Toa maoni swala la Manji na Coco beach

THEBLACKPEARL

Member
Jun 11, 2015
69
46
Hebu tuambiane nini hatma ya coco beach?? na je wazo la Mfanyabiashara Yusuph Manji la kuta kuuendeleza ufukwe ni la msingi au ubabaishaji!
mwenyewe (MANJI)

""amesema bado anasubiria majibu kutoka kwa Rais John Magufuli juu ya sakata la kuendeleza ufukwe wa Coco, maarufu Coco Beach uliopo Kinondoni jijini Dar es Salaam baada ya kumwandikia barua Desemba mwaka jana.


Manji alisema anatamani suala hilo limalizike kabla ya kuondoka rasmi katika kampuni hiyo mwezi ujao, na kwamba tayari alishamwandikia barua kiongozi huyo wa nchi juu ya usahihi wa mchakato wa zabuni wa kuendeleza eneo hilo la ufukwe wa Bahari ya Hindi.



Mfanyabiashara huyo anasema anashangazwa na baadhi ya viongozi wa Serikali kurudiarudia suala hilo na kusababisha kuwa maarufu kuliko hata Benki Kuu ya Tanzania (BoT).



Kwa mujibu wa mfanyabiashara huyo, suala la Coco Beach ilikuwa ni sehemu ya biashara na kwamba zabuni hiyo walishinda baada ya kutimiza masharti yaliyokuwa yamependekezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, lakini cha kushangaza hali imekuwa tofauti.



Mfanyabiashara huyo alifikia hatua hiyo kufuatia Rais John Magufuli kutangaza eneo hilo liendelee kutumika na watu wa kawaida kwa kile alichosema kuwa kuna mfanyabiashara ambaye anatumia fedha kuwahonga baadhi ya watumishi wa halmashauri hiyo ili kumiliki eneo hilo.



Rais Magufuli ambaye alikuwa akihutubia mkutano wa wafanyabiashara alisema; “Inanifadhaisha sana kuona mfanyabiashara tajiri akihonga maofisa kutumia vibaya fedha za umma kwa manufaa yake binafsi na wakazi kutoka mazingira duni wakishindwa kutumia ufukwe huo kuogelea na kuburudika.”



Hata hivyo, Manji alisema kuwa kampuni yake ilikuwa ikilihitaji eneo hilo kuliendeleza kwa ajili ya biashara na kuhudumia wananchi hivyo iwapo Rais ataridhia linyang’anywe licha ya kushinda zabuni na mahakamani, hawatakuwa na hatua nyingine ya kufanya."""


HEBU NIAMBIE MTANZANIA MWENZANGU WEWE UNAONAJE HILI SWALA TUMPE AU TUENDELEE KUBURUDIKA WENYEWE
KWA MAONI YANGU MIMI NADHANI MANISPAA YA KINONDONI INAWEZA KUUENDELEZA UFUKWE ENDAPO WATAJIPANGA SAWA SAWA
TOA MAONI TUONE TUNAFIKIA WAPI
 
Kama alinunua kihalali mpeni beach yake,mbona wanyama mmeuza uarabuni,tanganyika packers iko wapi?ruvu ranch iko wapi?tanzanite ziko wapi?
 
Mbona sehemu ziko nyingi za ufukwe kwa dar kwani lazima aendeleze coco tu.....aende kigamboni huko
 
A kamdai marehemu Kabwe! kwani Kwabwe Fukwe za mwanza aliuza zote hata pakufulia na kuchota maji! aende India kwao kwani Mtanzania gani anamiliki Beach India? Kwenye u Kweli hakuna ubaguzi! Manji usimsumbue Rais wetu?
 
Back
Top Bottom