Kwanza ufanano wao mkuu ni kwamba wote wanatibu.
Tofauti yao kubwa ni viwango vyao vya elimu, mmoja ana degree(daktari) na mwingine ana diploma(tabibu).
Daktari ni Tabibu pia, lakini Tabibu anaweza asiwe Daktari.
Kibongo huu mkanganyiko unaweza usiwe na issue sana sababu 80% ya population ni laymen.
Kwa nchi zilizoendelea ama ambazo zina high literacy rate hizi ni qualification mbili tofauti kabisa sababu wateja wanahitaji cha kwanza ujitambulishe wewe ni nani kabla hawajaanza kukueleza shida zao.
Na mteja anataka kama wewe ni tabibu basi useme ni tabibu, kama ni daktari useme ni daktari, kama ni specialist useme ni specialist na kama ni super-specialist basi useme.
Na wateja wanajua limit ama uwezo wa mwisho wa kila mtu iwe tabibu ama daktari ama specialist. Sasa ukijifanya wewe mjuaji sana basi hauchukui round mteja anaku-sue.