naamini dhambi kuu ya zitto ni kukataa kufanya siasa kwa style mnayotaka ninyi ambayo mnadhani ndio suluhu la matatizo yenu ambayo ukweli ukiyaangalia sana hayana upeo mkubwa isipokuwa chuki zenu dhidi ya ccm tu.
Zitto anaangalia siasa zaidi ya kuiondoa ccm madarakani tu. Kwake yeye kitu cha kwanza na muhimu ni kujenga demokrasia makini ya vyama vingi ambayo itawezekana tu pale watanzania watakapoongozwa kuondoa ukiritimba wa ccm (single party dominance). Cha pili ni kujenga misingi ya watanzania wote kutambua, kuamini na kuthamini utamaduni wa kidemokrasia ambao unachukulia tofauti za kifikira na kimisimamo kama mbolea na sio sumu ya maendeleo. Cha tatu kujenga tanzania yenye nguvu kiuchumi na kijamii ambayo itawezesha kufanikisha umoja wa kiafrika ambao kwake anaamini kuwa ndio mkombozi mkuu wa madhila na changamoto tunazokutana nazo sasa kama taifa la dunia ya tatu.
Omarilyas