Toka hapo nataka nifagie

Toka hapo nataka nifagie

chuma cha reli

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2012
Posts
2,764
Reaction score
2,566
"Toka hapo nataka nifagie"

Hiyo ni kauli iliyotoka kwenye kinywa cha mke wangu huku akiwa na bashasha ameshikilia fagio mkononi, mi ndio nilikuwa nimerudi kwenye mizunguko ya hapa na pale kwa unyonge nilisogea kuelekea upande mwingine yeye aendelee na usafi

Kauli kama hizi sio ngeni miongoni mwa wanaume waliooa au wanaoishi kinyumba na wanawake

Juzi kati mida ya jioni kama kawaida yetu wazee wa tasnia tulikuwa kiwanja chetu pendwa pande za Tel Aviv tunapiga mambo yetu wakati stori za hapa na pale zinaendelea ndipo mdau akatoa duku duku lake kuhusu wife wake, "dah siku izi naona wife anataka kunipanda kichwani ,yaani muda wote ananifokea ukirudi nyumbani ni kelele mwanzo mwisho , juzi tulikuwa katika harusi ya Majaliwa ameniaibisha kweli kweli mbele za watu alipoanza kunifosi tuondoke wakati Mimi ndio nilitaka tuondoke akanigeuzia kibao kwamba yeye ndio anataka tuondoke,yaani watu wote macho kwetu"

Wakurungwa wote tukapigwa na butwaa kusikia hayo lakini kuna kitu niligundua jamaa anajitahidi kutuelezea ili apate angalau ushauri wa kukabiliana na changamoto hiyo ingawa wanaume wote tuliokuwa pale jibu letu lilikuwa ni moja tu " wewe unamuendekeza mkeo, huyo unachapa kibao kimoja tu"

Wakati majibizano yakiendelea baina yetu kuna mzee mmoja alikuwa amekaa pembeni akiendelea na yake lakini alikuwa anasikiliza maongezi yetu yote ndipo akatugeukia na kutuambia "vijana huo ndio muda sahihi wa kuelezana na kushirikishana katika mambo yenu ya mahusiano"

Ila kwa hili suala la leo napenda kutumia nafasi hii kuwashauri na kuwaambia kitu kimoja lazima mjue siku zote kwamba wanawake ni watawala ndani ya nyumba kama ilivyo kwa wanaume kuwa viongozi ndani ya nyumba, Wanawake mara nyingi wanapenda kupata nafasi ya kuonekana ndani ya nafsi zao na jamii kwa ujumla kuonekana wao ndio wamesababisha mathalani mmefanya maendeleo flani basi wao wanapenda kuonekana wao ndio wamepelekea jambo ilo ndio maana Kuna ule usemi popote kwenye mafanikio ya Mwanaume basi Mwanamke yupo nyuma

Mwanaume ni kichwa cha familia lakini kumbuka Mwanamke ni shingo ya familia ,hivyo shingo inaweza kugeuza kichwa upande wowote inaoutaka so kuweni makini mnapodili na shingo maana kuna muda shingo inagoma mpaka ichuliwe na salimia , kijana suala la mke wako kukutawala halipo bali mke wako amekosa kupata uthamini (appreciation) mbele za watu hivyo anachofanya ni kusend messages , na mara nyingi bila yeye mwenyewe kunotice ndio maana hata ukija kumuuliza atakuluka futi mia, wake zetu wanatabia za mama zetu kuna muda anakukaripia eti uvue iyo suruali uliyovaa imechafuka

Mzee alituaga na kuondoka tukabaki tunaendelea kutafakari kwa kina zaidi
 
Ukimpa nafasi mwanamke anageuka kituko, anakujumlisha na watoto wako. Anataka akupangie jinsi ya kuvaa, kunyoa, nini ule, saa ngapi utoke/urudi, na mengine ya kuudhi.
Kama wife sometimes akirudi tuu kutoka kazini au mishe zake anaanza kutufokea wote mimi na watoto akimaliza anaenda kujifungia bedroom, nimeishiwa nguvu ila niko natafuta nyumba ndogo ili akija na kisirani zake mie najitoa taratiiibuuu, labda kashanichoka hataki sema.
 
Wewe na huyo mwanaume mwingine kuna vitu vidogovidogo mnavipuuza kutoka kwa wake zenu hadi wanaona mnafaa kuendeshwa
 
Ukimpa nafasi mwanamke anageuka kituko, anakujumlisha na watoto wako. Anataka akupangie jinsi ya kuvaa, kunyoa, nini ule, saa ngapi utoke/urudi, na mengine ya kuudhi.
Kama wife sometimes akirudi tuu kutoka kazini au mishe zake anaanza kutufokea wote mimi na watoto akimaliza anaenda kujifungia bedroom, nimeishiwa nguvu ila niko natafuta nyumba ndogo ili akija na kisirani zake mie najitoa taratiiibuuu, labda kashanichoka hataki sema.

wakuu thaman yako iko palepale ingawa kuna watu wana mapenzi kweli ila namna nzur ya kuyawasilisha wanakosaa. Kuambiwa upishe Alifanye eneo ulilokaa kuw safi kun shida gan!!? Hii inaleta ukakasi ukiwek tafsiri ya ubabari..
 
Hii imenichekesha sana "juzi tulikuwa katika harusi ya Majaliwa ameniaibisha kweli kweli mbele za watu alipoanza kunifosi tuondoke wakati Mimi ndio nilitaka tuondoke akanigeuzia kibao kwamba yeye ndio anataka tuondoke,yaani watu wote macho kwetu"😂😂😂

Na hii pia "wake zetu wanatabia za mama zetu kuna muda anakukaripia eti uvue iyo suruali uliyovaa imechafuka"😂😂😂
 
Na wewe umeruhusu hali hii? 😳😳😳
Ukimpa nafasi mwanamke anageuka kituko, anakujumlisha na watoto wako. Anataka akupangie jinsi ya kuvaa, kunyoa, nini ule, saa ngapi utoke/urudi, na mengine ya kuudhi.

Kama wife sometimes akirudi tuu kutoka kazini au mishe zake anaanza kutufokea wote mimi na watoto akimaliza anaenda kujifungia bedroom, nimeishiwa nguvu ila niko natafuta nyumba ndogo ili akija na kisirani zake mie najitoa taratiiibuuu, labda kashanichoka hataki sema.
 
"Toka hapo nataka nifagie"

Hiyo ni kauli iliyotoka kwenye kinywa cha mke wangu huku akiwa na bashasha ameshikilia fagio mkononi, mi ndio nilikuwa nimerudi kwenye mizunguko ya hapa na pale kwa unyonge nilisogea kuelekea upande mwingine yeye aendelee na usafi

Kauli kama hizi sio ngeni miongoni mwa wanaume waliooa au wanaoishi kinyumba na wanawake

Juzi kati mida ya jioni kama kawaida yetu wazee wa tasnia tulikuwa kiwanja chetu pendwa pande za Tel Aviv tunapiga mambo yetu wakati stori za hapa na pale zinaendelea ndipo mdau akatoa duku duku lake kuhusu wife wake, "dah siku izi naona wife anataka kunipanda kichwani ,yaani muda wote ananifokea ukirudi nyumbani ni kelele mwanzo mwisho , juzi tulikuwa katika harusi ya Majaliwa ameniaibisha kweli kweli mbele za watu alipoanza kunifosi tuondoke wakati Mimi ndio nilitaka tuondoke akanigeuzia kibao kwamba yeye ndio anataka tuondoke,yaani watu wote macho kwetu"

Wakurungwa wote tukapigwa na butwaa kusikia hayo lakini kuna kitu niligundua jamaa anajitahidi kutuelezea ili apate angalau ushauri wa kukabiliana na changamoto hiyo ingawa wanaume wote tuliokuwa pale jibu letu lilikuwa ni moja tu " wewe unamuendekeza mkeo, huyo unachapa kibao kimoja tu"

Wakati majibizano yakiendelea baina yetu kuna mzee mmoja alikuwa amekaa pembeni akiendelea na yake lakini alikuwa anasikiliza maongezi yetu yote ndipo akatugeukia na kutuambia "vijana huo ndio muda sahihi wa kuelezana na kushirikishana katika mambo yenu ya mahusiano"

Ila kwa hili suala la leo napenda kutumia nafasi hii kuwashauri na kuwaambia kitu kimoja lazima mjue siku zote kwamba wanawake ni watawala ndani ya nyumba kama ilivyo kwa wanaume kuwa viongozi ndani ya nyumba, Wanawake mara nyingi wanapenda kupata nafasi ya kuonekana ndani ya nafsi zao na jamii kwa ujumla kuonekana wao ndio wamesababisha mathalani mmefanya maendeleo flani basi wao wanapenda kuonekana wao ndio wamepelekea jambo ilo ndio maana Kuna ule usemi popote kwenye mafanikio ya Mwanaume basi Mwanamke yupo nyuma

Mwanaume ni kichwa cha familia lakini kumbuka Mwanamke ni shingo ya familia ,hivyo shingo inaweza kugeuza kichwa upande wowote inaoutaka so kuweni makini mnapodili na shingo maana kuna muda shingo inagoma mpaka ichuliwe na salimia , kijana suala la mke wako kukutawala halipo bali mke wako amekosa kupata uthamini (appreciation) mbele za watu hivyo anachofanya ni kusend messages , na mara nyingi bila yeye mwenyewe kunotice ndio maana hata ukija kumuuliza atakuluka futi mia, wake zetu wanatabia za mama zetu kuna muda anakukaripia eti uvue iyo suruali uliyovaa imechafuka

Mzee alituaga na kuondoka tukabaki tunaendelea kutafakari kwa kina zaidi
Jamaa yenu yuko sawa? Yeye alianzisha wazo la kutaka waondoke, baadae bibie naye anasema waondoke, kulikuwa na haja ya kubishana kuwa nani kati yao anataka wao waondoke kwenye hiyo sherehe? Mpaka watu wanawaangalia. Nahisi kama si utoto, basi wote wameshachokana. Mnataka kuondoka, ondokeni, ubishani wa nini?
 
Ukimpa nafasi mwanamke anageuka kituko, anakujumlisha na watoto wako. Anataka akupangie jinsi ya kuvaa, kunyoa, nini ule, saa ngapi utoke/urudi, na mengine ya kuudhi.
Kama wife sometimes akirudi tuu kutoka kazini au mishe zake anaanza kutufokea wote mimi na watoto akimaliza anaenda kujifungia bedroom, nimeishiwa nguvu ila niko natafuta nyumba ndogo ili akija na kisirani zake mie najitoa taratiiibuuu, labda kashanichoka hataki sema.
Sijui kama ni uamuzi sahihi zaidi ya maamuzi mengine mengi! Unamwagia petrol kwenye moto! Mketishe kitako ujue kulikoni!
 
Back
Top Bottom