Tofauti kati ya Kikwete, Pinda na Lowassa

lowassa ni kweli haitaji promo,ana kazi ambazo alisimamia na akaekeleza,pinda au kikwete wana lipi la kuigwa mfano? uwezo wa wa jk hakupaswa hata kuwa mkuu wa wilaya sema aliingia madarakani kwa promo sn,angalia alivyoingia madarakani alishinda kwa zaidi ya 80pc,2010 alishinda kwa 61pc,kama angegombea 2015 angeshinda kwa pc ngapi?

anaweza akawa ameyafanya yote kama unavyodai, lakini hamna kosa kosa kubwa kama la RICHMOND, ni miongoni mwa VIRUS waliolila na wanaendelea kulila taifa letu huku wakijibadili kama kinyonga kwani sasa wanajiita symbion! mpaka wamebadili na sheria ya manunuzi ya kutonunua USED kumkumbatia Lowassa na mitambo yake!Na yeye KAOZA, kama hamna wa kuwafanyia promo ndani ya CCM tafuteni upinzani kwani Nchi hii lazima iongozwe na MAGAMBA?
 
nakubaliana nawewe kuwa lowassa ni jembe, mtu mmoja kufanya maamuzi magumu ya kuibia Watanzania mabilioni ya pesa na kutuacha na njaa kali ni maamuzi yanayohitaji mtu mwenye roho ngumu kama paka
ni kweli process yoyote na hasa ya kuendesha nchi inahitaji maamuzi. Inabidi mtawala almost masaa 22 kati ya 24 ya siku (zidisha mara miaka anayokuwa madarakani) awe katika position ya kutoa maamuzi.

Laiti Mh. Lowassa angelijua kuwa ana potential kubwa katika hili na 'kujilinda', hivi leo nchi ingelikuwa haina mambo ya mchezo mchezo ambapo watu wanatumia miezi miwili huku watu wakifa kutoa uamuzi mdogo kama wa 1+3!

Rejea Pale Mwanza ambapo Mh. Lowassa alikwaluzana na mkuu wa wilaya au alipoleta wazo la 'mvua ya kutengeneza', hiyo ni ushahidi kuwa ni lazima ufanye maamuzi hata kama sio sahihi lakini wewe kama unayaamini ni sawa tu.

kweli kabisa sema tu ishu ya richmond imemwaribia.

Richmond siyo issue,mafisadi ndiyo wenye uwezo wa kuiendeleza nchi hii,tukimpeleka fukara ataanza moja kwanza kujipanga binafsi,mpaka ashibe tutakuwa tumeshachakaa vyakutosha.
 
enjo usinielewe vibaya dadangu, sina nia ya kumfanyia promo LOWASSA, sidhani kama anahitaji promo yoyote. Hapa tunajadili utendaji tukihusisha na maamuzi magumu kwa maslahi ya Taifa!!

Haihitajiki promo yoyote au kumbeba mwanao aliyefaulu kwa kiwango cha divisheni wani, ila yule wa div.IV lazima abebwe!!! PM Pinda ndio haswa anayehitaji promo kwa muonekano wake!!

Ukimaliza kuwalinganisha hivi uanze kuwalinganisha na kwenye Wizi nani mwizi zaidi ya mwenziwe! Manina!!!
 
Hahaha Lowasa hana haja ya promo ni mkali since long time hata kikwete anajua ndo maana akampa uwaziri mkuu

Alimpa kwasababu walikuwa bega kwa bega katika kuhakikisha anaingia Ikulu na kuna siri kubwa kati yao lakini sio kwa ajili ya ukali wake
 
Ukiwafanyia tathmini ya haraka haraka, utagundua kwamba kila mmoja ana mapungufu yake!

Hata hivyo kwa uchache ni kuwa: JK ni mzito wa kuamua, mzito wa kutekeleza na mwepesi wa kusahau!

PM Pinda yeye ni mzuri katika kurudia rudia maamuzi yaliyotolewa JK na hivyo kumfanya awe kigeugeu kwa maamuzi yake mwenyewe, pia huonyesha tabasamu nyembamba pale anapotambulishwa na JK kama 'mtoto wa mkulima'!!

LOWASSA yeye ni mwepesi wa kuamua, na pia ni mwepesi wa kutekeleza maamuzi yake na maamuzi ya wakuu wake wa kazi. Fuatilia alipokuwa waziri chini ya Rais Mkapa, na baadaye akiwa waziri mkuu chini ya JK!!
Kuhusu lowasa ni kweli huyu jamaa ni mwepesi sana wa kutoa maamuzi hata kama ni magumu bali yana manufaa.

Bila kumumunya maneno huyu lowasa ni kiongozi anayefaa kupewa nchi!
 
Lowasa ni bora kuliko JK na Pinda. Lakini, ana maamuzi ya kukurupuka bila kufikiria athari za mbeleni.
 
LOWASA =fisadi, jitu lisilona huruma kwa watanzania wenzake.
KIKWETU= sifa zote njema ni zake, hana baya,mapungufu hata moja labda kwenye masuala ya kifamilia.
PINDA=loading loading .............
 
kwa ninavyowaelewa mimi.
Jk hapendi kushindwa. Mtu wa makundi. Hana siri. Yuko radhi kumwaga mboga. Hapendi kuumiza kichwa. Ni mtu poa pasipokuwa na matatizo, n.k.

Pinda ni jasiri wa himaya yake. Ana uwezo wa kufanya maamuzi magumu na ya haraka. Si mtu wa kujilimbikizia. Ana hasira, n.k.

EL ni mchapakazi. Hapendi kiwingu mbele yake. Anaweza uongozi. Ana ushawishi. Ni mtu wa hila. Anapenda sana mali, n.k.
 
Huwezi elezea tofauti ya watu wakubwa watatu kwa paragraphy tatu, huu ni uvivu! remove the stupidy post, we have a lot to do to look at an attractive subject with the stupidy contents

Ukiwafanyia tathmini ya haraka haraka, utagundua kwamba kila mmoja ana mapungufu yake!

Hata hivyo kwa uchache ni kuwa: JK ni mzito wa kuamua, mzito wa kutekeleza na mwepesi wa kusahau!

PM Pinda yeye ni mzuri katika kurudia rudia maamuzi yaliyotolewa JK na hivyo kumfanya awe kigeugeu kwa maamuzi yake mwenyewe, pia huonyesha tabasamu nyembamba pale anapotambulishwa na JK kama 'mtoto wa mkulima'!!

LOWASSA yeye ni mwepesi wa kuamua, na pia ni mwepesi wa kutekeleza maamuzi yake na maamuzi ya wakuu wake wa kazi. Fuatilia alipokuwa waziri chini ya Rais Mkapa, na baadaye akiwa waziri mkuu chini ya JK!!
 
Ukiwafanyia tathmini ya haraka haraka, utagundua kwamba kila mmoja ana mapungufu yake!

Hata hivyo kwa uchache ni kuwa: JK ni mzito wa kuamua, mzito wa kutekeleza na mwepesi wa kusahau!

PM Pinda yeye ni mzuri katika kurudia rudia maamuzi yaliyotolewa JK na hivyo kumfanya awe kigeugeu kwa maamuzi yake mwenyewe, pia huonyesha tabasamu nyembamba pale anapotambulishwa na JK kama 'mtoto wa mkulima'!!

LOWASSA yeye ni mwepesi wa kuamua, na pia ni mwepesi wa kutekeleza maamuzi yake na maamuzi ya wakuu wake wa kazi. Fuatilia alipokuwa waziri chini ya Rais Mkapa, na baadaye akiwa waziri mkuu chini ya JK!!

Naongezea kapoint kadooogo kwa Waziri Mkuu, Ni mwepesi sana Wa kutoa machozi aonewe huruma..
 
Back
Top Bottom