TMAA yaongeza makusanyo ya maduhuli (mrabaha) ya madini

TMAA yaongeza makusanyo ya maduhuli (mrabaha) ya madini

JIS

Member
Joined
Dec 5, 2011
Posts
73
Reaction score
48
na Chalila Kibuda

WAKALA wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) amefanikiwa kuongeza mapato ya serikali yatokanayo na makusanyayo ya mrahaba kwenye uchimbaji na mauzo ya madini ya ujenzi mara 70 kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam na TMAA ongezeko hilo la maduhuli limetokana na matumizi ya hati ya mauzo ya madini iliyoanza kutumika Juni mwaka juzi.

Kwa mujibu wakala huyo, pamoja na ongezeko la mapato kutoka wastani wa milioni 2 za sasa kwa mwezi kabla ya matumizi ya hati hadi milioni 230 za sasa kwa mwezi, pia kumekuwepo na ongezeko kubwa la wachimbaji halali wa madini ya ujenzi.

"TMAA ikishirikiana na Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Mashariki, kwa msaada wa polisi, iliendesha operesheni kabambe ya kuondoa uchimbaji haramu wa madini ya ujenzi katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kwa muda wa siku 12 kuanzia Agosti mosi hadi 16 mwaka jana," ilisema taarifa hiyo.

Ilieleza kuwa operesheni hiyo ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa na kukidhi malengo yaliyotarajiwa na kutokana na hali hiyo idadi kubwa ya wachimbaji wadogo wa madini ya ujenzi wasio na leseni waliwasilisha maombi ya kupewa leseni za uchimbaji kwenye maeneo yaliyotengwa.

TMAA imesema kuanzia Julai mosi mwaka jana hadi Novemba 30 leseni 282 za uchimbaji wa madini ya ujenzi katika maeneo yaliyotengwa zilitolewa kati ya hizo, 270 ni za mchanga na 12 za kokoto.

Pamoja na mambo mengine alisema takwimu zinaonyesha mauzo ya madini kuongezeka kutoka bilioni 1.5 kabla ya kuanza kwa matumizi ya vocha hadi bilioni 4.3 kwa mwezi kwa sasa.



MY TAKE:

Hawa jamaa wa TMAA kwa kweli wanafanya kazi nzuri sana. Kumbe hata kwenye madini ya kokoto na mchanga kuna wizi mtupu? nchi hii watu wanakwepa sana kulipa kodi za Serikali.

Nilipata maelezo yao kwenye maonesho ya Nanenane huko Dodoma kuwa wamewezesha hata ile migodi mikubwa kuanza kulipa kodi ya mapato.

Chombo hiki kingeimarishwa na Serikali ya JK tungepata manufaa makubwa sana nchi hii. Hongera TMAA kwa kazi yenu nzuri. Keep it up.
 
Na kweli they are doing a good job,it is only narrow minded people who cannot see what these people are doing,waendelee tu na kazi wasiogope nguvu za mafisadi
 
Kwa kwel katika Wakala ambazo zinzchapa kazi hii naikubali, maana juzijuzi nimetoka Geita naona jamaa wanasema asaivi Serikali imeamka kupitia TMAA, hadi chunya mgodi mpya jamaa wapo, pia ukibeba mchanga/kokoto na ukikamtwa hauna kibali chao ni noma maana unakuwa unakwepa kulipa stahii za Serikali.
BIG UP TMAA msije bweteka.
 
Watanzania tunazidi kufunguka.
hakuna kurudi nyuma, hao jamaa (TMAA) safi sana, jana walitukamata Kibaha kisa tulikwepa kodi ya kokoto. safi sana!
 
  • Thanks
Reactions: PSM
Back
Top Bottom