Toka mtandaoni : Ripoti ya CAG inachefua

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,459
Reaction score
872,114
[emoji1241][emoji1241]Na BWANKU M BWANKU

*RIPOTI YA CAG INACHEFUA.*

Jana Ofisi ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali Mzalendo Prof Mussa Assad ilitoa ripoti yake ya ukaguzi wa maeneo mbalimbali kwa mwaka wa fedha wa 2017/18 Ofisini kwake. Ni ripoti mbaya sana iliyoibua madudu karibu kila mahari. Mamlaka za serikali za mitaa,mashirika ya umma,taasisi na vyama vya siasa kote ni majanga matupu. Hali si nzuri.

Tangu kutoka kwa ripoti hiyo nilikaa na wadau mbalimbali tukitumia masaa zaidi ya 15 kuisoma ripoti yenyewe kuanzia hii ya serikali za mitaa iliyohusisha halmashauri za majiji,manispaa,miji na wilaya 185 na hii ya mashirika zaidi ya 183 yaliyokaguliwa na Ofisi ya CAG lakini humo ndani unaweza kulia jinsi hela za umma zinavyopigwa. Inachefua.

Usiku mzima tulikuwa tunaipitia kila Sura ya ripoti na kuiangalia kwa mapana sana. Si ripoti nzuri sana kiukweli na katika hili hakuna kupepesa maneno kwa kuanza kunyoosheana vidole. Ni ripoti mbaya kila sehemu.

Halmashauri zetu ni vinara wa kubadirisha matumizi ya fedha ambapo halmashauri nyingi zikichepusha fedha kwenda kwenye matumizi mengine bila kufuata hata utaratibu. Miradi mingi imekula fedha za kutosha lakini wala haitumiki huku fedha nyingi za walipakodi zikiwa zimeshatafunwa.

Mamlaka za serikali 142 kati ya 183 nchini kama zinavyotakiwa kutenga asilimia 10 ya mapato yake ya ndani kwenda kwa vijana na wanawake wala hazitoi asilimia 10 hiyo iliyopo kisheria kuwaendea kundi la vijana na wanawake. Haijulikani fedha hizo zinaenda wapi maana walengwa wake haziwafikii. Hiki ni kichefuchefu cha ripoti hii.

Serikali za mitaa zetu zinafanya manunuzi kwa siri siri bila kuwapo hata na uthibitisho wa kimaandishi na uliozingatia ushindani halisi wa wazabuni. Hii inaonekana tenda za manunuzi kwenye hizi halmashauri zinatoka kwa kujuana juana tu na kindugu. Inasikitisha.

Malipo yasiyo sahihi na matumizi nje ya bajeti pia yameonekana sana kwa zaidi ya Billion 2 kutumika kwa vitu ambavyo havikuwa sahihi na vilivyokuwa nje ya bajeti halisi ya halmashauri. Halmashauri zetu zimegubikwa na madeni sugu ya muda mrefu yasiyolipwa hivyo kukwamisha serikali zetu kukopesheka.

Malimbikizo ya mabillion kwa mabillion ya wafanyakazi huku kukiwa na madeni makubwa ya watumishi kuidai serikali. Hali hii inachangia sana kushusha morali na moyo wa kujituma kwa watumishi wetu.

Yapo mengi sana kwenye serikali za mitaa. Halmashauri zetu ni omba omba haziwezi kujitegemea kabisa. Mamlaka za serikali za mitaa zinakidhi asilimia 13 tu ya kujiendesha. Hii ina maana bila fedha za ruzuku kutoka serikali kuu, serikali hizi zinageuka omba omba. Asilimia 87 ya matumizi ya serikali za mitaa inategemea fungu kutoka serikali kuu hivyo bila hiyo ruzuku ni njaa tupu.

Ni madudu tupu hakuna sehemu salama hata kidogo. Kuchepusha fedha kwenda kusikokusudiwa ni ugonjwa ulioota mbawa kwenye halmashauri zetu. Halmashauri 40 kwenye ripoti hii zinaonekana kuchepusha fedha za miradi ya maendeleo ya wananchi zaidi ya Million 500 na kuzitumia hata ambako hakukusudiwa. Haya ni mambo ya ajabu sana.

Madudu yapo mpaka kwenye Elimu Bure kwa baadhi ya halmashauri zetu kutuma fedha pungufu shule za msingi na sekondari ikiwa ni fedha za ruzuku kugharamia Elimu Bure. Zaidi ya Billion 2 sawa na asilimia 20 na ushee zimeshatafunwa kwenye hili. Fedha zinazotumwa mashuleni si sawa sawa na zinazotakiwa kufika shuleni hali CAG anayoisema kama inasababisha Shule zetu kushindwa kununua vifaa vya kufundishia, vifaa vya maabara,vitabu,kemikali,marekebisho madogomadogo. Wajanja wanakula hela hiyo.

Wizi, uozo na upigaji ni mwingi sana kwenye ripoti ya Mamlaka za Serikali za mitaa 185 zilizopo nchini kuanzia Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya.

*HALI YA MASHIRIKA YA UMMA.*

Hapa napo hali ni tete sana. Mashirika yetu mengi yanaingiza tu hasara kwa taifa bila kutengeneza faida wala tija yoyote.

Mashirika 14 hayana uhakika wa kutoa huduma katika siku zijazo kwani zina madeni makubwa kuliko hata mitaji yao. Yani Shirika linadaiwa fedha nyingi kuliko hata mtaji na uwekezaji wake. Ni hasara tu. Hii. Hii ndiyo Tanzania. Mashirika hayo ni Mamlaka ya Maji safi na usafi wa mazingira Lindi, Shirika la maendeleo ya Petrol,Bodi ya Utalii,DAWASCO,Baraza la Michezo la Taifa,Shirika la ndege(ATCL),Geothermal Development Company Limited,Baraza la Biashara la Taiga,Mamlaka ya Maji Safi,Mazingira-Mtwara na Mwanza,Kampuni ya TTCL,Bodi ya Maziwa na Transmission and Distribution Construction and Maintainance Company Limited. Haya mashirika ni hasara hasara hasara.

Sumatra nako Kuna upigani tupu. Huko kuna utoaji wa Leseni moja kwa zaidi ya gari moja. Huu ni udanganyifu ambao unaisababishia serikali ikose mapato me ngi sana kwa fedha hizo kwenda kwenye mfuko wa mtu fulani. Inachefua.

Huko kwenye Mifuko ya hifadhi ya Jamii(NHIF) ni madudu tupu. Kuna milundikano mizito ya madeni ya pango yanayozidi Billion 2 huku michango ya wanachama kwa mifuko hiyo ikishindwa kuwasilishwa kwa muda mrefu na kwa wakati. Ni ripoti mbaya sana. Ndugu zangu nchi hii inaibiwa sana[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]

Nitaendelea kuichambia ripoti hii na kueleza kila kitu. Lakini yote kwa yote ni ripoti mbaya sana mbaya sana.

*BRAND: UZINDUZI WA KITABU MAALUM CHA KUHAMASISHIA ELIMU-KUSINI MWEZI WA 8 NEWALA.*

Jr[emoji769]
 
Hizi ripoti ukisoma huna tofauti na mtu anayekata vitunguu,kwani sometimes unahisi machozi yanakutoka.Mimi sometimes najiuliza hivi uzalendo wa wasomi wa Tanzania upo wapi,kuna mtu anasimamia shirika au taasisi ya umaa ana Phd,Prof plus mi certificate kibao lakini unapewa taasisi baada ya kuijenga isimame wewe unaona ni fursa ya kupiga hela.Wasomi wabongo ndio maana watu wanaogopa kuwapa nafasi kubwa sababu wengi sio waaminifu.

Yaani kila sehemu ni hovyo kuna watu wanasema hatuna taasisi imara,lakini taasisi imara ni intergration ya watu waliokuwa imara na wenye uzalendo na uchungu wa nchi yao,lakini ukisoma ripoti ya CAG utaona hamna mwenye uhafadhali,kuanzia CCM ,vyama vya upinzani,taasisi,mashirika ya uma na halmashauri kote hovyo hovyo,ukirudi TAKUKURU napo wamejaa waigizaji watupu.

Ili nchi iendelee lazima kila mtu awe mzalendo na uchungu kwa hili taifa,ndipo tutafanikiwa kupata taasisi zilizo imara sababu zitakuwa zimejengwa na watu imara na si vinginevyo.Ila alichokifanya CAG nimekipenda amesimamia kile anachokiamini bila kuyumbishwa na mtu yoyote na namuombea mungu kila siku awe anafanya hivyo hivyo asimuogope mtu.

Magufuli na mkubali ila tukisema tuyapime maamuzi yake kupitia mapendekezo aliyoyatoa CAG utagundua workdone=0,kwani CAG alitoa mapendekezo 350 yaliyofanyiwa kazi 80 tu.
 
Tunashukuru kwa uchambuzi wako wa juu juu. Endelea kutuletea kwa undani. Wengine hatuna namna ya kupata hiyo ripoti.
Mimi nafikiri serikali za mitaa kushindwa kutekeleza majukumu yake kama kuwapa 10% inatokana na serikali kuu kuwanyanganya sehemu kubwa ya makusanyo na kuwarejeshea hela ndogo isyotoshereza mahitaji, badala yake wanahaha kuona kama mkono unaweza kwenda kinywani. Hamisha toa hapa peleka kule ni nyingi
Pesa nyingi tunayoambiwa inakiusanywa inaenda wapi?
 
Hizi ripoti ukisoma huna tofauti na mtu anayekata vitunguu,kwani sometimes unahisi machozi yanakutoka.Mimi sometimes najiuliza hivi uzalendo wa wasomi wa Tanzania upo wapi,kuna mtu anasimamia shirika au taasisi ya umaa ana Phd,Prof plus mi certificate kibao lakini unapewa taasisi baada ya kuijenga isimame wewe unaona ni fursa ya kupiga hela.Wasomi wabongo ndio maana watu wanaogopa kuwapa nafasi kubwa sababu wengi sio waaminifu.

Yaani kila sehemu ni hovyo kuna watu wanasema hatuna taasisi imara,lakini taasisi imara ni intergration ya watu waliokuwa imara na wenye uzalendo na uchungu wa nchi yao,lakini ukisoma ripoti ya CAG utaona hamna mwenye uhafadhali,kuanzia CCM ,vyama vya upinzani,taasisi,mashirika ya uma na halmashauri kote hovyo hovyo,ukirudi TAKUKURU napo wamejaa waigizaji watupu.

Ili nchi iendelee lazima kila mtu awe mzalendo na uchungu kwa hili taifa,ndipo tutafanikiwa kupata taasisi zilizo imara sababu zitakuwa zimejengwa na watu imara na si vinginevyo.Ila alichokifanya CAG nimekipenda amesimamia kile anachokiamini bila kuyumbishwa na mtu yoyote na namuombea mungu kila siku awe anafanya hivyo hivyo asimuogope mtu.

{Magufuli na mkubali ila tukisema tuyapime maamuzi yake kupitia mapendekezo aliyoyatoa CAG utagundua workdone=0,kwani CAG alitoa mapendekezo 91 yaliyofanyiwa kazi mawili tu.
Magufuli na mkubali ila tukisema tuyapime maamuzi yake kupitia mapendekezo aliyoyatoa CAG utagundua workdone=0,kwani CAG alitoa mapendekezo 91 yaliyofanyiwa kazi mawili tu} ....... Hakuna mahali jeshi la mtu mmoja lilishawahi kufanikiwa... Hata makomandoo hupata backup ya nyenzo na wataalam wengine

Jr[emoji769]
 
[emoji1241][emoji1241]Na BWANKU M BWANKU

*RIPOTI YA CAG INACHEFUA.*

Jana Ofisi ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali Mzalendo Prof Mussa Assad ilitoa ripoti yake ya ukaguzi wa maeneo mbalimbali kwa mwaka wa fedha wa 2017/18 Ofisini kwake. Ni ripoti mbaya sana iliyoibua madudu karibu kila mahari. Mamlaka za serikali za mitaa,mashirika ya umma,taasisi na vyama vya siasa kote ni majanga matupu. Hali si nzuri.

Tangu kutoka kwa ripoti hiyo nilikaa na wadau mbalimbali tukitumia masaa zaidi ya 15 kuisoma ripoti yenyewe kuanzia hii ya serikali za mitaa iliyohusisha halmashauri za majiji,manispaa,miji na wilaya 185 na hii ya mashirika zaidi ya 183 yaliyokaguliwa na Ofisi ya CAG lakini humo ndani unaweza kulia jinsi hela za umma zinavyopigwa. Inachefua.

Usiku mzima tulikuwa tunaipitia kila Sura ya ripoti na kuiangalia kwa mapana sana. Si ripoti nzuri sana kiukweli na katika hili hakuna kupepesa maneno kwa kuanza kunyoosheana vidole. Ni ripoti mbaya kila sehemu.

Halmashauri zetu ni vinara wa kubadirisha matumizi ya fedha ambapo halmashauri nyingi zikichepusha fedha kwenda kwenye matumizi mengine bila kufuata hata utaratibu. Miradi mingi imekula fedha za kutosha lakini wala haitumiki huku fedha nyingi za walipakodi zikiwa zimeshatafunwa.

Mamlaka za serikali 142 kati ya 183 nchini kama zinavyotakiwa kutenga asilimia 10 ya mapato yake ya ndani kwenda kwa vijana na wanawake wala hazitoi asilimia 10 hiyo iliyopo kisheria kuwaendea kundi la vijana na wanawake. Haijulikani fedha hizo zinaenda wapi maana walengwa wake haziwafikii. Hiki ni kichefuchefu cha ripoti hii.

Serikali za mitaa zetu zinafanya manunuzi kwa siri siri bila kuwapo hata na uthibitisho wa kimaandishi na uliozingatia ushindani halisi wa wazabuni. Hii inaonekana tenda za manunuzi kwenye hizi halmashauri zinatoka kwa kujuana juana tu na kindugu. Inasikitisha.

Malipo yasiyo sahihi na matumizi nje ya bajeti pia yameonekana sana kwa zaidi ya Billion 2 kutumika kwa vitu ambavyo havikuwa sahihi na vilivyokuwa nje ya bajeti halisi ya halmashauri. Halmashauri zetu zimegubikwa na madeni sugu ya muda mrefu yasiyolipwa hivyo kukwamisha serikali zetu kukopesheka.

Malimbikizo ya mabillion kwa mabillion ya wafanyakazi huku kukiwa na madeni makubwa ya watumishi kuidai serikali. Hali hii inachangia sana kushusha morali na moyo wa kujituma kwa watumishi wetu.

Yapo mengi sana kwenye serikali za mitaa. Halmashauri zetu ni omba omba haziwezi kujitegemea kabisa. Mamlaka za serikali za mitaa zinakidhi asilimia 13 tu ya kujiendesha. Hii ina maana bila fedha za ruzuku kutoka serikali kuu, serikali hizi zinageuka omba omba. Asilimia 87 ya matumizi ya serikali za mitaa inategemea fungu kutoka serikali kuu hivyo bila hiyo ruzuku ni njaa tupu.

Ni madudu tupu hakuna sehemu salama hata kidogo. Kuchepusha fedha kwenda kusikokusudiwa ni ugonjwa ulioota mbawa kwenye halmashauri zetu. Halmashauri 40 kwenye ripoti hii zinaonekana kuchepusha fedha za miradi ya maendeleo ya wananchi zaidi ya Million 500 na kuzitumia hata ambako hakukusudiwa. Haya ni mambo ya ajabu sana.

Madudu yapo mpaka kwenye Elimu Bure kwa baadhi ya halmashauri zetu kutuma fedha pungufu shule za msingi na sekondari ikiwa ni fedha za ruzuku kugharamia Elimu Bure. Zaidi ya Billion 2 sawa na asilimia 20 na ushee zimeshatafunwa kwenye hili. Fedha zinazotumwa mashuleni si sawa sawa na zinazotakiwa kufika shuleni hali CAG anayoisema kama inasababisha Shule zetu kushindwa kununua vifaa vya kufundishia, vifaa vya maabara,vitabu,kemikali,marekebisho madogomadogo. Wajanja wanakula hela hiyo.

Wizi, uozo na upigaji ni mwingi sana kwenye ripoti ya Mamlaka za Serikali za mitaa 185 zilizopo nchini kuanzia Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya.

*HALI YA MASHIRIKA YA UMMA.*

Hapa napo hali ni tete sana. Mashirika yetu mengi yanaingiza tu hasara kwa taifa bila kutengeneza faida wala tija yoyote.

Mashirika 14 hayana uhakika wa kutoa huduma katika siku zijazo kwani zina madeni makubwa kuliko hata mitaji yao. Yani Shirika linadaiwa fedha nyingi kuliko hata mtaji na uwekezaji wake. Ni hasara tu. Hii. Hii ndiyo Tanzania. Mashirika hayo ni Mamlaka ya Maji safi na usafi wa mazingira Lindi, Shirika la maendeleo ya Petrol,Bodi ya Utalii,DAWASCO,Baraza la Michezo la Taifa,Shirika la ndege(ATCL),Geothermal Development Company Limited,Baraza la Biashara la Taiga,Mamlaka ya Maji Safi,Mazingira-Mtwara na Mwanza,Kampuni ya TTCL,Bodi ya Maziwa na Transmission and Distribution Construction and Maintainance Company Limited. Haya mashirika ni hasara hasara hasara.

Sumatra nako Kuna upigani tupu. Huko kuna utoaji wa Leseni moja kwa zaidi ya gari moja. Huu ni udanganyifu ambao unaisababishia serikali ikose mapato me ngi sana kwa fedha hizo kwenda kwenye mfuko wa mtu fulani. Inachefua.

Huko kwenye Mifuko ya hifadhi ya Jamii(NHIF) ni madudu tupu. Kuna milundikano mizito ya madeni ya pango yanayozidi Billion 2 huku michango ya wanachama kwa mifuko hiyo ikishindwa kuwasilishwa kwa muda mrefu na kwa wakati. Ni ripoti mbaya sana. Ndugu zangu nchi hii inaibiwa sana[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]

Nitaendelea kuichambia ripoti hii na kueleza kila kitu. Lakini yote kwa yote ni ripoti mbaya sana mbaya sana.

*BRAND: UZINDUZI WA KITABU MAALUM CHA KUHAMASISHIA ELIMU-KUSINI MWEZI WA 8 NEWALA.*

Jr[emoji769]
Tatizo watu wa nchi hii ushabikia mambo ya kijinga kichinga sana.Jambo muhimu kama hili wako kimya sana kama vile hawajui kusoma wala kusikia.

Lakini weka mambo ya udaku ma PHD holders watachangia pumba zao mpk kujaza uji.

Mtu anasimama jukuani kwamba nchi inaendelea kumbe tunaendelea kwa kupigwa kimya kimya.

Ahhhh!!!! Tena nimegundua ndio maana mkulu wa Bunge hakupenda hii ripoti kabisa ila tutafika tuuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Laiti watanzania wengi wangejua kuwa utawala wa sasa hakuna cha maana wanachofanya ila kuharibu zaidi na kujihakikishia tu wanashinda uchaguzi ujao, basi watu wangeshangaa sana. Populism ni mbaya sana.
 
Awamu hii ndio kinara wa wizi kuliko awamu zote, kuanzia baba mwenye nyumba, bashite na mtetezi wa ndungai na tulia wakiendelea kushika usukani hawa,2025 nchi itakuwa scrap yenye vila ka vya madeni na umasikini ulio kubuhu,
CCM must go
 
TTCL walimwita Magufuli kwa mbwembwe kumkabidhi gawio la Tshs1.5b kumbe wako hoi kwa madeni!
 
[emoji3][emoji3][emoji3]lilikuwa changa la kisiasa lile kwa maslahi binafsi
 
TTCL walimwita Magufuli kwa mbwembwe kumkabidhi gawio la Tshs1.5b kumbe wako hoi kwa madeni!
Sasa viongozi wengi wanafanya kila wawezalo kuweza kusavaivu ukichaa uliopo kwani hakuna namna. Angalia mfano kuhamia Dom ofisi za wizara zipo kwenye vibanda vya mabati, ili mradi tu sifa apate. Mimi sina sifa ya kumpa mtu kwa hilo. Kwani kuna emergency gani?
 
Kazi kweli
 
Inasemekana Ufisadi uliofanywa awamu hii umezidi awamu zote nne hata zikijumlishwa pamoja !
 
Hakutaka kutengeneza mfumo unaofanya kazi badala yake akajitengeneza yeye anayefanya kazi na kupora vyanzo vya mapato vya halmshauri nyingi. Haya ndio matokeo.
 
Mm nikionaga mtu anashabikia CCM kiukweli namuona kama mchumia tumbo mbinafsi hana mapenzi ya dhati na hii nchi.
 
Back
Top Bottom