Tofauti kati ya kupendwa na kuonyeshwa mapenzi

Tofauti kati ya kupendwa na kuonyeshwa mapenzi

Mdharuba

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2011
Posts
824
Reaction score
522
Habari wanajamvi,

Naomba nieleze (japo kwa ufupi) tofauti iliyopo kati ya kupenda na kuonyesha mapenzi.Ni ukweli ulio wazi kuwa wanaume tulio wengi sana tunajikuta tukidanganyika kirahisi mikononi mwa wanawake. Wanawake haswa wale wanaojua haswa mbinu na njia sahihi za kumdaka mwanaume anayemtaka awe kwenye himaya yake.

1.KUPENDWA
Japo ulimwengu umevurugika kwa sasa kwakuwa asilimia kubwa ya wanawake wanaongozwa na tamaa, lakini bado wapo wanawake ambao wanapenda-wana mapenzi ya kweli haswa.

(i) Wanawake hawa mara nyingi huwa wako tayari kwa chochote utakacho wewe mwanaume na wanajitolea kwa mambo mengi sana kwa ajili yako.

(ii) Wana uwezo wa kuona uhalisia wa mambo, wanaelewa maisha halisi yalivyo i.e kuna kupata na kukosa!! Hawawezi kukupa lawama kwa kukosa kwako zaidi watakutia moyo ili uendelee kutafuta zaidi.

(iii) Wanawake hawa hawana demand ya vitu vikubwa ambavyo anajua kabisa viko nje ya uwezo wako, kinyume chake atakupa support kubwa sana na kukusaidia hata kifedha( kama ana nafasi) kwa kutambua umuhimu wako kwake.

(iv) Wanawake wanaopenda ni wepesi kusamehe. Yaani pale unapomkosea na kumuomba msamaha huwa hawajiulizi mara nyingi au wakachukua siku 7 bado amenuna, naomba nisisitize hapa kuwa haijalishi kosa ni kubwa kiasi gani, lakini wanawake wanaopenda wanajua maana halisi ya neno samahani.

(v) Wanawake wanaopenda huwa wako open sana, anaeleza kila hatua ya maisha yake na anayoyaendea. Hawa huwa hawana usiri kwa namna yoyote ile.

(vi) Wanawake hawa pia huwa wanaheshimu unachokifanya, hata unapomwambia "niko busy" anaelewa haswa maana halisi ya wewe kuwa busy na anatambua nafasi ya unavyovifanya katika maisha yenu.

(vii) Jambo la kupigwa faru(kugegedwa) huwa anapenda zaidi liwe katika wakati maalum kwa sababu huwa hana hofu ya kukupoteza sababu moyoni mwake uko peke yako.

2. WANAONYESHA MAPENZI
Hawa ni wale pretenders ambao mara nyingi huwa wanakuwa na wanaume zaidi ya mmoja, huyu ni rahisi sana kumgundua kama uko makini, lakin kama hujayajua vizuri mapenzi ni rahisi sana kudanganyika. Sifa zao ni kinyume na wale tuliowataja hapo juu.

(i) Wanasumbua sana, anahakikisha anakuweka busy siku nzima.. Kama wewe ni wa kuchat basi atakuchatisha masaa yote na kama wewe ni wa kuongea kwenye simu basi utaongeleshwa sana. Unaweza kujikuta unashindwa kuhudumia mtu ofisin kwako uko busy unajibu msg zake, na ukichelewa kidogo tu utaona sms "Mbona kimya?".

(ii) Wana wivu saaaanaaa.. Yaani yeye muda wote anajifanya anakuhitajia, hata ukiwa unaongea na wazee wako kuhusu mambo ya kifamilia yeye akikuta simu inatumika basi ugomvi.

(iii) Huwa wanatanguliza sana kuuliza nafasi zao kwako "Baby, hivi mimi nina nafasi gani kwako?" Hili swali mara nyingi linakuja hata pale unapomwambia kuwa hutakua nae leo labda utakua somewhre na rafiki zako, au utaondoka kikazi au woteva. Kuwa makini sana, maana swali hili analiuliza huku anahuzunika.

(iv) Waonyeshaji mapenzi huwa hawajutii machozi yao. Yaani hawa ni wepesi sana kulia, kitu kidogo tu kashalia ili umuonee huruma na uamini kuwa anakupenda.

(v) Wanapenda mno kukusifia, hata pale unapohisi kuwa umevuruga!! Wanakupa nafasi ya kuona wanakujali na kukuvimbisha kichwa ili uwaone watu wema.

(v) Waonyeshaji mapenzi huwa wanakupa mipango mikubwa sana ambayo mara nyingi unaiona kabisa kuwa iko juu tena kushoto kabisa mwa uwezo wako, Lakini wanakupa moyo kuwa u can, na anasisitiza ujitume zaidi. Wewe hapa utahisi upo na mke mwenye mipango na vision lakini kuwa makini sana, yeye anachotaka kutoka kwako ni uaminifu tu..

(vi) Wepesi sana kukubali kupigwa faru (Kugegedwa) . Na hapa ndipo wengi wanapotuteka.

WAONYESHAJI MAPENZI, huwa wanatafuta tu njia ya kuaminiwa hawana jingine, kwahyo kuwa makini sana na hawa watu wanaojifanya kupenda sana hawa ni waonyeshaji mapenzi na sio wapendaji. Hawajutii kukukimbia ikiwa maslahi yake hayajapatikana. Wanaume wengi tunahadaika sana na waonyeshwaji mapenzi kuliko wapendaji kweli. Ewe mwanaume mwenzangu, chondechonde, chunguza uliyenaye, kama anakupenda au anakuonyesha mapenzi na uanze kuchukua hatua.

N.B.
Niliwahi kuwa nao wote wawili mpendaji na muonyeshaji mapenzisimultenously kwa muda wa miaka mitatu.Nilijifunza mengi sana. Hayo niliyoyaleta hapo ni baadhi tu.

Naomba kuwasilisha
 
Mimi naonaga sawa tu. Sinaga muda wa kujali.
 
Aisee nna mmoja naona ni mtaalamu anachanganya kupenda na kuonyesha mapenzi fuly kunichanganya
 
duuuu kwa stlye hii mimi nimekutana na muonyesha mapenzi daaah ngoja nimpe kibutiii chakeeeee mapeeeemaaaaa 😡🙄
 
Hahahhahaa nawatahadharisha tu wanaume wenzangu

ahhhh lazima tubadilishe mbinu, nina Rafiki angu huyo ni kiboko wa ku fake, huwa namuambia unaishi maisha ya kitumwa sana. Yaani hata kitu hajakipenda anakuja kulalamika pembeni mi siwezi kwa kweli. Hii thread ina ukweli 97%
 
Watoto wa siku hizi wanapenda sana mapenzi ya kitamthilia, khe khe khe khe khe!!!Muda wa kulilia mapenzi ama kubembelezana hakuna jamani, sijui labda wawasubirini vijana wa under 30 ndio wawe wanawalialia na kutoa kamasi.

.......waonyesha mapenzi.
 
Back
Top Bottom