Tofauti ya mchumi na bahili

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
419
670
UCHUMI KWA WASIO WACHUMI

Sio neno geni, lakini kama ilivyo kawaida kwa watu wasio na utaalamu wa somo husika kutumia maana zinazowafanya wachanganye maneno. Uchumi ni ile hali ya kufanya rasilimali kuendelea kuwepo kwa matumizi kwa muda mrefu bila kuathiri kwa ukubwa rasilimali nyinginezo. Mchumi ni mtu anayeelekeza rasilimali katika hali ya kukuza rasilimali husika. Rasilimali zinazoheshimiwa katika uchumi ni pamoja rasilimali pesa, rasilimali watu, rasilimali muda, mazingira nk.


TOFAUTI YA MCHUMI NA BAHILI

Kutokana na kukosa namna ya kutofautisha maneno husika, watu wengi wamekuwa wakichanganya maneno hayo. Nimeeleza awali kuwa nia ya mchumi ni kukuza rasimali inayokuwa haba wakati husika, japo rasilimali zote ni haba, ila hazina usawa katika uhaba wake. Hivyo mchumi huangalia rasilimali zote ili kujua rasilimali ipi ni ya kuikuza (maximize) kwa wakati husika.

Tofauti kubwa kati ya mchumi na mbahili ni kuwa, mbahili huangalia pesa kama rasilimali pekee na hivyo hupoteza rasilimali nyingine au mara nyingine hupoteza hata pesa aliyonayo.

Mfano wa kawaida ni kwa baadhi ya watu wa serikali kukataa baadhi ya miradi kutokana na gharama, kwa kuwa wao huona pesa ni rasilimali pekee, huweka miundombinu ya gharama nafuu ambayo inawafanya(kwenye long run) kuingia gharama kubwa kuliko walioikwepa mwanzo. Mfano ni ujenzi wa barabara ambazo kila mwezi zimekuwa zikikarabatiwa, hii ni kwa sababu wanatamani kuiweka hela ila wanakosa ufahamu wa namna nzuri kuiweka, hivyo basi utaona wazi kuwa wanaoitwa wachumi walioko katika idara husika ni wabahili, kama si wabahili basi ni wala rushwa ambao hawaoni umuhimu wa kutumia ujuzi wao katika kutengeneza miundombinu iliyobora badala yake hugawana hela.

Moja kati ya swali ambalo linamtofautisha mchumi na mbahili ni lile ambalo linauliza ipi ni njia ya kiuchumi Zaidi ya kusafiri kutoka Dar hadi Mwanza, kwa kutumia gari, treni au ndege? Hili swali ukiliangalia kiubahili utaangalia usafiri wenye nauli kidogo bila kuangalia kitu gani unataka kukikuza(maximize) kwa wakati husika. Taarifa za swali hazijakamilika hivyo wakati wa kujibu swali kama hilo ni lazima uweke scenarios au kiuchumi wanaita assumptions ili kutetea kwa nini kusafiri kwa usafiri Fulani ni ya kiuchumi Zaidi kuliko nyingine.

Katika swali kama hilo, mchumi hatoangalia gharama za nauli bali kitu anachotaka kukikuza kwa wakati husika. Huwezi kupanda treni wakati una mgonjwa wa dharura, kwa hiyo kama hela ipo ili kukuza rasimali mtu, itabidi upande ndege.

Ni mfano kama huu naweza kuutoa kutofautisha, inawezekana mtu yuko anakula chakula cha elf 15 lakini anapigiwa simu na kutakiwa kuwepo mahali kwenye kazi ya shilingi laki mbili, hapo mchumi ataacha chakula na kuiwahi hiyo kazi ikiwa anataka kukuza rasimali muda, yaani kama kula kunaweza kumchelewesha, ili afuate hiyo kazi basi mchumi ataacha chakula hata kama amelipa.

Lakini mbahili atabaki amalize chakula hata kama itaathiri muda wa yeye kufika kwenye kazi ya laki mbili na Zaidi.


Signed

Oedipus
 
Mkinga ni mchumi maana hata magorofa aliyojenga Manzese na kariakoo tunayaona....
Mpare ni bahili. Anashinda njaa lakini sijawahi ona gorofa la mpare kariakoo. Akinunua gari ujue ni passo.
Nadhani nimeeleweka
 
Afrika wachumi ni wachache sana.
Wengi ni wezi( mfano Wachgg) ,matapeli( Mfano Whya) , Wachawi(Wknga), Wala Rushwa (Wskma),Wanyanganyi(Wkrya),Mafisadi(Wakikuyu ), Walaghai(Wnykysa) na Waongo (Wanasiasa wote)

Ubahili ni jambo linalotokana na mazingira na mitizamo ya watu.
Mtu anayependa kuomba omba anawaza kusaidiwa au kupewa kila anachokihitaji akinyimwa anaona kuwa kuna ubahili. Mtu anayejitegemea bila kuomba au kutegemea misaada hawezi kuona ubahili wa MTU. Kuna mtu akifika baa yeye ni mizinga tu. Akiona mtu aliyetegemea amnunulie bia halafu akakosa anaona kuwa ni ubahili kumbe yeye ndiye tatizo. Wenzetu wazungu hawana mambo ya kutoa pesa tuu bila kuwa napangilio au bajeti (ni bahili lakini wana mipango yao).Mtu mwenye kipato halali lazima wakati mwingine anaonekana kama bahili kwenye matumizi yasiyo Rasmi.
Ndio maana Mabilionea wote ni wanyonyaji .Wanawanyonya wafanyakazi wao kwa kuwalipa mishahara kidogo sana (Ni bahili wa kutoa pesa japo wana akiba kubwa)
Ubahili ni hatua ya mwanzo ya kukuza uchumi.
Ukiona mfanyabiashara aliyeanza chini sio bahili basi huyo ni mwizi.
Vina wengi wa sasa sio bahili kwa sababu wamerithi Mali toka kwa wazazi wao ambao walikua bahili wakati wanatafuta Mali.
Unakuta kijana anarithishwa Jengo LA Hoteli au Club iliyojengwa miaka ya 70 na babu yake aliyekua anashinda kwa kula kipande cha mkate lakini leo anashinda baa na kula kiti moto na Kvant na kujisifu kuwa yeye ni mchumi sio bahili.

Wazungu karne zilizopita hawakuja Afrika kutalii Bali kutafuta Mali ,walikua wanaishi maisha ya kibahili.

Mfano Kwa hali ya Kawaida Mtu mwenye mshahara wa laki tano kwa mwezi na hana sehemu ya kupiga dili au kupata hela ya ziada au Rushwa au Vinginevyo hawezi kuepuka ubahili . Hawezi kula supu ya Kuku kila siku na kununua kiatu cha 150,000/- na Shati na suruali 45,000/- .
Mtu huyo huyo Akikutana na mwenzake mwenye kitengo cha manunuzi na madili mengineyo atajisifu kuwa yeye sio bahili.

Kifupi tu ni kwamba kuwa Mchumi au Bahili inategemea na aina ya Biashara,mtaji, Chanzo cha Biashara (au mtaji) au Mazingira ya Kipato au Kazi , Uwezo wa kifamilia n.k.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom