Tofauti kati ya Wakenya na Watanzania

Tofauti kati ya Wakenya na Watanzania

Kiongozi bora ni yule alie karibu na wanachi wake ktk kuhakiki analinda mali za watanzania sasa hawa tulio nao watatufikisha huko tunakotaka ili tuweze gawana asilimali tulonazo kwa watu wote
 
Inawezekana kabisa kuikataa east africa ili kuokoa uchumi wetu. Kenya ni watu wabaya sana

Hamna nchi inayoweza kustawi bila kushirikiana na nchi nyingine..tatizo lipo kwa watanzania wenyewe munapotia mikataba ya kibiashara pamoja na ufisadi..lalamikia serikali yako ya CCM nakufanya marekebisho oct 25,bila hivyo utaendelea kutuchukia wakenya na sisi tutabaki kupaa
 
Sisi tunawekeza sana kwenye siasa, mambo ya biashara hayatuhusu; angalia tumeua viwanda na mashirika makubwa halafu tumeanzisha mikoa mipya na pia tumetangaza majimbo mapya ya uchaguzi. Tumefanya pia uwekezaji wa wilaya mpya za kutosha kabisa and hence tumeajiri wana siasa wengi na makada wa chama wengi tu wa kitosha, biashara ya nini kwetu?
 
Mkuu benki za Kenya hapa Bongo sio KCB na Equity tuu, zipo pia CBA (Kenyatta Family), I & M bank na NIC bank
 
Hamna nchi inayoweza kustawi bila kushirikiana na nchi nyingine..tatizo lipo kwa watanzania wenyewe munapotia mikataba ya kibiashara pamoja na ufisadi..lalamikia serikali yako ya CCM nakufanya marekebisho oct 25,bila hivyo utaendelea kutuchukia wakenya na sisi tutabaki kupaa

Hapo unafikiri kuna marekebisho mkuu. Bado tanzania hatujapata mpizani wa kweli bora nchi itawaliwe kijeshi
 
Kwa wakati huu tanzania haiitaji demokrasi hata kidogo bora kikwete nchi aikabidhi jeshi lakini siyo ukawa
 
Katufu
kwanza kabisa nikupongeze kwa analysis yako nzuri. Mimi kama mtanzania niliyeishi kenya kwa kama miaka 10 nilirudi nchini na kutafuta watanzania wenzangu wenye uchungu na jinsi nchi yao inavyozidiwa na Kenya katika almost kila kitu.
Pili, ningependa kuongeza hoja ya Kenya kuwa katika mstari wa mbele kupush for soko la pamoja la Afrika Mashariki ili makampuni yao yapate access to the Tanzanian market bila hata kuhangaika sana. Nawasihi sana waTZ mkikatae hiki kitu kwa nguvu zenu zote!
Inashangaza sana kuona serikali yetu kupunguza safari za KQ kwa ajili ya kampuni ya nje (fastjet) lakini walishindwa kufanya hivyo Air Tanzania walipokuwa wanauhitaji msaada huo.
Mwaka huu watanzania nawaombeni sana tuiondoe CCM lasivyo tutakuja kuwa maskini na kituko cha Afrika Mashariki. Takwimu zinaonyesha hadi miaka ya 80 waTZ walikuwa ndio wasomi wa Afrika Mashariki lakini sasa elimu ya Tanzania imedorora sana, all thanks to CCM!
Wanatuhadaa eti wanatujengea airport mpya. The new JKIA ina uwezo wa kuhandle wasafiri milioni 20 kwa mwaka wakati kiwanja chetu, pamoja na expansion inayoendelea, kitakuwa na capacity ya wasafiri milioni 7 tu! AIBU......msidanganyike waTZ tafadhali nimechoka kuitetea nchi yangu huku Nairobi!
 
Last edited by a moderator:
hivi unajua aliyeihujumu general tyre?
unajua wakenya wanaasilimia ngapi za umiliki wa kenya airways?
unajua uchumi wa mtu mmoja mmoja kwa wakenya?

Wakenya wanacheza smart games na Watanzania bado tumelala..

After Precision Airlines (PA) kuwa threat kwa operation za Kenya Airways (KQ) route za Tanzania na Kenya, KQ wakaingia ubia na PA very smartly na wakawa wanaihujumu undercover. Leo hii PA iko hoi na tayari Operations za Jomo Kenyatta-KIA, Jomo Kenyatta-Mwl. Nyerere zimerudi kwa KQ...

Pili, baada ya TBL kuruhusiwa kuuza bia Kenya, na Kenya walete bia zao Tanzania. TBL wakakaribia kuuwa bia za Wakenya huko kwao wakati huo bia yao TUSKER ikawa haifanyi vizuri hapa Tanzania. Wakavunja makubaliano, ili kila mtu afanye biashara yake kwake. After years EABL ya Kenya ikaingia ubia na SBL na wakaipa License ya kuzalisha na kusambaza TUSKER hapa nchini.. Smartly EABL wanauza hapa kwetu wakati sisi TBL haiuzi kule kwao..

Wakati hayo yote yanafanyika Watanzania tunalazwa na fikra za kijinga za viongozi wetu wa CCM.. Education Matters alot

2004 Tanzania tulikuwa na Ndege mbili za serikali (Air Tanzania) na Kenya walikuwa na Ndege 19 (Kenya Airways-KQ)..
2015 Tanzania tuna Ndege 1 ya kukodi kwa ajili ya kupigia Kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Kenya wana Ndege 47 zinazotua katika viwanja 62 vya mabara yote duniani...

Tukumbuke bila kuwa na Shirika letu la Ndege Utalii tunaongelea ni kazi bure..

Kenya taratibu inautawala Uchumi wa Tanzania, tayari wana Bank mbili zinazofanya kazi nchini (KCB and Equity Bank), Tanzania bado hatuna Bank yeyote Kenya.

Supermarkets za Kenya tayari zimeingia nchini na kuuwa zetu (Nakumat tayari imeshainunua Shoprite (T), UCHUMI Supermarkets).. Sisi Imalaseko Supermarkets zilishakufa kule Kenya.

Soko la Hisa Dar Es Salaam (DSE) lina Jumla ya Kampuni 21, kati ya hizo Kampuni 7 ni za Kikenya lakini Soko la Hisa la Nairobi (NSE) lina zaidi ya Kampuni 64 na hakuna kampuni hata moja ya Kitanzania.. Hii ni mbaya sana kiuchumi..


Serengeti National Parks ni mbuga bora iliyoshika namba moja kwa Afrika, na Ngorongoro ikiwa namba 5.. Masai Mara ya Kenya ni namba 8. Lakini pia Tanzania tuna Mlima Mrefu zaidi Afrika Mlima Kilimanjaro ambao pia ni kivutia kikubwa cha Utalii..

Lakini maajabu ni kwamba Kenya wanakusanya pato kubwa sana kwenye Utalii kuliko Tanzania. Mwaka 2013 pamoja na matukio ya kigaidi Kenya ilitembelewa na watalii million 1.4 wakati Tanzania yenye amani tele ilitembelewa na watalii million 1.04.. Amani wanayoihubiri CCM na vivutio vyetu vya Utalii bado havijatufaidisha chochote..


Pato la Mtanzania kwa mwaka ni Tshs. 1,996,000 na Pato la Mkenya kwa mwaka ni Tshs. 3,176,000..
Pato la nchi (Tanzania) ni Tshs. Trillion 98.36 na Pato la nchi kwa Kenya ni Tshs. Trillion 140..


Tanzania kuna madini ya kila aina, Tanzanite, Dhahabu, Rubi, Uranium, Makaa ya Mawe, Chuma, Kenya hawana madini ya aina yeyote lakini bado wametuzidi pakubwa kwenye pato la Taifa.. Sekta ya madini inachangia 3.3% kwenye pato la taifa kutokana na mikataba mibovu uliyowekwa na viongozi wa CCM..

Kiwanda cha General Tyre cha Arusha kilikuwa kinazalisha TYRE bora kabisa za kazi. Kilikuwa na Soko kubwa Afrika Mashariki na kati. Gari zote za Tours zinazotembea porini Afrika Mashariki yote na Afrika ya Kati zilikuwa zinafunga TYRE ya GENERAL. Hata wale wapigana vita za msituni huko Kongo na Sudan walikuwa hawaendi kupambana bila kuhakikisha Land Rover yake imefungwa Tyre ya General. Magari ya serikali yote yalikuwa yanafunga Tyre ya General..

Kiwanda kilikuwa kinalipa kodi isiyopungua Billion 100 kila mwaka.. CCM wakafanya hujuma kukiua, zinatolewa subsidy zinaishia kwenye matumbo yao. Wakenya walivyosmart wakaiba ile Technology ya Tyre za General wakafungua kiwanda chao huko kwao kikaitwa YANA Tyre ambaye sasa ndiye Supplier mkubwa wa Tyre Afrika Mashariki na Kati..

Kampeni zinaanza wamejifanya kuifufua General Tyre, Je, wataweza kupambana na Yana Tyres?? Kenyans are always SMART kuliko akili za CCM

CCM wanasema hapa ni Kazi tu.. hahaha

 
Pamoja na kukubaliana na baadhi ya facts ulizotumia kwenye hoja zako lkn sikubaliani na mantiki na ulinganifu unaotaka kujenga.

Kwanza uzi wako unaanza kwa kuonesha tofauti ya Wakenya na Watanzania, lkn unamalizia na kuonesha tofauti kati ya Wakenya na CCM. Hapa umeniacha kinywa wazi. Sijajua ulitaka kuonesha uduni wa Watanzania dhidi ya Wakenya au jinsi CCM ilivyoshindwa kuleta maendeleo kama ya Wakenya? Kama hoja yako ni kuhusu uduni na unyonge kwa Watanzania ushindwe na ulegee kabisa.

Kama ulitaka kuponda CCM hapo nakuunga mkono lakn ni vizuri pia kuwa mwangalifu kwa kutokumia takwimu pekee bila kuzichambua. Kwanza, ulipaswa ku-acknoledge tofauti ya uchumi wa Kenya na Tanzania kuwa hazijaanza leo!!!!
Pili, ulipaswa uangalie maendeleo ktk maeneo mengi kwa mfano, pamoja na per capita income, ulipaswa pia uzungumzie ukuaji wa uchumi baina ya nchi hizi. Ni ipi inafanya vizuri?

Lkn kitu kingine ulipaswa uangalie structure ya uchumi wa nchi hizi. Tanzania inategemea nini ktk kukuza uchumi na Kenya inatagemea nini, na comparative advantage ya kila nchi pamoja na mazingira yake.

Lkn pia si vibaya kama ungetafsiri unafuu wa mtu mmoja ktk nchi hizi ukilinganisha na uwiano wa chumi za nchi hizi.

Hizi habari za kuwa mnatumika bila kujijua kwa propaganda za kuiabudu Kenya dhidi ya Tanzania hazikubaliki.

Ni kweli kwamba wengi humu tunataka mabadiliko sasa kwa kuindoa CCM lkn pia si vizuri kutuaminisha kwamba sisi Watanzania hakuna chochote tunachofanya vizuri au kwamba Kenya hii hii ninayoifahamu mimi ni nchi ya ajabu sana duniani kwa kila kitu na kwamba Tanzania ni kinyume chake.
 
hayo yatawezekana vipi kama wafanyabiashara wakubwa hawataki kulipa kodi kwa kujihusisha na siasa? angalia kwenye ishu ndogo tu biashara ya mbao na mkaa watu wanakwepa utaratibu na sheria zilizopo kuokoa miti yetu kwa kupata kibali lakini watz tumeendelea kufanya vitu kinyume huku tukilalamika hatuendelei, tukibadili akili zetu tutakua mbali, tunainyima serikali mapato halafu tunalaumu timiza wajibu dai haki
 
We mleta mada ona sasa umesababisha mpaka vidonda vya tumbo vimeanza kuuma. Unasema ukweli bila kuumauma?? Watanzania hatupendi hivyo. Tunapenda kusifiwa tu na tunapokesea waziwazi tuambiwe bahati mbaya. Na bado Wakenya watatuburuza sana mpaka tuache ujuha.
 
Halafu waliotufikisha hapo wanapanda majukwaani na wanatuita WAPUMBAFU TENA MALOFA eti wametuletea tingatinga tulichague waendelee kututukana maskni nchi yetu TANGANYIKA
 
Back
Top Bottom