Tofaut ya vipimo hivi ni nin MRDT na BS

Tofaut ya vipimo hivi ni nin MRDT na BS

Malaria inasababishwa na plasmodium ambapo kuna aina kama nne za plasmodium wanaobebwa na mbu, kuna plasmodium vivax,ovale,falciparum na malariae.

MRDT ni Malarial Rapid Diagnosis Test inatumika kugundua uwepo wa malaria kwa haraka zaidi, inafanya kazi kwa kutumia antibody na antigen, antibody ni vilinda mwili vilivyopo kwenye seli, antigen ni visababisha ugonjwa.

Katika mRDT ni kwamba antigen za plasmodium zinaitikia sana kwa antibody ambazo ni aina fulani ya protein inaitwa HRP-II(Histidine Rich Protein-II), maabara tukichukua sample ya damu kama ina malaria tukiweka hio protein vikakutana vinatengeneza rangi mpya hivyo tukiona hio rangi tunasema mgonjwa ana malaria.

BS ni Blood Smear yaani tunachukua sample ya damu tunaweka kwenye kislide flan kama kichupa cha mstatili tunasmear kisha tunachungulia kwenye hadubini (microscope) tukiona plasmodium tunasema mgonjwa ana malaria.
 
Faida ya mRDT ni kwamba ni haraka kupata majibu ndani ya dakika10 mpaka 20 inatoa majibu.
Hasara yake, haiwezi kugundua uwepo wa vimelea vya malaria kama vipo kwa kiwango kidogo maana reaction ya HRP-II inahitaji plasmodium wawe wengi kiasi.
 
Faida ya BS inatoa majibu ya uhakika hata kama plasmodium ni wachache kwenye damu.

Hasara yake ni inachelewesha majibu, inahitaji walau dakika60 au zaidi mpaka kuandaa sample, kusmear, kufanya microscopy na kutoa majibu.
 
MRDT ni kwa ajili ya kuanza tiba haraka bila kuchelewa.

BS ni kwa ajili ya kuhakikisha uhakika wa matibabu na kujua ukubwa wa maambukizi.
 
1. MRDT ni qualitative inapima presence of plasmodium antigen in the blood na sio actual parasite. MRDT iko prone kukupa false positive kwa kudect antigens ambazo si za malaria. MRDT ikiwa positive chance ya kuwa kweli una malaria ni kubwa
2. BS ndo Gold standard. Ina quantify parasites ni more sensitive. Shida yake kuifanya inahitaji utaalamu mkubwa kuliko MRDT
 
Wataalamu wanasema MRDT ni kipimo cha haraka haraka na rahisi ili kutengeneza dhana ya kutokuwepo malaria kwa mgonjwa (Negative), na ikitokea hiyo dhana ikawa tofauti (Positive) basi kipimo cha juu zaidi na standard (BS) ndio kitumike kuthibitisha uwepo kweli wa vimelea wa malaria na wingi wao.

Hivyo, kwa lugha nyepesi kabisa, Mgonjwa ataanza kwa kupimwa na MRDT na matokeo yakiwa negative, mchezo unaishia hapo hapo. Lakini matokeo yakiwa Positive inabidi kipimo cha BS kifuate ili kuthibitisha hiyo positive ni kweli imetokana na uwepo na uwingi wa vimelea wa malaria ama la.
 
kuna wakati pia inatokea hyperparastemia au hata mutation za protein antigen kina HRP na aldolase inaleta false negative!
Researches zilizofanyika tutumie mkuu tuone prevalence ya mutated hizo protein antigen kwa mazingira yetu kiasi Cha kuleta hizo false negative ....so far ni ngapi na imeonesha kwa kiasi Gani hiyo mutated plasmodium ?
 
Kabisa ni vile tu research ikimalizika haitumiwi inatunzwa makabatini.
 
Back
Top Bottom