Tofauti ya Lowassa na Magufuli hii hapa

Tofauti ya Lowassa na Magufuli hii hapa

Nyie watoto, beba madeli yenu mkauze maji.Lowasa hawezi kushnda.Hıı haijapote kiasi cha kukabidhi nchi kwa wendawazimu na walanguzi.HATASHNDA, USIPOTEZE MUDA NA JASHO LAKO KUMTETEA.

Yodoki II;
Miye naona hujaelewa hata wa kumjibu. Naona ubabe kwako ndiyo zaidi ya kutumia hoja. CCM mmezoeya kuyapitisha kibabe, mnajua tukiwazingua watatoka mjengoni sisi tupitishe chap chap madudu yetu. Hapa ni kura zinapigwa. Tutamchagua mtu kwa utendaji wake na maono.
Kama unampenda sana Kofuli, toa hoja zako kama alizotoa mleta hoja. Mkimpitisha kibabe si mnajua tena?? Atakuwa rais wa wachache, hana experience, anataka kutenda vizuri, azuiwe na ule mfumo wetu. Ataiangusha nchi. Miaka 5 ni muda, na hatupo tayari kumpa majaribio. Kubali tu Lowasa ni jembe si hivyo tu kwani umemeguka mahali?? Kura yangu nampa Lowasa, weye yako??
 
Ndovile napenda vijana wa tanzania wanapo ongea ukweli ahsante sana kijana mwenzangu tukomae hadi kieleweke.
 
kwa nini sasa lowassa hakujiuzuru mapema kulinda heshima yake kama alikuwa na mashaka na mkataba ule?
Nani amefanya hivyo katika nchi hii,hata hivyo alijiuzuru uwaziri mkuu wakati tokomeza, escrow mbona PM hakujiuzuru kama Mtendaji mkuu wa serikali?
 
Habari wakuu
Hii nimeipata mahali nikaona vema kushare hapa JF

Nafasi ya Urais sio nafasi ya kupata "kama zali". Hata uwe kiongozi mzuri kiasi gani huwezi kushtukizwa na kupewa mikoba ya nchi kirahisi rahisi tu. Lazima uwe umejipanga, umejiandaa na uko tayari. Hotuba za Magufuli zinadhihirisha kuwa aliingia kwenye kinyang'anyiro kwa kujaribu. Membe alitangaza nia Lindi, Makamba alitangaza nia Mlimani City, Muhongo- Musoma, Mh.Lowassa;Arusha n.k. Magufuli alitangaza nia wapi? Alitaja vipaumbele gani? Nini kauli mbiu yake? HAKUNA.

Huwezi kumpa mtu 'miaka 5 ya kujiandaa' kuongoza nchi. Tunataka mtu aliyejiandaa an akiingia ikulu aanze kuongoza nchi mara moja. Mtu huyu ni Edward Lowassa.

Kuna tofauti kubwa kati ya Magufuli na Lowassa. Wote ni wepesi katika kufanya maamuzi. Lakini mmoja hufanya maamuzi yenye tija wakati mwingine hufanya maamuzi yenye madhara. Tuangalie mifano:
Mh.Magufuli 'alipiga' bei nyumba za serikali na leo hii serikali inatumia mamilioni kuwapangishia hotelini watumishi wake.HASARA!

Mh.Lowassa amesimamia ujenzi wa UDOM na kuongeza idadi ya wataalam mbalimbali nchini.FAIDA.
Ndg.Makufuli amenunua vivuko, pantoni na mashine za tiketi kwa mabilioni lakini hazifanyi kazi/ hazina ufanisi.HASARA. Mh.Lowassa alisimamia ujenzi wa bomba la maji kutoka ziwa Victoria mpaka Shinyanga huku akipuuzia vitisho vya Wasudani na Wamisri vya kuhodhi matumizi ya maji ya Victoria kwa mkataba wa kikoloni.FAIDA.

Mh.Magufuli alibomoa fuel station "shell" huko Mwanza, serikali ikashindwa kesi, tukalipa mabilioni.HASARA. Mh.Lowassa alivunja mkataba wa City Water, hatukushtakiwa.FAIDA.

Mh.Magufuli alikamata wavuvi "halali" tumeshitakiwa, tumedondokea pua, tutawalipa meli yao na gharama nyingine kadhaa, hapo hujajumlisha gharama za utunzaji wa wale samaki.HASARA. Mh.Lowassa, wakati ndege za Malawi zishaanza kuzurura maeneo ya Kyera na Nyasa huku tukiwachekea, alitoa tamko Bungeni...."tuko imara, tumejipanga...". Wakafunga Virago.FAIDA.

Ndg.Magufuli amewanyang'anya kandarasi wajenzi kadhaa kwa matamko tu bila kuzingatia taratibu za mikataba. Wametushtaki, wameshinda, tumewalipa.HASARA.

Mh.Lowassa alitaka kuvunja mkataba wa Richmond, kama sio AG Johnson Mwanyika kuomba..."mapumziko ya saa moja nje ya mkutano" ili awasiliane na mamlaka ya juu na baadae kurejea na agizo kuwa..."imeagizwa; mkataba usivunjwe.." pengine leo tusingekuwa tunazungumzia Richmond, baba yake na Dowans, babu wa Symbion Powers. TUNGENUFAIKA.

UCCM wangu hauwezi kunipofua nisiuone ukweli huo hapo juu. Ujirani wangu na Mh.Magufuli hapa Chato hauwezi kunishinikiza nimuazime miaka 5 ya kujiandaa badala ya kutawala. NITAMPIGIA LOWASSA.
 
Nilijua unatoa analysis kumbe ni udaku pole sana
 
romaki

Hujitambui ndo mana unaangalia faida za upande mmoja msifanye watanzania Kuwa ni wajinga kwa kuanza kuosha kikombe nje wakat ndani kichafu we unayemtakasa lowasa waambie ambao hawajielewi ndo watakuelewa
 
Last edited by a moderator:
Hujitambui ndo mana unaangalia faida za upande mmoja msifanye watanzania Kuwa ni wajinga kwa kuanza kuosha kikombe nje wakat ndani kichafu we unayemtakasa lowasa waambie ambao hawajielewi ndo watakuelewa

Hii ndo hoja yako au mipasho tu kama kule bungeni mtu anatoa mipasho afu wabunge wote wa ccm wanapiga makofi, we kama una ubaya wake leta hapa na ushahidi juu na sio tuhuma za kufikirika kwa hisia za kimihemko
 
Back
Top Bottom