Tofauti ya wazi ya waraka wa TEC na KKKT

kisinja

JF-Expert Member
Sep 30, 2013
241
295
Binafsi nadhani ukiusoma waraka wa TEC na KKKT naona tofauti ya Kiuandishi na Mantiki. Waraka wa TEC ulijikita zaidi katika kipindi cha Kwaresma na Umuhimu wake kwa Wakristo hasa Wakatoliki. Sehemu kubwa ya waraka ulihusu wakatoliki na nini wafanye katika kipindi cha Kwaresma. Sehemu ikajikita katika masuala ya Kisiasa...kiutamaduni na kiuchumi na ukisoma utagundua lengo lilikuwa kuonyesha changamoto zilizopo katika nchi kwa ujumla.

Kwa maoni yangu waraka ule umeandikwa ki- falsafa zaidi. Jambo ambalo linasaidia kutoa nafasi kwa watu kupambanua bila kupiga kelele na ndio maana nadhani waraka ule haukupata kelele na mabishano tunayoyaona sasa. Pia Namna ya uwasilishaji wake haukuwa sana kana tulivyoona uwasilishaji wa waraka wa KKKT kwa kuwa baadhi ya watu wanahoji hata namna waraka ulivyopatikana kwa wanajamii....nadhani hapa lipo la kujifunza (Japo wakereketwa baadhi hawatakubali)

Namna ya uwasilishaji kwenye public, lugha tumizi, na namna ilivyopokelewa na reaction inaacha maswali kiasi fulani. Kwa mfano tumeona mitandao ya kijamii ikipokea kwa spidi kubwa tamko hili na kupata support kubwa sana kwa upande wa Upinzani na hata Maalim Seif kapongeza leo na jana Mbowe kapata nguvu mpya kwa kauli yake tofauti na waraka wa TEC na tunaona sasa kuhusishwa kukubwa kwa waraka huu na u-kkkt (kukosa nafasi....) jambo linalodhoofisha.

Binafsi na niko tayari kukosolewa hii ni mara ya kwanza rasmi nasikia neno "BARAZA LA MAASKOFU WA KKKT" japo najua KKKT wana maaskofu wao lakini hicho chombo rasmi ndo mara ya kwanza kuskia kama chombo rasmi ukiacha BARAZA LA MAASKOFU KATOLIKI TANZANIA. Mara nyingi nimewaskia wakitoa maoni kama CCT sasa sijajua kama CCT watakujaje this time au wameshindwa kuafikiana na KKKT ikabidi watoke kivyao.

Nadhani yako mengi ya kujifunza na tuwe tayari kujifunza pia kupitia mitandao badala ya kutukanana.

Wenye uelewa tafadhali tubadilishane mawazo. Tusishambulie individuals tuone michango yao na namna tunaweza kujifunza kwa faida ya taifa letu..

Soma: WARAKA: Maaskofu Katoliki waonya uminywaji wa demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari nchini

Soma: Maaskofu KKKT: Tunasikitishwa na matukio ya kupotezwa watu, kubanwa kwa Uhuru wa Mahakama, Bunge na Tume ya Uchaguzi...
 
Binafsi nadhani ukiusoma waraka wa TEC na KKKT Naona tofauti ya Kiuandishi na Mantiki. Waraka wa TEC ulijikita zaidi katika kipindi cha Kwaresma na Umuhimu wake kwa Wakristo hasa Wakatoliki. Sehemu kubwa ya waraka ulihusu wakatoliki na nini wafanye katika kipindi cha Kwaresma. Sehemu ikajikita katika masuala ya Kisiasa...kiutamaduni na kiuchumi na ukisoma utagundua lengo lilikuwa kuonyesha changamoto zilizopo katika nchi kwa ujumla.

Kwa maoni yangu waraka ule umeandikwa ki- falsafa zaidi. Jambo ambalo linasaidia kutoa nafasi kwa watu kupambanua bila kupiga kelele na ndio maana nadhani waraka ule haukupata kelele na mabishano tunayoyaona sasa. Pia Namna ya uwasilishaji wake haukuwa sana kana tulivyoona uwasilishaji wa waraka wa KKKT kwa kuwa baadhi ya watu wanahoji hata namna waraka ulivyopatikana kwa wanajamii....nadhani hapa lipo la kujifunza (Japo wakereketwa baadhi hawatakubali)

Namna ya uwasilishaji kwenye public, Lugha tumizi, na namna ilivyopokelewa na reaction inaacha maswali kiasi fulani. Kwa mfano tumeona mitandao ya kijamii ikipokea kwa spidi kubwa tamko hili na kupata support kubwa sana kwa upande wa Upinzani.....na hata Maalim Seif kapongeza leo na jana Mbowe kapata nguvu mpya kwa kauli yake tofauti na waraka wa TEC na tunaona sasa kuhusishwa kukubwa kwa waraka huu na u-kkkt (kukosa nafasi....) jambo linalodhoofisha.

Binafsi na niko tayari kukosolewa hii ni mara ya kwanza rasmi nasikia neno "BARAZA LA MAASKOFU WA KKKT" japo najua kkkkt wana maaskofu wao lakini hicho chombo rasmi ndo mara ya kwanza kuskia kama chombo rasmi ukiacha BARAZA LA MAASKOFU KATOLIKI TANZANIA. mara nyingi nimewaskia wakitoa maoni kama CCT sasa sijajua kama CCT watakujaje this time au wameshindwa kuafikiana na KKKT ikabidi watoke kivyao.

Nadhani yako mengi ya kujifunza na tuwe tayari kujifunza pia kupitia mitandao badala ya kutukanana.

Wenye uelewa tafadhali tubadilishane mawazo. Tusishambulie individuals tuone michango yao na namna tunaweza kujifunza kwa faida ya taifa letu..

Kaka,

Sijui mambo mengi kuhusu KKKT lakini nilishawahi kusikia wana kitu kiitwacho NYUMBA YA MAASKOFU.

Ila kwa wakatoliki kama usemavyo ni kweli maaskofu wetu wakiandika ni vigumu kuubishia maana wanaandika very philosophical way.

Kama waraka wa wakatoliki umetoka hata kwareasima haijaanza na sasa tuko wiki ya Pasaka, basi maana yake mabishano yanayoendelea ni kwa huu mpya, wa KKKT.

Kwa kifupi wana uzoefu wa kuandika kiasi kwamba hata askofu mwenzao akiukana kama inavyoendelea sasa anaishia kuonekana ameumbuka.

Nadhani maaskofu wa makanisa mengine hawakujikita sana kwenye haya masuala ya nyaraka na huenda hawakuwahi kuona umuhimu.
 
tumefika mahali we call a spade a spade and not a big spoon
maaskofu ni sehemu ya jamii
mambo ya ovyo yanayoendelea yanawaathiri as individuals and as the church
wameona wasizungukezunguke
you grab the bull by the horn

Nakubaliana na ww mkuu. Lakini kama taifa tuone namna ya kuakaa pamoja ili kuondoa changamoto zilizopo. Naimani tutaafika kwa kuwa nchi yetu ni moja na watanzania ni wamoja
 
Back
Top Bottom