TMA: Utabiri wa hali ya hewa hatarishi kwa siku 5. Mikoa ya Ukanda wa Pwani kuathirika zaidi

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) imetoa utabiri wa hali ya hewa iliyoiiata ni hatarishi kwa siku tano ikionesha mikoa itakayo athirika zaidi ni iliyo katika ukanda wa Pwani

056F8F35-BD29-41DF-900E-2E4B1E29BF87.jpeg

TMA imetoa angalizo la mvua kubwa siku ya Novemba 06, kwa baadhi ya mikoa ya Pwani na Ukanda wa Kaskazini katika mikoa ya Pwani, Dar na Tanga pamoja na Visiwa vya Pemba na Unguja

Aidha, hakuna tahadhari iliyotolewa katika siku za Novemba 07 na Novemba 08 ingawa Novemba 09 kumetolewa angalizo la mvua kubwa katika maeneo ya mikoa ya Morogoro, Lindi, Mtwara, Pwani, Dar, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba

93A501EA-EA73-4424-B079-E790174BA12D.jpeg

Hata hivyo, Mamlaka imebainisha kuwa uwezekano wa kutokea kwa utabiri huu ni wa Wastani na Kiwango cha athari zinazoweza kutokea ni cha Wastani

Ikibainisha athari zinazoweza kutokea imesema ni pamoja na baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, ucheleweshwaji wa usafiri na kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za Kijamii na Kiuchumi
 
Asubuhi imepiga jalamba huku Pwani... Ilikuwa ya dakika kumi tu mziki wake tumeuona
Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) imetoa utabiri wa hali ya hewa iliyoiiata ni hatarishi kwa siku tano ikionesha mikoa itakayo athirika zaidi ni iliyo katika ukanda wa Pwani

View attachment 1255260

TMA imetoa angalizo la mvua kubwa siku ya Novemba 06, kwa baadhi ya mikoa ya Pwani na Ukanda wa Kaskazini katika mikoa ya Pwani, Dar na Tanga pamoja na Visiwa vya Pemba na Unguja

Aidha, hakuna tahadhari iliyotolewa katika siku za Novemba 07 na Novemba 08 ingawa Novemba 09 kumetolewa angalizo la mvua kubwa katika maeneo ya mikoa ya Morogoro, Lindi, Mtwara, Pwani, Dar, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba

View attachment 1255261

Hata hivyo, Mamlaka imebainisha kuwa uwezekano wa kutokea kwa utabiri huu ni wa Wastani na Kiwango cha athari zinazoweza kutokea ni cha Wastani

Ikibainisha athari zinazoweza kutokea imesema ni pamoja na baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, ucheleweshwaji wa usafiri na kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za Kijamii na Kiuchumi
 
Naishukuru serikali ya awamu ya 5 chini ya dokta John Pombe Magufuli kwa kutuletea masika mara mbili ndani ya msimu mmoja, hii yote ni kuonyesha ni jinsi gani serikali ya awamu ya 5 inavyowajali wakulima wanyonge tunaotegemea mvua katika kilimo chetu.
 
Nashukuru mahindi yangu yataenda vema!! Mvua hizi nzuri inanyesha inapumzika,
 
Nimepanda miti yangu ya matunda na kivuli kwa hiyo ninahitaji sana mvua.

Wewe uza mitumba kibarazani haitanyeshewa.
Kibarazani! Mitumba siyo chapati niko kwenye barabara ya watembea kwa miguu na wao wamabanana na magari, walivyo wakatili hawaturuhusu tuweke vibanda mvua yetu jua letu.
 
Back
Top Bottom