Tohara ya Kisiasa,Msamaha na Maridhiano Dhidi Ya Kutibu Mipasuko Kisiasa

mwanamichakato

JF-Expert Member
Mar 20, 2015
1,168
1,071
Kabla na baada ya uchaguzi mkuu kumekuwepo na nyufa,makorongo,mipasuko na migongano mikubwa katika vyama karibuni vyote vya kisiasa nchini Tanzania..Ni wakati sasa wa vyama vya siasa kuzaliwa upya kwa kujingenga kimfumo,kufinyanga makosa yao,kujifanyia tohara , kujitengeneza kimshikamano,kujirekebisha kwenye mapungufu n.k ili kuwa imara zaidi ktk mitanange iliopo na ijayo kisiasa.

Hakuna chama kinachoweza kujitabanaisha kuwa hakikukumbwa na misukosuko ya namna yeyote na mambo ni shwali...ukweli upo wazi na amin amin nawaambia kama mianya ya mapungufu isipotibitwa mipasuko mikubwa zaidi ipo mbeleni.Ukomavu wa kisiasa ni pamoja na kukiri makosa,mapungufu,..Lakini kuwajibika kwa kutatua matatizo na si kuwa na kiburi cha kupambana na matokeo badala ya kutibu chanzo cha matokeo.

Napingana mnoo na dhana ya baadhi ya vyama {viongozi wa vyama} kuwashughulikia baadhi ya wanachama wao wa kawaida ama waandamizi waliooneshwa kukerwa/Kuumizwa/kuchoshwa/kukwazika/kujeruhiwa na mienendo,taratibu,utendaji,utumishi,falsafa,uongozi,kukosa imani na chama,maamuzi,miongozo yenye mapungufu,kauli mbiu n.k.
 
Back
Top Bottom