Tofauti kubwa hivi nchi moja- je ni sawa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tofauti kubwa hivi nchi moja- je ni sawa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MzalendoHalisi, Feb 7, 2009.

 1. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Wandugu nimeenda BBC country profiles nikaangalia Life Expectancy (LE) Tanzania (51 years men: 54 years women)

  na Visiwani (42 years men: 44 years women) tofauti miaka zaidi ya 10 yaani Tanzania wanaishi miaka 10 zaidi kwa wastani ukilinganisha na Zanzibar!

  Hii inawezekana ktk nchi moja??

  Nilidhani LE visiwani ingekuwa juu zaidi kwa vile ukimwi kule kidogo!

  Waungwana mnasemaje?

  Wenzetu Visiwani mnasemaje?


  See the source: BBC NEWS | Africa | Country profiles | Regions and territories: Zanzibar

  and BBC NEWS | Africa | Country profiles | Country profile: Tanzania
   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  Feb 7, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Peleka hii topiki kwenye habari na matangazo madogomadogo kwenye,hapa ni penye siasa ,tunahitaji kampeni ya kuing,oa CCM Tanganyika na Zanzibar ,hata kama athari zake ni kufa kwa Muungano ,CCM lazima ing'olewe kwani akioza samaki mmoja wote wameoza ,kila anaebadilishwa anamshinda mwenziwe ,kwa sababu Watanzania tulioungana tumedharau msemo huo wa kuoza samaki au si kweli ,msemo ni mzito na unawahusu CCM ,kuanzia balozi wa nyumba kumi kumi mpaka rais wao wote hawafai,sasa kuelekea 2010 ni debe mtindo mmoja waondoke hakuna kubadilisha mawaziri wala kujiuzulu wote wakwapuke na kutafuta sehemu ya kujitajirisha lakini si serikalini.Serikali imewashinda . hawa CCM wanajaribu kuwapindisha watu kwa habari hizi na zile kwa ufupi wanawaweka wapinzani bize ili wao wajipange,kuna mambo haya yanayotokea tokea ,haya kama sikosei yanapangwa na CCM ili kuwashughulisha wabunge na vyama vya upinzani. Hivyo hapa ni debe tu mtindo mmoja. Fahamuni tu ukifa muungano na CCM ndio mwisho hivyo ,kwa utawala utakaokuja wote watanyea debeni ila kwa kusuguana nao kila siku na wao kubadilishana zamu tufika kiama hawang'oki.Na kama hamuamini jaribuni kupigia debe Serikali ya Tanganyika muone watakavyobabaika na wengine kuanza kukimbia nchi.

  Hivi hamuweki akilini ni kwa sababu zipi za msingi ikawa kukizuka tafrani za muungano wanakuwa mstari wa mbele ,si lolote isipokuwa kulinda maslahi yao na Chama chao,hakuna asikwambie mtu kuwa sijui Muungano umeanza hivi ,watu hivi..hakuna ni wizi tu wanajua njia za wizi zitakuwa finyu na wao hawatarejea tena katika wakati kama huu walio nao wa kufanya lolote lile na hakuna wa kuwaingili...hivi fikiria ikiwa moto wa kuidai Tanganyika utaibuka na Zanzibar nao watakuwa wanawaripuka kwa upande wao ,hamuoni picha watakayokuwa nayo mafisadi hawa..pakushika watakuwa hakuna ,watababaika kabisa kabisa ,lakini sasa wanafika kuweka vinasa sauti wanafika kumwaga unga wanafika kuamua matokeo ya uchaguzi wanavyotaka wao ,hivi hamuyaoni haya kuwa ni mambo ya kulinda maslahi yao ,mwananchi hana anacchokipata zaidi ya kudanganywa kwa kujengewa barabara na zahanati zisizokuwa na madawa ,mashule yasiokuwa na walimu ,mabilioni kwa mabilioni wanakwiba halafu hawahawa CCM wanarudi na kuwambia wananchi wajichangie kama si wizi ni kitu gani ? hIZI FEDHA ZINAZOIBIWA WANATWAMBIA ZINARUDISHWA ,zinarudishwa wapi kwa taratibu gani ?nani kati ya hao waliorudisha fedha wamefungwa ,wanaonekana mitaani kwa misingi gani mtu analiibia TAIFA halafu anaachwa apete mijini,mmeona nchi gani mambo haya kama sio hapa kwenye shimo la wezi,wizi mtupu walionao hakuna wanachokifanya ni kutudhalilisha tu kwa kuwa ni wao kwa wao ,kama wangekuwa na imani za kweli na TAIFA hili kusingekuwa na dhamana hata moja ,kesi za watu hawa si kesi sawa na kesi za kuiba kuku kwamba mtu awekewe dhamana hawa ni wahujumu wa Uchumi ,mambo wanayoyafanya ya kutafuta ushahidi ni kulindana tu hakuna jingine,hawa ni watu ambao serikali iliyopo madarakani inakula nao sahani moja hakuna jingine ni wamoja interest zao ni moja ,kuliibia Taifa na ndivyo wanavyofanya ,ni miaka mingapi tokea wizi ufanyike ni miaka mingapi kero za Muungano ni miaka mingapi wameweka mikataba isiyofahamika ,leo bado wanatuburuza na kutufanya mapunguani ,wanatuchezesha kwata au gwaride ,mheshimiwa umeshindwa Kuongoza na kila siku zikizidi ndivyo mnavyozidi kuboronga ,hatuendi mbele makesi ya wizi yote mnayazungulusha tu na kubabaisha watu ,yote washikaji wenzenu wamebakwa kwa wizi hivyo mnatumia kila mbinu kuwaokoa ili muendelee nao japo uraiani ,halafu mnatufanya wajinga kwa kutuambia ahusishwe mtu tu na sio serikali au Chama ,tukiwauliza Chama cheni kimewafanya nini watu hawa,serikali yenu imewafanya nini watu hawa ,haya mambo sio siri ,mnawatafutia mawakili ,hapa wakili hana mshiko katika kuliibia Taifa ,mtu anawekewa dhama ya Bilioni kibao asubuhi yake anaileta unafikiri atashindwa kuvuka wizi huo ? Wakitoka na kushinda kesi hizo mtawambia nini WANANCHI ?
   
  Last edited: Feb 7, 2009
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,598
  Likes Received: 18,601
  Trophy Points: 280
  Ndio hiyo inawezekana kwa sababu calculation ya life expectancy ni hesabu ya death rate at variance age groups wakilinganisha na birth rate na kutafuta avarage kwa kuoanisha na idadi ya watu. Kwa maneno Zanzibar hata kama haina death rate kubwa ya ukimwi, inaweza kuwa na high child mortalility rate inayopelekea idadi ya watu wanaokufa kwenye umri mkubwa kuwa ni ndogo zaidi ya jumla yao wote huku birth rate ikiwa ni ndogo.
  Life expectancy yetu ni kubwa kuwazidi kutokana mawingi wetu yaani asilimia ya vifo vyote ukilinganisha na wanaozaliwa na wanaokufa kwenye umri mkubwa, bara tumewapita sana wenzetu. Yaani tunaakufa sana, watoto wanazaliwa sana huku vizee vya bara haswa kwetu Usukumani, vinaishi sana.

  Wazibari ni wateke, shauri ya kuishi maisha laini. Wanaolewa mapema, wanazaa mapema na kuzeeka mapema. Mwanamke wa miaka 60 Zanzibar ni bibi zamani wakati hapa bara, waweza piga hodi. Idadi ya vifo vya umri mkubwa bara ni vingi kuliko Zanzibar kitu ambacho kimeishushia maksi Zanzibar.

  Ichi inayoongoza kwa maisha marefu ni Macau ikifuatiwa na japan kutokana na kuwa na vizee vingi, death rate na birth rate ni ndogo na idadi za watu ni ndogo. China inaongoza kwa idadi ya watuu, idadi ya wazee, idadi ya vifo, idadi ya vizazi lakini iko juu kutokana na wingi wao.
   
 4. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #4
  Feb 8, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Thanks Pasco for your nice explanations. I bet if student could capitalise on Jamiiforums surely their academic life gonna be so easy. This is both economically, socially, politically and academicaly as all these issues are critically addressed here.
   
 5. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #5
  Feb 8, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Ni kwasababu Zanzibar maisha ni ya tabu zaidi kuliko Bara na ningeshauri Wazanzibari wakaachiwa uhuru wa kujiendeleza zaidi kuliko wanaopewa sasa.
   
 6. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #6
  Feb 8, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Ukiangalia LE SSA ukimwi umechangia sana kufanya umri wa kuishi kushuka. Tafiti zinatuonyesha nchi kama Botswana, Swaziland LE ni miaka 40 tu kwa kuwa 25-30%ya watu wazima wameambikizwa tayari!

  Uliangalia takwimu kwa Tanzania 5.8% ndo pravalence wakati Visiwani ni less than 1%. Ndo maana nikauliza sababu zingine za Visiwani kuwa na LE kidogo zaidi kwa 10 years!
   
  Last edited: Feb 8, 2009
Loading...