Topic gani hufungwa au kufutwa kabisa JF? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Topic gani hufungwa au kufutwa kabisa JF?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Invisible, Aug 8, 2010.

 1. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #1
  Aug 8, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,099
  Likes Received: 199
  Trophy Points: 160
  Baadhi ya watu wamekuwa wakijaribu kuupindisha ukweli ndani ya JF na kuanza kuwafanya watumiaji wa JF kudhani kuwa aidha wanaonewa au kuna jambo nyuma ya pazia. Ni wakati muafaka wa kuwafahamisha watumiaji wa JF (wanachama na wasio wanachama) nini hufanywa na moderators na kwa misingi ipi.

  Kwanza tuziangalie kanuni/sheria za JF ambazo ndizo hutumika kuwahukumu watumiaji wote (si nje ya hapo!). Mara nyingi tumekuwa tukiwasisitiza wanachama (members) kuwa ni vema wakazisoma sheria hizi kabla ya kuanza kuitumia JF ili hatua flani zinapochukuliwa zisionekane kuwa zimewakandamiza, ni wajibu wetu kama watumiaji wa JF kuanza kuangalia sheria hizi na kupendekeza wapi pafanyike marekebisho na kivipi.

  =============
  SHERIA NA KANUNI ZA JAMII FORUMS

  Tafadhali jiepushe na mambo yafuatayo:

  Wadau wengi wamekuwa wakiivunja kanuni hii ambayo tulikubaliana tangu 2006; haturuhusu kwa namna yoyote iwayo kuvunjiana heshima kwa makusudi wala matusi kwa namna yoyote iwayo. Mfano: Kuandika neno fvck kwa nia ya kukwepa censorship ni kutukana kwa kudhamiria kabisa, tumelishtukia hili na mara inapobainika hoja husika huondolewa na mhusika kufahamishwa juu ya kosa lake, anapothibitika kuendelea kukaidi basi hufungiwa kwa muda au kufutiwa uanachama kabisa!
  Hili nalo pia husababisha hoja za watu kufungwa, kufutwa au mhusika kupewa onyo.

  Nadhani maelezo yaliyo juu yanajieleza wazi, natamani wengi wangeelewa maana ya maneno hayo juu! JF si sehemu ya kuanzisha uchochezi aidha wa kidini, kisiasa n.k.

  Endapo itabainika umeanzisha hoja kwa nia ya kuibua uchochezi au ugomvi na mtu basi tunasikitika hoja hiyo itakufa HARAKA SANA.
  Kuna wadau walikuwa na kawaida ya kuwasiliana na wenzao kwa mapenzi yao wenyewe au hata bila wao kuhitaji, namna pekee ya kuwasilisha PM au email ambayo unaona inaleta tatizo kwako si kuibwaga katika hadhara bali kuituma kwetu na sisi tukaifanyia uchunguzi na kubaini ubovu wa PM wenyewe au Email husika ili mhusika achukuliwe hatua za kinidhamu. Tunalichukulia suala la PM na Emails kuwa private, kulileta hadharani ni kutafuta magomvi na kudhalilishana.

  Kwa bahati hili halijatokea sana JF, threads ambazo zinakuwa zinaonekana kuwa na links ambazo si salama huwa zinaondolewa haraka, aidha waanzishaji wa hoja husika hufahamishwa lakini wakionekana kukaidi hatuna sababu za kuendelea kuwasiliana nao badala ya kuwafungia kwa muda (kutokana na kukaidi) na kisha kuanza kuwa-monitor kadiri siku zinavyokwenda.
  Wahusika mnaovunja sheria hii mnajua athari yake; tunaweza kuwa tunachukizwa na kitu flani kilichofanywa na kiongozi au mtu flani ndani ya serikali au kidini, kuanzisha shutma ambazo zinalenga kumchafua mtu bila kuwa na ushahidi wa kutosha ni kutaka kumchafulia jina mhusika.

  JF si sehemu ya kuchafuliana majina, hatua za kinidhamu huchukuliwa kwa wale wenye nia ya kuitumia JF kwa maslahi yao binafsi.

  JF haitatumika kama 'attacking tool' kwa wale ambao aidha wamesimamishwa kazi sehemu, wamekosa nafasi flani za kikazi katika taasisi/idara/wizara/makampuni n.k, wamechokana/achana au shindwa elewana kwenye ndoa/mahusiano, wameshindwa kuelewana katika biashara na mengineyo ya mwelekeo huu; tukibaini kuwa unajaribu kuitumia JF kwa malengo haya, tunasikitika tutaiondoa.
  Tunaheshimu SANA hoja za kila mmoja, kuna wadau walikuwa wanadhani huenda wao si mali kitu hapa JF, tunatambua kuwa Mwenyezi Mungu katujalia karama tofauti, lakini wakati huohuo tunaamini kila mmoja anaweza kubadilika kadiri siku zinavyokwenda. Hakuna mwanachama wetu ambaye tunamwona "mbabe" dhidi ya wenzake, wote ni sawa mbele zetu na tunawapa heshima sawa.
  Hii si sheria bali ni angalizo tu.

  ==========================

  Other Rules to be noted:

  Nadhani nimeigusia hii hapo juu, lakini ni msisitizo zaidi.


  Maelezo ya hapo juu hasa yenye rangi nyekundu hupelekea posts nyingi kuondoshwa na pengine wahusika KUFUNGIWA kwa muda!
  Niliyoiwekea rangi nyekundu mkuu MS aliianza, mdau mwingine (Shy) naye amekuwa akiweka links kibao kwenye post zake, sharing is caring... Lakini sharing inapofanyika hapa JF ni vema kuweka content husika kisha utoe CREDIT kwa chanzo cha habari, haipendezi kubwaga habari JF bila kuweka chanzo (credit) cha habari. Japo kuna vyombo huchukua habari zetu hapa bila kutu-credit lakini sisi bado tunasisitiza wanachama wetu kuona umuhimu wa kuthamini vyanzo vya habari zetu.
  Hili tulilisisitiza kuwa endapo litawatokea wanachama basi wawasiliane nasi haraka. Wanaoonekana kutuma malalamiko ni wachache na hatua huchukuliwa.
  Inajieleza


  Mpaka sasa hatujapokea malalamiko ya kuvunjwa kwa sheria hii lakini ipo
  Wengi wamekuwa wakiivunja hii makusudi kabisa; wanaanzisha salaam ndani ya topic na mods huchukua hatua za kuondoa kila post yenye kuwa nje ya hoja au wanapoona topic imejaa majibizano yasiyo na tija kwa jamii basi topic nzima hufungwa au kuondolewa kabisa. Aidha, kuanzisha mjadala wa kidini sehemu ya siasa wakati kuna jukwaa la dini ni kukosea, mods huhamisha mjadala husika kwenda jukwaa husika wakiwa wameacha redirection na ukibonyeza title ya topic husika utajikuta unaendelea kuisoma katika location mpya.

  Ieleweke kuwa kila post ambayo inaondolewa kwenye public domain ipo; zinabaki kwa ushahidi siku za usoni maana wengine hukana kuwa walifanya makosa wanayoambiwa walifanya; hatufuti MOJA KWA MOJA, zinawekwa sehemu kwa ajili ya reference za makosa ya wanachama wetu.
  Inajieleza wazi tu. "Member flani" kuna kipindi alikosea kulingana na mojawapo ya sheria lakini alipogundua aka-submit unban request nasi tukawasiliana na yule ambaye walikuwa wamekoseana na wakakubaliana kuwa yameisha na akafunguliwa. Tunatambua kuwa wote huwa tunajikuta tumepandwa na jazba na wakati mwingine kutoa kauli ambazo si za kiungwana, uungwana ni vitendo, ukigundua umekosea ukaomba radhi basi utasamehewa!
  Inajieleza
  Signatures za watu wengine huwa ndefu SANA, au zina maneno yasiyo na heshima kabisa. Huwa tunaziondoa na kumfahamisha mhusika, akionekana kuwa mbishi basi ananyimwa access ya kuwa na signature. Hii pia hujitokeza kwa avatars.
  Inarejea kulekule, kuwa ni vema unapochukua content kokote haijalishi ni copyrighted au sio copyrighted, basi toa credit ya chanzo cha habari usiibwage as if ni wewe umeandaa hoja husika.
  Hizo juu zinajieleza; ingawa nyingine ni kama zinajirudia

  Na hii ndo huwapa mods kazi ngumu, wanajaribu kuzipitia threads kuangalia kama zinastahili kubakia katika public domain au zinavunja yale niliyoonyesha kwa rangi nyekundu hapo juu.... Inakuwa ni mtihani lakini kwa ushirikiano wa members wanaojali basi huzifanyia kazi accordingly.

  IELEWEKE KUWA:

  JF kamwe haitamsimamia au kumpendelea mtu kwa sababu ya DINI yake au ITIKADI YA KISIASA aliyokuwa nayo.

  Tutaendelea kutoa uhuru, hatuwezi kumfungia mtu kwakuwa hupendi anavyopingana na mtizamo wako wa kisiasa au kidini; kama huwezi kujizibizana naye kaa mbali naye.

  Hatutamwonea huruma yeyote anayeonekana kutaka kuvunja sheria kwa kisingizio chochote kile; endapo unaona kuna mtu kaenda kombo na sheria hizi usisite kuwasiliana nasi, unaweza kubonyeza CONTACT US au hata kutumia barua pepe kwenda support@jamiiforums.com ili hatua za haraka zichukuliwe.

  Malalamiko ya baadhi ya comments au topics kuachwa bila kutoa ushirikiano kwa kuziripoti hoja zenyewe via REPORT Button yanatarajiwa japo tunaamini tumeweka button wazi kwa kila mtumiaji.

  Naamini nimeyajibu maswali ya baadhi ya watu.
   
 2. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #2
  Aug 8, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmmmmmh
  mix with yours
   
 3. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #3
  Aug 8, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,275
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Asante sana Invisible kwa kutukumbusha kuendelea kuzitunza sheria zetu tulizojiwekea, maana JF inazidi kuwa kubwa sasa ina wanachama wa rika mbalimbali wenye uwezo tofauti, kuna wenye elimu ya kati, kuna maprofesa, kuna viongozi wa kitaifa, kuna wanafunzi/walimu, vile vile kuna wazuri na wabaya etc.

  Kwa hiyo JF inahitaji organization ya hali ya juu ili ku maintain huo mchanyato, bila kufanya hivyo tunaweza kujikuta tunafanya mambo ya ajabu ajabu. Nilishawahi kushuhudia members wa Forum fulani (ya nje) wakipelekana mahakamani kwa sababu ndogo tu ya tofauti iliyoachiwa iwe sugu kwenye posts zao.
   
 4. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #4
  Aug 8, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,975
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Tunashukuru kwa kutukumbusha.Ila na wewe umevunja sheria,umeandika sredi ndefu sana.Ha ha ha!
   
 5. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #5
  Aug 8, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,099
  Likes Received: 199
  Trophy Points: 160
  Lakini umeisoma... :spy:
   
 6. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #6
  Aug 8, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,975
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Nimeisoma ila kwa tabu kweli.Mpaka nimesahau yote ya juu.Nakumbuka la mwisho tu..
   
 7. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #7
  Aug 8, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 4,933
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280
  lugha zisizopendeza ni vyema zikakoma....huwa nakumbusha kuna watoto nao wanapita humu tuwe wazazi na walezi wema wa taifa letu kwa ujumla......!
   
 8. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 21,271
  Likes Received: 3,946
  Trophy Points: 280
  Mkuu Sana,
  On a lesser note though...Avatar yako inakonyezakonyeza na tumeambiwa kuwa katika ile sheria yetu ya kujamiiana kukonyeza ni kosa...hapo vipi?
   
 9. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #9
  Aug 9, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,382
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  mmh na wewe atajifungia mwenyewe..
  Lakini umeambiwa wanaangalia na Back ground ya tukio ..kuna watu wao kuvunja sheria kwao ni kawaida.
  Asante invisible kwa kutukumbusha
   
 10. K

  Katabazi JF-Expert Member

  #10
  Aug 9, 2010
  Joined: Feb 18, 2007
  Messages: 355
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu invisible, hivi thread ikifungwa au kufutwa inakuwa bado inaonekana?Na hizi tunazokuta zimepigwa msitari juu yake ziko kundi hilo?Nisamehe kama imeelezwa na nimeruka. Asante.
   
 11. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #11
  Aug 9, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,099
  Likes Received: 199
  Trophy Points: 160
  Mkuu, how many times unaanzisha topic zilizo opposite na Slaa? Huwezi ku-sense kitu unapoanzisha nyingine na zikaondolewa?

  Kumbuka, tunaweza kutofautiana kwa hoja, vikiingia vioja basi huichakachua hoja ya mhusika na kuipelekea aidha 'natural death' au kutupwa kapuni. Vinginevyo, wewe endelea kurusha mawe; nilimwona Slaa mwenyewe akikujibu kuwa anafurahishwa na changamoto anazozipata kwako na anaelewa unakuwa unalenga nini, sasa unapopata mtu akakubali kukusoma basi jaribu kumpa heshima na umwulize kiungwana swali lako ili apoteze dakika kadhaa kufikiria majibu muafaka.

  Mkuu, ukiona topic imepitishwa mstari katikati, maanake mjadala umefungwa kwa mjadala zaidi lakini unaruhusiwa kusoma kilichomo kwenye mjadala husika; kama unadhani mjadala huo unahitajika bado basi unaweza kuwafahamisha mods na wakachukua hatua za haraka kuufungua ili uendelee. Hoja iliyofutwa kabisa haipo wazi kwako hivyo kuweza kuirejelea ni vigumu.

  Shukrani wakuu
   
 12. K

  Katabazi JF-Expert Member

  #12
  Aug 10, 2010
  Joined: Feb 18, 2007
  Messages: 355
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu Invisible!

  Kwa kweli na mimi kuna wakati nilihisi labda una wasaidizi wa kukujibia baadhi ya mambo, kiubinadamu hii shughuli inabidi uwe na Turbo equipment ,ndio uweze kuifanya na la kusikitisha ni bahati mbaya /nzuri kuwa unafanya kazi na binadamu-mawe, matope vyote vinakuja kwako ni nadra kuwapata watu wanao angalau tambua kuwa hii kazi ni ngumu.

  Anyway wakati mwingine mengi tunafanya kwa ajili ya binadamu-hujui wangapi wanafaidi hata kama hawasemi. Mungu azidi kukujalia hizo nguvu au kama ni vidonge uzidi kupata ambavyo vina nguvu zaidi. Maana watu hawataki hata uugue masaa kadhaa-JF ipo kazi!:confused2:
   
 13. b

  buckreef JF-Expert Member

  #13
  Aug 12, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 310
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Invisible,

  Makala yako ndefu sana ila umeeleweka, labda utekelezaji ndio utakuwa mgumu.

  Kuna watu naona kila siku wanakiuka lakini hawachukuliwi hatua.
   
 14. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #14
  Aug 16, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,615
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  mmh!! Umesomeka, ingawa nilikuwa nasinzia nashituka naendelea kwa huo urefu.
   
 15. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #15
  Aug 31, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,354
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Mkuu Invisible, nashukuru kwa kutukumbusha. Sijui kwannini sijawahi soma, nilikuwa na-presume something else. Having gone through it, really good material kwa ajili yetu. Thanks Mkuu kwa kazi nzito hapa jamvini.

  Ukweli ni kuwa watu kama MS huwa wanakera, naona tumepumzika sasa!!
   
 16. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #16
  Sep 1, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 10,622
  Likes Received: 1,472
  Trophy Points: 280
  habari ndiyo hiyo
   
 17. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #17
  Sep 7, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,275
  Likes Received: 353
  Trophy Points: 180
  Naona kuna haja ya kuzisummarise as kuna watu wana allergy na ngwini
   
 18. n

  nkosiyamakosini Member

  #18
  Nov 12, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tupo pamoja Invisible. thanks
   
 19. WIRELESS

  WIRELESS Senior Member

  #19
  Dec 23, 2010
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 107
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamani mimi mgeni ku_ pm ndo nini?
   
 20. R

  Rechi New Member

  #20
  Dec 11, 2011
  Joined: Dec 11, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watakuwa wameelewa muongozo wa fj
   
Loading...