Tofauti Kati ya roho mbaya na roho nzuri

Tofauti Kati ya roho mbaya na roho nzuri

Tuchki

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2017
Posts
1,740
Reaction score
1,446
Habari za leo ndugu zangu,hongereni Kwa majukumu.
Kuna Jambo huwa linanitatiza tangu nikiwa mtoto mpaka umri huu wa kuitwa mtu mzima hivyo ningependa kuwashirikisha.
Hivi roho mbaya ni kitu gani inakuaje mtu anaambiwa ana roho mbaya na mwingine anaambiwa ana roho nzuri.

Kwa mfano kwenye maisha yangu nimechunguza na kugundua asilimia kubwa mtu akifanya jambo la kufurahisha nafsi yake au akishindwa kumsaidia mtu jambo ambalo lipo nje ya uwezo wake watu husema kua mtu huyo ana roho mbaya.

Vile vile kuna Ile hali ya kuweza kufanya jambo jema Kwa mtu Kwa muda mrefu lakin siku mkiwaruzana kidogo mtu yule yule atasema kuwa Fulani ana roho mbaya ama atasema kuwa wewe ni mbaya.

Pia Kwa upande mwingine huwa nasikia kuna watu wenye roho nzuri ambao wakifanya mambo huwa wanasifiwa Na kupendwa mno sijajua moja Kwa moja hawa huwa wanafanya mambo gani mpaka kupewa sifa hizo kwani mengi huwa yanafanywa sirini.

Najua humu tupo wengi na baadhi yetu tumewahi kuambiwa kua tuna roho nzuri pia kuna tumeambiwa tuna roho mbaya, naomba tuchangie mada hii tukitoa mifano na mazingira ambayo mtu uliwahi kuitwa una roho mbaya ama kuitwa una roho nzuri na ikitokea umeitwa moja ya jina hilo huwa unajisikia vipi, pia unaweza kua uliitwa/unaitwa majina yote tajwa kati ya hayo unaweza pia kutoa mchango,ili tuweze kujifunza na kukabiliana na changamoto tuzipatazo kutoka Kwa jamii.








Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mambo yote ya ajabu duniani yapo Africa Mkuu.

Wakati Roho ikiwa ni kitu ambacho hakionekani( It is just a myth)... Waafrica ndo watu pekee duniani wenye kujua huyu ana roho nzuri na huyu ana roho mbaya.


Kama mtu anafanya mambo mema/mazuri why tusiseme ana tabia/mambo mazuri? Why roho nzuri?😎
 
Watu wenye roho mbaya wapo,na wenye roho nzuri wapo.Pia wapo wanaosingiziwa tu hizo sifa zote mbili.
Ni topiki nzuri.Nitatoa tu maoni yangu,nionavyo mimi.Mtu mwema ni yule ambaye hakumbuki mema anayotenda kwa wengine,bali hukumbuka yale mabaya au makosa,hata ya bahati mbaya aliyotenda kwa wengine.Mtu mwema hazingatii jema afanyalo.Mara nyingi hulisahau haraka au hujisahaulisha haraka kadri iwezekanavyo ili isije ikamti kiburi.Si kazi rahisi lakini.

Pili,hata utende mema kiasi gani,si kila mtu ana shukrani au kuridhika.hutakosa watakao kuchafua kwa wema huo huo.leo tuna watu wengi wameshaathirika,ama kwa kusikia,kushuhudia au hata kuwakuta,ya binadamu kusahau au kukosa shukrani,hadi wameamua kupooza ama kurudi nyuma katika kutenda wema,hata wa kawaida tu.Wameamua kuwa mabandidu wa chini chini,wakitoa sana sana huduma ya mdomo tu.Hili ni baya sana,ubinafsi na silka ya kuhukumu.Si kila binadamu hana shukrani na huwezi kuwajua kwa kuwasoma tu.Na,sidhani ni sahihi sana kutaka utende wema kwa wenye shukrani tu,hutatofautiana sana na shetani.

Tatu,kuna mambo kadhaa yanazunguka katika utendaji huo huo wa wema ambao ama hufanya wema uwe na athari nzuri kwa mtendewa au kinyume chake.Mfano,kutenda wema kwa binadamu mwenzako,lakini ukionyesha kutomheshimu na kumthamini (labda sababu ya uhitaji au hali aliyonayo),kukosa kuwa makini (insensitivity) juu ya hisia zake mhitaji wema kwa kujisifia wema uutendao kwake au kutangaza shida za huyo mtendewa wema kwa watu kiholela.Haya na mengine meengi ya namna hii,hulowesha nguvu na umaana wa wema woote uufanyao,labda umkute mtu huyo mtendewa wema,naye ni mwema kwa asili kiasi ya kama akaamua kutoangalia ubaradhuli wa mtenda wema na kuzingatia,kuthamini,kujali na kukumbuka utatuzi ulioupata tu kwa mtenda wema kwake,japo baradhuli.Na wapo watu wa namna hii.

Utaona katika hili hapo juu,wapo wanaotenda wema sana,ila wanalalamika kuwa watu hawana shukrani au wanalalamikiwa sana,licha ya wema wao.Kama awatendeao wema si washenzi,ukichunguza sana utagundua ni wale watendao wema kwa ajili ya nafsi zao.yaani kutaka sifa tu si utatuzi wa shida za watu,kuanika shida za wengine kiholela...kifupi,wema wao ni kwa ajili ya matumizi yao binafsi ambayo ni mabovu mno.Hawawezi kuona uharibifu wanaoufanya kwa wanaowatendea wema ilimradi anaamini anatenda wema na hilo tu latosha kudai ama kutarajia shukrani.Wengi wa namna hii ni wabwatukaji holela kutaka sifa na heshima za bei rahisi kwa kudhalilisha wahitaji.

Lakini pia,wapo wema wanaojua namna ya kuutenda wema kwa misimngi ta utu,imani na uelewa.Hawa huutenda bila kuweka sifa au majivuno yao mbele.Siri za mhitaji atazizingatia,atajitahidi kuonyesha staha,heshima,utu na kujali kwa wahitaji,hata wawe duni kihali mbele zake.Japo hata wema wa namna hii,wakikutana na wanaohitaji kutendewa wema ambao wenyewe ni mafedhuli,ila wanajifanya wanyonge na wapole kipindi cha uhitaji tu,nao usishangae kukumbana na kulaumiwa,kusemwa vibaya n.k. licha ya wema wao wote huo tena uliojaa umakini.

Nne,wakikutana mtenda wema wa aina ile ya awali,ya kupenda sifa zaidi,kutojali wala kuthamini kwa anayemtendea wema,huyu akikutana na baradhuli mhitaji wema ambaye kwa sasa ni uhitaji tu unampeleka kwa huyu mtu,hata akishatimiza haja zake,ni dhahiri matokeo yanajulikana.Ni kulalama,kulaumu,kushutumu na hata kumtusi mtenda wema baradhuli mwenzake.

Tano,wakikutana watu wa aina inayofanana,yaani mtu mwema na mwenye staha,utu,ubinadamu,heshima n.k. kwa mhitaji wema ambaye naye,licha ya uhitaji,ila ana asili ya wema na shukrani,hapa matokeo yanabashirika.Ndio utakuta hadi wajukuu wanakuja kuheshimiana sababu ya hawa wawili.

Mwisho,wema si kitu cha mjadala.Usitende wema ukitaraji shukrani au malipo fulani ama kuonyesha hilo,japo kibinadamu msukumo huo ni mkubwa.Tenda wema kwa mtu huyu,akimaliza shida zake,wala usitazame anakoelekea.Mungu atakuletea mwingine kabisa (siku ya uhitaji kama itatokea),na utashangaa unatendewa wema mara dufu zaidi ya ulioutenda kwa wengine kabisa.Ukisubiri ama kungoja au hata kufuatilia kwa uliyemtendea wema,hapo ndipo shida,kivumbi na matatizo yatakapoanza si ajabu,japo si lazima.Wema una thawabu.uhitaji wa watu nauona ni mtego na mtihani wa Mungu.Ukiweza kuutenda wema sawa sawa,bila kungoja shukrani,kutaka sifa (hii hufuta thawabu ya Mungu,hata ukitenda wema) sio tu mtendewa wema atauona toka usoni na rohoni mwako na atakuheshimu na kukujali kirahisi akiamini huna matarajio makubwa mno toka kwake hadi yamtishe,bali Mungu hulipa wema kwa namna sahihi zaidi ya tonavyotamani au kutarajia,ila mara nyingi,si kwa kupitia uliowatendea wema.

Isijalishe utalaumiwa,kukumbana na msururu wa wasio na shukrani,matusi au hata hasara,kutenda wema si kitu cha kukiacha au kukatishwa tamaa.Hailipi na haijawahi kulipa kukwepa kutenda wema.Utatendea wema watu kumi,tisa hawatakuwa na shukrani kabisa kwako,lakini mmoja tu aweza kuja kukuonyesha shukrani kubwa kupita hao kumi,mara dufu ilimradi uliutenda wema kwa namna sahihi.
Njema zaidi,shukrani hapa duniani waweza ipate kwingine kabisa,si kwa uliotendea wema.
Hatutendi wema ili tusikie tukisifiwa au tushangae tukilaumiwa licha ya wema tulioutenda.Ukiwa mtu wa kusikilizia matokeo ya mema uyatendayo,ni dalili kuwa wewe si mtu mwema,ila mfukuzia sifa za wema.MTU MWEMA HAKUMBUKI MEMA YAKE,ILA MABAYA AYATENDAYO KWA WENGINE.Usipokumbuka mema uliyoyatenda,hutasumbuliwa na kelele za watu wasio na shukrani na uliowatendea wema kwani,hutaona kama zinakuhusu sana.
 
wewe unafikiri kutoa ni Kazi ndogo?
Wacha tu waitwe roho nzuri wenye kutoa coz ni kitu ngumu sana
 
Back
Top Bottom