Katika vyuo 100 bora Afrika kwa mwaka huu 2013 University of Dar es Salaam wamechukua nafasi ya 6 na kuanzia hapo mpaka namba 98 kuna Hubert Kariuki Memorial na hakuna chuo kingine cha Tanzania.Kwanza, naomba anayejua anisaidie kujua hii ranking inaangalia vigezo gani?Pili, je vyuo vyetu sio bora kiasi hicho, kwa mfano Kenya pamoja na Nairobi University kuwa ya 17, kuna vyuo vingine 5 katika orodha hiyo. Huku Uganda ikiingiza Makerere pekee katika nafasi ya 10.Nauliza ili nijue jamani maana kuuliza sio ujinga.Wakuu wanaJF naomba kuwasilisha.Soma mwenyewe hapa:Top 100 Universities in Africa | 2013 World University Ranking