Tofauti kati ya Simba, Yanga na Azam katika Picha.


M

Masuke

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2008
Messages
4,609
Likes
139
Points
160
M

Masuke

JF-Expert Member
Joined Feb 28, 2008
4,609 139 160
Hapa chini ni kocha mpya wa Simba akikagua uwanja wa mazoezi unaotumiwa na timu hiyo.


Na hizi picha hapa chini ni vijana wa Yanga wakiwa mazoezini.

Chini ni kocha mpya wa Azam akiwa anatambulishwa kwa wachezaji katika uwanja wao ambao hutumika pia kwenye baadhi ya mechi za ligi kuu.

Kwa haraka haraka ukiangalia hizo picha unaweza kujua kwamba Timu ya Azam inashiriki ligi kuu na zingine ni timu za mtaani au timu za shule kwa ajili ya mashindano ya UMISETA.

Kwa kweli kuna kila sababu ya Simba na Yanga kutengeneza japo pitch kwa ajili ya mazoezi, bora wenzetu Yanga uwanja wao wenyewe wa mazoezi wanao japo ni mbovu sasa kichekesho ni wenzangu na mimi wa pale msimbazi kila siku tunaambiwa uwanja uko Bunju sijui kwa nini wanashindwa kutenga japo milioni mia moja kila mwaka ili kuboresha japo pitch na facilities zingine ili kama inawezekana timu inaweka kambi huko huko wakati inajiandaa na mashindano.

Uongozi ukiamua ni rahisi sana, maana wanahitaji kuwa na kitu kama hostel ambayo inawezakuwa na vyumba kama 30 kwa ajili ya kulala, sehemu ya jiko, sehemu ya mazoezi kwa maana ya gym, sehemu kwa ajili ya mikutano pamoja na kufanyia mafunzo kwa nadharia, wakiamua ni rahisi sana, ni suala la kutenga japo milioni mia tu kila mwaka na baada ya miaka kama kumi watakuwa na uwanja wao wa mazoezi na hostel ambayo inaweza kuwa ni bora sana.
 
Utingo

Utingo

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Messages
7,239
Likes
333
Points
180
Utingo

Utingo

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2009
7,239 333 180
Azam is a football team...Yanga na simba ni aibu. Kwa zaidi ya miaka 60 timu bado ziko katika mazingira haya.....??!!
 
B

bujashi25

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2013
Messages
623
Likes
40
Points
45
B

bujashi25

JF-Expert Member
Joined Jun 17, 2013
623 40 45
Lakini cha ajabu huwa anaambulia kipigo kutoka kwa hizo timu zisizokuwa na viwanja japo vya mazoezi sijui tatizo huwa ni nini hasa!
 
M

Masuke

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2008
Messages
4,609
Likes
139
Points
160
M

Masuke

JF-Expert Member
Joined Feb 28, 2008
4,609 139 160
Lakini cha ajabu huwa anaambulia kipigo kutoka kwa hizo timu zisizokuwa na viwanja japo vya mazoezi sijui tatizo huwa ni nini hasa!
Mkuu ni kweli kwamba huwa anapokea vipigo lakini si mara zote, angalia mechi za mzunguko wa kwanza msimu huu, Yanga kanyolewa mara moja, Simba naye kanyolewa mara moja na wote wawili kinyozi wao ni Azam, huwezi jua labda mwanzo wa faida ya kuwa na kiwanja kizuri na facilities zingine za kwako mwenyewe ndo unaanza sasa.

Anyway tuachane na hayo, hoja kubwa iliyopo ni je kweli hizi timu zetu kongwe hazina uwezo wa kutengeneza hata pitch tu kwa ajili ya mazoezi? hadi watumie viwanja vya kukodi kila mwaka?
 
Amavubi

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Messages
30,043
Likes
5,227
Points
280
Amavubi

Amavubi

JF-Expert Member
Joined Dec 9, 2010
30,043 5,227 280
tofauti ziko nyingi sana. historia ya timu hizi, wamiliki, uanachama etc
 
B

Baba Kiki

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2012
Messages
1,461
Likes
568
Points
280
Age
41
B

Baba Kiki

JF-Expert Member
Joined May 31, 2012
1,461 568 280
Kusema ukweli ni aibu sana Simba na Yanga kutokuwa na japo kijiwe cha kufanyia mazoezi. Huwa najiuliza hivi ikiwa kila shule ya msingi ina kiwanja chenye nyasi na magoli inakuwaje kwa Simba? Haiingii akilini uanze kufikiria uwanja wa mabilioni ya shilingi wakati huna hata eneo tu lenye magoli na nyasi.

Yanga nao wanashindwa kuotesha nyasi tu wakati uwanja wanao, hii nayo ni zaidi ya ajabu

Viongozi wa timu zote waache habari za kufikirika, waanze kufanya kazi kwa vitendo kidogo kidogo
 
CHAI CHUNGU

CHAI CHUNGU

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2012
Messages
7,139
Likes
121
Points
160
Age
39
CHAI CHUNGU

CHAI CHUNGU

JF-Expert Member
Joined Feb 20, 2012
7,139 121 160
Mkuu Masuke mie nilichogundua kwenye hizo picha ni kocha wa simba kama anashangaa na kutoamini kama simba ipo ligi kuu au ni zile timu za diwani cup?
 
Last edited by a moderator:
Kuntah Kinte

Kuntah Kinte

Senior Member
Joined
Oct 25, 2013
Messages
134
Likes
19
Points
35
Kuntah Kinte

Kuntah Kinte

Senior Member
Joined Oct 25, 2013
134 19 35

Mshambuliaji wa timu ya Kilimanjaro Stars, Edward Christopher akikokota mpira wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Kampala Kampasi ya Biashara nchini Uganda leo kujianda na mchezo wa kesho dhidi ya Sudan Kundi B, michuono ya Tusker Challenge.
 
K

Konaball

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2009
Messages
2,444
Likes
1,012
Points
280
K

Konaball

JF-Expert Member
Joined Mar 11, 2009
2,444 1,012 280


Angalia na tofauti hii pia
 
K

Konaball

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2009
Messages
2,444
Likes
1,012
Points
280
K

Konaball

JF-Expert Member
Joined Mar 11, 2009
2,444 1,012 280


Kocha anawasili uwanja wa kinesi katika mazoezi
 
M

Masuke

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2008
Messages
4,609
Likes
139
Points
160
M

Masuke

JF-Expert Member
Joined Feb 28, 2008
4,609 139 160
Mkuu Masuke mie nilichogundua kwenye hizo picha ni kocha wa simba kama anashangaa na kutoamini kama simba ipo ligi kuu au ni zile timu za diwani cup?
Mkuu kinachotusumbua mashabiki wa hizi timu ni kwamba zimekuwa kama sehemu ya maisha yetu lakini kiukweli ni aibu sana kuwa na timu zenye rasilimali za mashabiki halafu unatumia viwanja vya kukodi kila mara angalau basi wangekuwa wanakodi viwanja vyenye ubora, viwanja vyenyewe wanavyokodi ni vibovu bora kiwanja chetu cha kijiji au cha shule yetu ya msingi.
 
Last edited by a moderator:
M

Masuke

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2008
Messages
4,609
Likes
139
Points
160
M

Masuke

JF-Expert Member
Joined Feb 28, 2008
4,609 139 160
M

mokala1989

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2013
Messages
2,248
Likes
57
Points
145
M

mokala1989

JF-Expert Member
Joined May 4, 2013
2,248 57 145
azam is a football team...yanga na simba ni aibu. Kwa zaidi ya miaka 60 timu bado ziko katika mazingira haya.....??!!
kocha wa simba anaonekana kuchoka gafla, hata timu yangu yanga ni majanga, mwanachama no. 1 wa yanga upo wapi? Au namba moja ilikufa na nyerere?
 
Kitoabu

Kitoabu

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2011
Messages
5,764
Likes
185
Points
160
Kitoabu

Kitoabu

JF-Expert Member
Joined Jul 7, 2011
5,764 185 160
Lakini cha ajabu huwa anaambulia kipigo kutoka kwa hizo timu zisizokuwa na viwanja japo vya mazoezi sijui tatizo huwa ni nini hasa!
Napata tabu kuamini kama wewe nimfuatiliaji wa soka letu hapa Bongo. Azam nitimu kati ya timu mbili ambapo mpaka unamalizika mzunguko wa pili bado haijapoteza mchezao wowote. Azam ndio timu pekee ambayo imezifunga timu hizo kongwe (Yanga na Simba) Katika mzunguko wa kwanza uliomalizika. Yanga alifubgwa 3-2, huku Simba ikifungwa 2-1. Sasa unanishangaza unapo lopoka eti "japokua Simba na Yanga hazina viwanja lakini ndio kilasiku zinamfunga Azam" nashindwa kukuelewa.
 
Kitoabu

Kitoabu

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2011
Messages
5,764
Likes
185
Points
160
Kitoabu

Kitoabu

JF-Expert Member
Joined Jul 7, 2011
5,764 185 160
Yanga na Simba bado wapo kwenye analogy wakati sisi (Azam) tupo digital.
 
Okhondima

Okhondima

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2013
Messages
1,060
Likes
288
Points
180
Okhondima

Okhondima

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2013
1,060 288 180
Lakini cha ajabu huwa anaambulia kipigo kutoka kwa hizo timu zisizokuwa na viwanja japo vya mazoezi sijui tatizo huwa ni nini hasa!
Mkubwa,mpira unaangaliaga kweli?

"Nlikuwepo":bolt:
 
L

lifeline

Member
Joined
Sep 10, 2013
Messages
64
Likes
1
Points
0
L

lifeline

Member
Joined Sep 10, 2013
64 1 0
[SIZE=4[/SIZE]Azam ikacheze ligi ya mafuta Qatar..timu gani bila ya wanachama au ya kumfurahisha the big boss
 
Maundumula

Maundumula

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Messages
7,050
Likes
90
Points
145
Maundumula

Maundumula

JF-Expert Member
Joined Nov 4, 2010
7,050 90 145
Private property is always more productive.

Unawaambia Yanga na simba waweke milioni 100 halafu makomandoo watakula nini?

Dawa ya Yanga na simba ni sisi washabiki kususia kuziacha zife kibudu halafu kila watu waanzishe timu huko mitaani kwao. Kinondoni Worriors, Temeke United, Singida combine nk halafu uone tutakavyopiga hatua katika soka.
 
Maundumula

Maundumula

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Messages
7,050
Likes
90
Points
145
Maundumula

Maundumula

JF-Expert Member
Joined Nov 4, 2010
7,050 90 145
Kila mara huwa wanadaiwa na wenye mahoteli , hivi basi la Simba lilishaachiwa?
 

Forum statistics

Threads 1,250,719
Members 481,468
Posts 29,743,134