TMA: Mvua Dar zimefika ukingoni

TMA: Mvua Dar zimefika ukingoni

SOGHOO

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2015
Posts
1,268
Reaction score
568
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mvua zilizoanza kunyesha Machi hadi Mei, mwaka huu na kusababisha athari mbalimbali, ikiwamo vifo, upotevu wa makazi na uharibifu wa miundombinu katika Jiji la Dar es Salaam zimefikia ukingoni.

=================================

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mvua zilizoanza kunyesha Machi hadi Mei, mwaka huu na kusababisha athari mbalimbali, ikiwamo vifo, upotevu wa makazi na uharibifu wa miundombinu katika Jiji la Dar es Salaam zimefikia ukingoni.


Mkurugenzi wa Huduma wa Utabiri wa hali ya Hewa (TMA), Dk. Hamza Kabelwa, alisema kwa sasa mvua zitaendelea hadi Mei 20, mwaka huu, lakini katika mikoa ya Pwani Kaskazini inayojumuisha mikoa ya Pwani, Tanga, na visiwa vya Unguja na Pemba.

"Kwa jana na leo, vituo vya maeneo hayo havijasoma mvua. Kituo cha Pemba Mei 16, mwaka huu, kilisoma mvua milimita 35, huku kwingine ikiendelea kupungua…taarifa zetu tunazichukua kwa siku kumi. Kwa sasa tunakusanya taarifa ya siku kumi zijazo na tutaiweka wazi kwa ajili ya umma kujua," alisema.

Alisema kwa wakazi wa Dar es Salaam, mvua zimekwisha na kwamba, zitakazoendelea kwenye maeneo mengine hazitakuwa na kasi kama iliyokuwa Mei 6 na 7, mwaka huu.

Dk. Kabelwa alisema kwa sasa wanafanyia uchambuzi wa mifumo ya hali ya hewa ili kuona hali ya mvua ikoje.

Chanzo: Nipashe
 
Wa mabondeni tuendelee kuzaana kama kawa
 
Hawa walisema mpaka tar 21 sasa imekuwaje? Utabir wao kama unamashaka hv!
 
Wa Jangwani ngoja turejee makwetu kwa raha zetu...

Tuliteseka kwa mamvua nanyi tesekeni mwa mifoleni sasa

Kutesa kwa zamu.
 
WAondoe jengo la DART Jangwani ndio na sisi tuige mfano wa kuondoka mabondeni
 
Hawa watu wakiona jua linawaka watasema mvua imeisha lakini ghafla mvua ikija kwa kasi na kuleta athari hapohapo hubadilika na kutoa maonyo!nilishaga toa mada/Topic miezi 2 ilopita hapa jf kuhusu hawa watabiri wetu na hii style yao
 
Back
Top Bottom