Tofauti ya mtu na binadamu

Ni darasa la zaidi ya siku 7 andaa pesa ufundishwe vizuri kabisaa yaan tuition!!!!
 
Mtu ni aina ya kiumbe hai/mnyama mwenye utashi wa akili zaidi ya wanyama wote(Hii huweza kujulikana kwa genetic factors/biological).
Binadamu ni ile thamani,ya mtu katika mahusiano na jamii kiujumla.Na hapa huja tofauti kati ya mtu hadi mtu kulingana na mwenendo wake katika maneno ,mawazo na matendo kiujumla
 
Anayejua kinachotofautisha utu na ubinadamu anijuze tafadhali
Binadamu ni utambulisho wako miongoni mwa viumbe vingine lakini utu ni jinsi unavyoishi kama unaishi ovyo tunasema fulani hana utu yani ni kama mnyama au watu na viatu, unafananishwa na viatu kwa namna ulivyo hopeless.
 
haya maelezo yanatofautiana na kichwa cha habari. maana utu na mtu ni vitu tofauti, pia binadamu na ubinadamu ni vitu tofauti.
Hapana yuko sahihi sana, mtu ni zao la utu na binadamu ni zao la Adam. Kwahyo hapa hata ngedere anaweza akawa mtu lakini hawezi kuwa binadamu.
Utu na ubinadamu unatofautiana, utu uko juu sana ya ubinadamu. Utu ni hari ya kujari, upendo, huruma, kusaidia nk wkt ubinadamu unaweza ukayabeba hayo yote na unaweza usiyabebe na bado ubinadamu ukawa ni defence. Mfn. wivu, uchoyo, uroho, ubinafsi, kujipenda binafsi yote haya ni sehemu ya ubinadamu. Ila yako nje ya utu.
 
Jambo lolote ukijifanyia mwenyewe, hilo tunaita utu. Ukivaa kwa heshima, ukiongea kwa heshima huo ni utu.
Jambo lolote ukimfanyia mwingine, huo ni ubinadamu. Ukimsaidia masikini, yatima, ukimtetea mnyonge huo ni ubinadamu.

Kukosa utu, maana yake yale unayojifanyia mwenyewe ni ya hovyo.
Kukosa ubinadamu, maana yake yale unayowafanyia wengine ni ya hovyo.
 
Mtu na Binadamu ni viumbe wenye kufanana kwa maumbo yao na jinsia zao, ila tabia na fikra zao ndizo zinazowatofautisha,
Binadamu ni kiumbe ambaye hana uvumilivu na anatabia za asili za viumbe wengine kama mbuzi,nyoka, nguruwe nk.
Mtu ni kiumbe ambaye ni mstahimilivu na hana tabia za asili kama viumbe wengine kwa mfano ukimkopa atakuomba umrudishie tu ulichokopa, ukimkanyaga atakuomba samahani
Ukimdhurumu atakutakia heri kwa kifupi ni punguani.
 
Mtu ni aina ya kiumbe hai/mnyama mwenye utashi wa akili zaidi ya wanyama wote(Hii huweza kujulikana kwa genetic factors/biological).
Binadamu ni ile thamani,ya mtu katika mahusiano na jamii kiujumla.Na hapa huja tofauti kati ya mtu hadi mtu kulingana na mwenendo wake katika maneno ,mawazo na matendo kiujumla
Umenena vyema mkuu
 
Back
Top Bottom