Tofauti kati ya Nguvu ya umma na Uhaini

MwanaIFM

Member
Nov 20, 2010
42
27
Jamani wanaJF ninaomba mchango wenu, kwa uelewa wangu nimefikiri na kujaribu kutofautisha mambo haya mawili.Kwa tafsiri yangu na uelewa wangu vitu hivi vina maana:-
1.People’s power/Nguvu ya umma:Ni maandamano ya kisiasa yasiyokua ya fujo wala umwagaji damu yanayohusu wananchi, haswa wakiongozwa na vyama vya wafanyakazi ambapo huhusisha aina mbalimbali ya “protests” na “ demonstrations” ili kushinikiza serikali iliyopo madarakani kutekeleza mambo Fulani.Na historia inaonyesha vuguvugu za namna hii zilianza kupata umaarufu mkubwa baada ya mafanikio ya mwaka 1986 huko Phillipines (EDSA Revolution of 1986). Na hii japokua huhesabiwa kama mapinduzi ya kisiasa lakini huwa hayahusishi “direct confrontation” kati ya vikosi vya usalama na hao waandamanaji.Bali hujikita zaidi katika kupaza sauti ambazo ingekua bila umoja huo zisingesikika.
2.Treason(Uhaini),Uasi(Rebellion) ,Armed revolution(Kama kule Zanzibar 1964): Hii ni aina nyingine ya namna wananchi wanaweza kuiondoa serikali iliyopo madarakani kwa kutumia nguvu na aina hii huhusisha umwagaji mkubwa wa damu na mara nyingi huwa haikubaliki kisheria.
Sasa mimi ninaposhindwa kuelewa ni jinsi watu wengi(Pengine hata mimi) tunaposhindwa kutofautisha kati ya vitu hivyo viwili na mifano mizuri ni Tunisia na Misri kwa aina ya kwanza na kile kinachoendelea huko Libya sasa hivi ambapo mimi nadhani waLibya wanaangukia katika aina ya pili ambayo si kitu kizuri sana au kinachofaa kushabikiwa.
Kazi kwenu wakubwa niko tayari kurekebishwa kama nimekosea katika kutofautisha “Scenario” hizo mbili, madhumuni yangu ni kujifunza zaidi kuliko kulumbana.
 
Back
Top Bottom