Toka hapo nataka nifagie

Toka hapo nataka nifagie

"Toka hapo nataka nifagie"

Hiyo ni kauli iliyotoka kwenye kinywa cha mke wangu huku akiwa na bashasha ameshikilia fagio mkononi, mi ndio nilikuwa nimerudi kwenye mizunguko ya hapa na pale kwa unyonge nilisogea kuelekea upande mwingine yeye aendelee na usafi

Kauli kama hizi sio ngeni miongoni mwa wanaume waliooa au wanaoishi kinyumba na wanawake

Juzi kati mida ya jioni kama kawaida yetu wazee wa tasnia tulikuwa kiwanja chetu pendwa pande za Tel Aviv tunapiga mambo yetu wakati stori za hapa na pale zinaendelea ndipo mdau akatoa duku duku lake kuhusu wife wake, "dah siku izi naona wife anataka kunipanda kichwani ,yaani muda wote ananifokea ukirudi nyumbani ni kelele mwanzo mwisho , juzi tulikuwa katika harusi ya Majaliwa ameniaibisha kweli kweli mbele za watu alipoanza kunifosi tuondoke wakati Mimi ndio nilitaka tuondoke akanigeuzia kibao kwamba yeye ndio anataka tuondoke,yaani watu wote macho kwetu"

Wakurungwa wote tukapigwa na butwaa kusikia hayo lakini kuna kitu niligundua jamaa anajitahidi kutuelezea ili apate angalau ushauri wa kukabiliana na changamoto hiyo ingawa wanaume wote tuliokuwa pale jibu letu lilikuwa ni moja tu " wewe unamuendekeza mkeo, huyo unachapa kibao kimoja tu"

Wakati majibizano yakiendelea baina yetu kuna mzee mmoja alikuwa amekaa pembeni akiendelea na yake lakini alikuwa anasikiliza maongezi yetu yote ndipo akatugeukia na kutuambia "vijana huo ndio muda sahihi wa kuelezana na kushirikishana katika mambo yenu ya mahusiano"

Ila kwa hili suala la leo napenda kutumia nafasi hii kuwashauri na kuwaambia kitu kimoja lazima mjue siku zote kwamba wanawake ni watawala ndani ya nyumba kama ilivyo kwa wanaume kuwa viongozi ndani ya nyumba, Wanawake mara nyingi wanapenda kupata nafasi ya kuonekana ndani ya nafsi zao na jamii kwa ujumla kuonekana wao ndio wamesababisha mathalani mmefanya maendeleo flani basi wao wanapenda kuonekana wao ndio wamepelekea jambo ilo ndio maana Kuna ule usemi popote kwenye mafanikio ya Mwanaume basi Mwanamke yupo nyuma

Mwanaume ni kichwa cha familia lakini kumbuka Mwanamke ni shingo ya familia ,hivyo shingo inaweza kugeuza kichwa upande wowote inaoutaka so kuweni makini mnapodili na shingo maana kuna muda shingo inagoma mpaka ichuliwe na salimia , kijana suala la mke wako kukutawala halipo bali mke wako amekosa kupata uthamini (appreciation) mbele za watu hivyo anachofanya ni kusend messages , na mara nyingi bila yeye mwenyewe kunotice ndio maana hata ukija kumuuliza atakuluka futi mia, wake zetu wanatabia za mama zetu kuna muda anakukaripia eti uvue iyo suruali uliyovaa imechafuka

Mzee alituaga na kuondoka tukabaki tunaendelea kutafakari kwa kina zaidi
Pole sana, ila.mkuu huyo mke amekuoa au umemuoa?

Hayo mambo ni ya kuwekana sawa na mkeo ndani ya nyumba, zungumza nae mweleze kuhusu utovu wake wa nidhamu na vile ambayo anakukosea heshima, tena mwambie akileta kichwa ngumu utamrudisha kwao akafunzwe vizuri

Ila.pia na wewe jiangalie, pengine unamkosea mkeo heshima ndio maana nae haoni umuhimu wa kukuheshimu
 
Mwanamke kama mtoto bila makofi hawezi kuwa sawa

Ulilelewa na makofi nini ? Duh pole sana kwa kulelewa kwa ukatili lkn usirudie kosa la Wazazi/Walezi wako, usilee watoto wako hivyo kwa makofi, hiyo laana iishie kwako na usipasishe.

Say no to abuse, ...
 
Sijui kama ni uamuzi sahihi zaidi ya maamuzi mengine mengi! Unamwagia petrol kwenye moto! Mketishe kitako ujue kulikoni!
Sometimes inabidi utoke halafu uangalie uhusiano kutokea nje ili ujue jinsi ya kujinasua, kuna vitu watu wanafanya kwa makusudi na si kwamba hawajui wafanyalo
 
Sometimes inabidi utoke halafu uangalie uhusiano kutokea nje ili ujue jinsi ya kujinasua, kuna vitu watu wanafanya kwa makusudi na si kwamba hawajui wafanyalo
Usije ukatoka na kujifungia nje wakati funguo umeacha ndani mkuu!
 
Afu kibaya zaidi msela wako kaja yuko vizur,anataka mkapige maji weekend.mke anakuita chumban michambo inaanza,mara mnaenda kulewa ,mara maendeleo ndio Mana hayaonekani .mara jilani kapeleka mtoto wake English medium,huwa nasubir nikajichaji tu.nikirudi ndo tunaongea lugha moja ,maisha kujifananisha na level za watu wengine wanawake wanakera aisee
 
Mkuu ukiwa na mwanamke mwenye kidomo domo tabu kweli kweli.😂😂😂 Yani mie huyo ningeshamzabua makofi mapema tu

Af hii tabia ya kujifananisha na akina fulani sijui wanaipendeaga nini. Sometime natamani nimwambie si ungeenda ukawe mkewe sasa.😝:-*Usinchoshe akili mimi.
 
Wew ni mstaarabu ila jua kabisa wenzio si wastaarabu hasa katika matumizi ya hekima katika kauli zao. Wengi wanatumia midomo kama silaha to put us down. Implication yake ni makofi tu ili kuweka nidhamu sawa.
Ulilelewa na makofi nini ? Duh pole sana kwa kulelewa kwa ukatili lkn usirudie kosa la Wazazi/Walezi wako, usilee watoto wako hivyo kwa makofi, hiyo laana iishie kwako na usipasishe.

Say no to abuse, ...
 
Mkuu ukiwa na mwanamke mwenye kidomo domo tabu kweli kweli. Yani mie huyo ningeshamzabua makofi mapema tu

Af hii tabia ya kujifananisha na akina fulani sijui wanaipendeaga nini. Sometime natamani nimwambie si ungeenda ukawe mkewe sasa.:-*Usinchoshe akili mimi.
Wanakera chief,yaani nmepigana life nmei balance iko pw tu.Nataka nikapate mawazo mapya na friends eti tu castle light na tu k vant ndo anifananishe na manager wa company flan.kuwa ndo Sina maendeleo,hawa organism ukiwasikiliza Sana ,unaweza mtoa mtoto kafala nyambafuuu
 
Ukimpa nafasi mwanamke anageuka kituko, anakujumlisha na watoto wako. Anataka akupangie jinsi ya kuvaa, kunyoa, nini ule, saa ngapi utoke/urudi, na mengine ya kuudhi.
Kama wife sometimes akirudi tuu kutoka kazini au mishe zake anaanza kutufokea wote mimi na watoto akimaliza anaenda kujifungia bedroom, nimeishiwa nguvu ila niko natafuta nyumba ndogo ili akija na kisirani zake mie najitoa taratiiibuuu, labda kashanichoka hataki sema.
Halafu akifanikiwa katika yote mwishoni atakwambia tatizo lako huna msimamo. Ila ukimpinga katika suggestions zake several times atakuwa anakununia tu kwamba huambiliki kila analoshauri hulisikilizi.😂!

Katika hili ndio inadhiirisha mungu kweli alikuwa fundi. Kutengeneza kiumbe ambacho kinakubaliana na kukataa kuhusu jambo moja kwa nyakati tofauti tofauti.
 
Ukimpa nafasi mwanamke anageuka kituko, anakujumlisha na watoto wako. Anataka akupangie jinsi ya kuvaa, kunyoa, nini ule, saa ngapi utoke/urudi, na mengine ya kuudhi.
Kama wife sometimes akirudi tuu kutoka kazini au mishe zake anaanza kutufokea wote mimi na watoto akimaliza anaenda kujifungia bedroom, nimeishiwa nguvu ila niko natafuta nyumba ndogo ili akija na kisirani zake mie najitoa taratiiibuuu, labda kashanichoka hataki sema.
Mwanamke Kama huyo unaishi naye wa nini??

Au mmejenga nae maghorofa unaogopa kumuacha??

Naona Kama unataka kusolve tatizo kwa kuongeza tatizo..

Sent from my M100 using JamiiForums mobile app
 
Wewe kama ni mstaarabu wenzako jua kabisa wenzio sio wastaarabu kabisa hasa katika matumizi ya hekima katika kauli zao. Wengi wanatumia midomo kama silaha to put us down. Implication yake ni makofi tu ili kuweka nidhamu sawa.

Well, hapo labda tupo tofauti, mimi siwezi kumpiga Mwanamke hata siku moja na siyo Mwanamke tu binadamu yoyote yule, mimi natumia nguvu tu inapobidi na mara nyingi inakuwa ni kujilinda na hii ni kama tu nikishindwa kuondoka sehemu ya tukio, labda nimevamiwa na ni lazima nijitetee hapo sawa lkn kwa hali ya kawaida ni mtu amani, nimefundishwa hivyo, for the record ni mtu wa martial art Jiu -jitsu kwa miaka mingi tu sasa, na moja kati ya mafundisho tunayopewa kuanzia mwanzoni kabisa ni kutokuwa mgomvi na kutumia nguvu tu inapobidi kwa kujilinda tu lkn kwa hali ya kawaida kama unaweza kuondoka sehemu ya tukio fanya hivyo, hivyo mimi ni mtu wa peace na naumia sana nikiona mtu anampiga mtoto au Mwanamke hasa ukiwa ni Mwanaume unafanya hivyo, kwa sababu unafanya hivyo tu kwa kuwa umemzidi nguvu yule unayempiga laiti angekuwa amekuzidi nguvu au mko sawa usingethubutu kunyoosha mkono, hivyo huo ni uonevu.

Say no to abuse, ...
 
Well, hapo labda tupo tofauti, mimi siwezi kumpiga Mwanamke hata siku moja na siyo Mwanamke tu binadamu yoyote yule, mimi natumia nguvu tu inapobidi na mara nyingi inakuwa ni kujilinda na hii ni kama tu nikishindwa kuondoka sehemu ya tukio, labda nimevamiwa na ni lazima nijitetee hapo sawa lkn kwa hali ya kawaida ni mtu amani, nimefundishwa hivyo, for the record ni mtu wa martial art Jiu -jitsu kwa miaka mingi tu sasa, na moja kati ya mafundisho tunayopewa kuanzia mwanzoni kabisa ni kutokuwa mgomvi na kutumia nguvu tu inapobidi kwa kujilinda tu lkn kwa hali ya kawaida kama unaweza kuondoka fanya hivyo, hivyo mimi ni mtu wa peace na naumia sana nikiona mtu anampiga mtoto au Mwanamke hasa ukiwa ni Mwanaume unafanya hivyo,kwa sababu unafanya hivyo tu kwa kuwa umemzidi nguvu yuke unayempiga laiti angakuwa amekuzidi nguvu au mko sawa usingethubutu kunyoosha mkono, hivyo huo ni uonevu.

Say no to abuse, ...
Hamna asiyependa amani mzee, ila kuna viumbe flani wao wapo kwa ajili ya kukuondolea amani. Utafanyiwa drama hizo ilimradi tu siku iharibike.😝
 
Hamna asiyependa amani mzee, ila kuna viumbe flani wao wapo kwa ajili ya kukuondolea amani. Utafanyiwa drama hizo ilimradi tu siku iharibike.😝

Unaweza kujizuia, ni training tu, isitoshe huwezi kumbasilisha mtu mzima kwa kumpiga, kumbuka huyo amelelewa hivyo umekutana naye akiwa ni mtu mzima tayari na hakuna unachoweza kufanya kumbadilisha hata kama utatumia nguvu sana sana unaweza kumpiga ghafla akaanguka akafariki halafu unakuwa umeua, inatokea kwa watu tayari inakuwa murder case na hapo maisha yako yote yatabadilka kuanzia hapo utaishia jela, dreams zako zote kwisha, mafanikio yako yote kwisha, plans zote ulizokuwa nazo zinaishia hapo, sasa kwa nini kama unaweza kuondoka sehemu ya tukio ? Isitoshe kama ni demu wako tengana naye, Wanawake wako wengi, at least ndivyo jinsi ninavyoona mimi.

Demu utatengana nae sawa, mke je?
 
Mkuu ukiwa na mwanamke mwenye kidomo domo tabu kweli kweli. Yani mie huyo ningeshamzabua makofi mapema tu

Af hii tabia ya kujifananisha na akina fulani sijui wanaipendeaga nini. Sometime natamani nimwambie si ungeenda ukawe mkewe sasa.:-*Usinchoshe akili mimi.

Hivi mnadhani makofi ndo mnakomoa? Vimakofi vya mpenzi haviumi wala, ndo kwaaanza roho inabaki baridiii...

NB: Nimezungumzia makofi, sio ngumi wala mateke
 
Hivi mnadhani makofi ndo mnakomoa? Vimakofi vya mpenzi haviumi wala, ndo kwaaanza roho inabaki baridiii...

NB: Nimezungumzia makofi, sio ngumi wala mateke
Uzuri hua mnavitaftaga maksudi😂 mie nawagaiaga bila hiyana kutuliza mapepe.😁
 
Back
Top Bottom