivyo halali, imefanyika si kwa sababu hakuna sheria na utaratibu wa kisheria unaowaongoza polisi kukusanya ushahidi wao kwa kutumia njia zote ikiwemo hiyo ya "kutesa au - enhanced interrogation", bali ni kwa sababu ya IMPUNITY isiyo rasmi wàliyo nayo ambayo huwasukuma kutekeleza for their self & personal interest badala ya public interests....!!