Buntungwa
JF-Expert Member
- Oct 29, 2010
- 549
- 310
Wakuu habar za jioni,
Poleni na majukumu ya kutafuta pesa,"tujadili haya maneno 2 MAPENZI na UPENDO
Nijambo ninalojiuliza kwa mda kidogo tofauti ya MAPENZI na UPENDO
MAPENZI ni matamanio ya mwili, tendo la kufanya mapenzi, mnaweza mkawa na mapenzi bila upendo, watu wengi wanaangaika na MAPENZI hawapo kwenye upendo.
Mfano: Mwanaume anamuangalia mwanamke na kutamani kufanya nae MAPENZI tu, ena akimuona mwanamke mwenye makalio makubwa, mguu wa bia au mwanamke chuchu saa 6 na kadha wa kadha hapo ni mapenzi ndio yanamsukuma hakuna UPENDO.
Mwanamke ametawaliwa na mapenzi anasema namtaka mwanaume mwenye 'six packs', gari zuri, mrefu and so so hapo ni mapenzi yametawala hakuna UPENDO.
Kuna watu wengi hawajawahi KUPENDANA ni MAPENZI tu ndio yamewaunganisha, MAPENZI ni tendo na tamaa ya mwili,J E mapenzi yakiisha kitaendelea nini?
MWANAMKE
Ndio maana ukijua leo unaenda kukutana na mtu wako unakamia sana unaangaika sana, utajipamba haswa hata kama huna pesa ya salon utakopa ili upendeze. Utaweka vitu sehemu za siri ili ukamnogeshe jamaa hapo hakuna UPENDO hayo ni mapenzi, kwenye upendo hakuna mbwembwe.
MWANAUME
Akijua anaenda kukutana na mtu wake anakamia haswa mara anywe supu ya pweza,mara udongo wa congo,atumie dawa za kuongeza uume au nguvu za ume hapo hakuna UPENDO unawaza mapenzi tu.
Tunatumia nguvu kubwa kutengeneza MAPENZI tunakosea sana inabidi tutumie nguvu na akili zetu zote kujenga UPENDO.
UPENDO
Kwenye UPENDO kunabaraka nyingi sana, kwenye upendo hakuitaji mpaka utumie vumbi la Kongo kwani mambo yatajiseti yenyewe. Kwenye UPENDO unajenga urafiki ambao hamta ogopana, mtaongea, mtacheka, mtafurahi na kila kitu kitakuwa sawa.
Kwenye upendo hakuna kukashifiana mara oooh huyu anakibamia au huyu anarambo au unamuona mwenzio mbwa,au unamuna kama mwanaume mwenzio au mwanamke mwenzio.
Jiulize uko kwenye MAPENZI au UPENDO.
Nawatakia Jioni njema. Povu ruksa.