Tofauti Iliyopo kati ya YOUTUBE na VEVO

Tofauti Iliyopo kati ya YOUTUBE na VEVO

MimiJoel

Member
Joined
Sep 22, 2017
Posts
42
Reaction score
46
1.VEVO inamilikiwa kwa ubia na Sony Music , Universal Music, google na Abu Dhabi Media wakati YouTube ipo chini ya google.

2.Vevo Inahusu muziki pekee wakati YouTube Ni videos zote Hadi Filamu

2.Vevo inaonekana nchi chache Sana Hadi sasa wakati YouTube Ni dunia nzima isipokuwa maeneo machache ambayo labda nchi husika imezuia.

3.Views nyingi za wanamuziki walio Vevo hutegemea kupata views nyingi kutoka YouTube kwa Akaunt zao kuunganishwa huko kwasababu kwenye website ya VEVO pekee viewers huwa wachache

4.Uzuri wa Kuwa Vevo Ni Kuwa unakutana na videos original tu za msanii Mara moja kuliko YouTube kunakuwa na pirated videos nyingi ambazo zinaweza kushindana na video original ya msanii kwa views hivyo msanii kukosa mapato kirahisi

5.Vevo Inaingiza pesa vizuri kupitia YouTube kwasababu accounts za wasanii wengi zipo chini ya makampuni au labels za muziki zinazoendeshwa na makampuni hayo sio wanamuziki wenyewe Kwahiyo Inakuwa rahisi advertisers kuonyesha matangazo Yao Vevo kwenye Akaunt nyingi original

6.Kwenye VEVO msanii anaweza asifaidike na views za videos zake kutegemeana na mikataba aloingia na makampuni au wanagawana faida wakati YouTube ya kawaida mapato huwa ya msanii pekee.

7. VEVO Ina channel YouTube ila YouTube haina channel VEVO

8.Msanii Kuwa Vevo unaweza Kuwa promoted na kampuni hiyo sababu wao wapo exclusively kibiashara so wanapromote Sana video za msanii wao kwenye Chanel's nyingine za VEVO za wasanii wengine wakati YouTube ya kawaida sio rahisi itategemea zaidi fan base ya msanii Kama Ni kubwa.

9.Wakati YouTube ta kawaida ikiwa na piracy kubwa ya kazi za wasanii, VEVO imeshutumiwa na wasanii wengine wakubwa mfano Will.i.a.m kulazimisha wasanii wasapoti brands au biashara za makampuni wasiotaka kufanya nao kazi

10. VEVO wanabana zaidi ubunifu na uhuru wa msanii kupost videos wanataka videos rasmi zaidi wakati YouTube msanii yupo huru zaidi, Lady Gaga alikuwa na Akaunt Mbili ya VEVO na YouTube ya kawaida

11. Kuna mastaa wengi wakubwa hawapo VEVO na kuna mastaa wengi wakubwa wapo VEVO

12.Ikiwa tayari Mtu Ana matangazo ya google katika Akaunt yake iwe VEVO au YouTube ya kawaida sio rahisi msanii kununua views kwasababu google wapo makini Sana kulitambua Hilo ili wasipoteze uaminifu wa kibiashara na makampuni yanayolipa pesa kutangaza biashara zao wasipate viewers hewa. inaweza Kuwa rahisi kununua views YouTube kwa Akaunt ambazo hazina matangazo ya google ingawa wakijua pia wanafuta channel yako

13: All in All YouTube ndio yenye nguvu zaidi sababu Vevo wanawategemea YouTube kibiashara ndio maana Ni washirika.

14.Msanii Kuwa VEVO channel yako inaonekana tu haraka inasaidia Mtu kujua fasta original Akaunt ya msanii kwa Alama ya VEVO ila Kuwa VEVO sio Kuwa maarufu zaidi, Kuwa na kazi nzuri zaidi sababu kipaumbele cha VEVO Ni kwa wasanii wa Sony na Universal Music au labels za kampuni nyingine, Ni hiari msanii binafsi kuwepo VEVO,

15.Youtube Ina watumiaji wengi zaidi kutokana na Kuwa na options ya videos nyingi kwa watazamaji wakati VEVO Ni chache mno

16.Bila uwepo wa YouTube VEVO itakosa nguvu ya wasanii wakubwa ambapo traffic kubwa ya viewers wa videos zao hutokea YouTube na sio website rasmi ya VEVO
 
Back
Top Bottom