Huwezi kupata takwimu ya mtu masikini ila unaweza kupata tabaka la watu masikini na wanapimwa kwa vigezo mbalimbali mfano
1.wasioweza kupata hata mlo mmoja kwa siku
2.wasio na makazi na malazi
3.walio nyuma zaidi kuendana na maendeleo ya teknolojia
4.wasio na uwezo wa kupambana na majanga mbalimbali mfano matetemeko ya ardhi, mafuriko n.k.
5.wasio na huduma muhimu kama maji safi na salama, choo, umeme, huduma za afya n.k.
6.wasio na vyanzo vyovyote vya kuweza kuingiza kipato (tegemezi) hapa inawahusisha ombaomba
7.Baadhi ya makundi maalumu mfano watoto wa mitaani, malaya wanaojiuza n.k.
Zipo sababu nyingi ambao hutumika kupima umasikini na hutofautiana kutoka eneo na eneo au mtu na mtu kiasi kwamba sio rahisi kupata mtu specific kuwa ni masikini au top 10 ya watu masikini...Vipimo huwa vinatumika kwa ngazi ya jamii na Nchi.