Mwanga Lutila
JF-Expert Member
- Nov 10, 2016
- 4,205
- 14,123
Jana nikiwa nimempeleka bibi hosptali ya Rufaa hapa Iringa Mjini Mida ya SAA mbili Asubuhi tukiwa kwenye foleni ya kumuona Daktari alikuja mama akiwa amevaa niqab 'kimtaani tunaita kininja" naye akapanga foleni ya kumuona Daktari, baada ya muda kidogo akatokea Nesi (mama mtu mzima) akaanza kumfokea yule mama kwa Lugha ambayo si nzuri na kusema "wewe mama ukitaka kutibiwa hebu toa taka taka lako hilo ulilovaa nyie ndio magaidi mnaotembea na mabomu kwa ajili ya kulipua watu " yule mama akabaki kimya lakini kila mtu akabaki kushangaa na kumwangalia yule Nesi.
Sasa nauliza je kuvaa ni niqab ni marufuku kwenye mahosptali?
Sasa nauliza je kuvaa ni niqab ni marufuku kwenye mahosptali?