TMA yatoa tahadhari ya mvua kubwa na upepo katika mikoa 6 kwa siku 5 mfululizo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetangaza mvua kubwa katika mikoa sita bara na baadhi ya maeneo visiwa vya Unguja na Pemba zitakazodumu kwa siku tano kuanzia leo Jumamosi Desemba 28, 2019.

Akitoa taarifa kwa umma, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Wilberforce Kikwasi amesema mvua zinazoendelea kunyesha hivi sasa jijini Dar es Salaam, Morogoro, Pwani, mikoa ya kusini pamoja na Unguja na Pemba ni za siku tano mfululizo kuanzia na kuwataka wananchi wa maeneo hayo kuchukua tahadhari.

“TMA inatoa tahadhari juu ya uwepo vipindi vifupi vya mvua kubwa katika baadhi ya maeneo yaliyopo Kusini mwa nchi yetu hususani Ruvuma, Lindi, Mtwara eneo la kusini mkoa wa Morogoro, mkoa wa Pwani, Dar es Salaam pamoja na maeneo machache ya visiwa vya Unguja na Pemba.”

“Hali hii ya mvua inatokana na kuendelea kuimarika kwa ukanda wa mvua katika maeneo ya Kusini mwa nchi yetu na hivyo kusababisha kujengeka kwa mawingu makubwa na mazito yanayosababisha mvua kubwa zitakazoambatana na upepo mkubwa na radi hivyo wananchi waliopo maeneo hayo wanatakiwa kuchukua tahadhari,” amesema Kikwasi.

Kikwasi amesema TMA inaendelea kufuatilia kwa karibu maeneo hayo na kutoa mrejesho pale itakapohitajika.

“Taarifa hii inaanza leo Desemba 28, 2019 na ni kwa siku tano zijazo, TMA itaendelea kufuatilia na kutoa mrejesho kupitia miundombinu mbalimbali ya mawasiliano kupitia vyombo vya habari ikiwamo mitandao ya kijamii, televisheni na redio,” amesema Kikwasi.
 
Khaaa kisa imenyesha Leo kwa hyo Na wao wanateleza na beat tu au sio?

Cc: Bushmamy hebu njoo uone hawa vituko wenzio
 
Hawa jamaa bwana huwa ni bure kabisa. ilitakiwa hii itoke last week au before! Sasa mvua imeanza nao ndio wanajiinua yaani.
 
3877da66836489950d78c47bebec4cc1

Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetangaza mvua kubwa katika mikoa sita bara na baadhi ya maeneo visiwa vya Unguja na Pemba zitakazodumu kwa siku tano kuanzia leo Jumamosi Desemba 28, 2019.

Akitoa taarifa kwa umma, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Wilberforce Kikwasi amesema mvua zinazoendelea kunyesha hivi sasa jijini Dar es Salaam, Morogoro, Pwani, mikoa ya kusini pamoja na Unguja na Pemba ni za siku tano mfululizo kuanzia na kuwataka wananchi wa maeneo hayo kuchukua tahadhari.

“TMA inatoa tahadhari juu ya uwepo vipindi vifupi vya mvua kubwa katika baadhi ya maeneo yaliyopo Kusini mwa nchi yetu hususani Ruvuma, Lindi, Mtwara eneo la kusini mkoa wa Morogoro, mkoa wa Pwani, Dar es Salaam pamoja na maeneo machache ya visiwa vya Unguja na Pemba.”

“Hali hii ya mvua inatokana na kuendelea kuimarika kwa ukanda wa mvua katika maeneo ya Kusini mwa nchi yetu na hivyo kusababisha kujengeka kwa mawingu makubwa na mazito yanayosababisha mvua kubwa zitakazoambatana na upepo mkubwa na radi hivyo wananchi waliopo maeneo hayo wanatakiwa kuchukua tahadhari,” amesema Kikwasi.

Kikwasi amesema TMA inaendelea kufuatilia kwa karibu maeneo hayo na kutoa mrejesho pale itakapohitajika.

“Taarifa hii inaanza leo Desemba 28, 2019 na ni kwa siku tano zijazo, TMA itaendelea kufuatilia na kutoa mrejesho kupitia miundombinu mbalimbali ya mawasiliano kupitia vyombo vya habari ikiwamo mitandao ya kijamii, televisheni na redio,” amesema Kikwasi.
Taken
 
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya kunyesha kwa mvua kubwa itakayoambatana na upepo mkali na radi kwa siku tano mfululizo mikoa ya Dar es salaam, Morogoro, Ruvuma, Lindi, Mtwara, Pwani pamoja na maeneo machache ya Visiwa vya Unguja na Pemba.

Back
Top Bottom