SI KWELI PreGE2025 TLS yamkemea Maria Sarungi

SI KWELI PreGE2025 TLS yamkemea Maria Sarungi

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
Je, hii taarifa kuwa Chama cha wanasheria wa Tanganyika (TLS) kimemkemea Maria Sarungi?
IMG_20250521_213559_998.JPG
 
Tunachokijua
Chama cha wanasheria Tanganyika (Tanganyika Law Society - TLS) ni taasisi ya wanachama inayowakilisha mawakili Tanzania bara. TLS inaundwa kupitia sheria ya chama cha wanasheria Tanganyika Sura ya 307 R.E 2002.

Madai

Mtumiaji mmoja wa mtandao wa Instagram alichapisha grafiki inayoonekana kuwa ni ya nembo ya chobo cha habari cha Jambo TV huku ikiambatana na ujumbe unaosomkea “TLS yamkemea Maria Sarungi”. Grafiki hiyo imeambatana na picha ya Rais wa Chama cha wanasheria Tanganyika (Tanganyika Law Society) Boniface Mwabukusi na inayoonekana kuwa ni barua kutkoka TLS.

Uhalisia wa madai hayo

Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa madai hayo si ya kweli. Ufuatiliaji kwa nji ya mtandao umebaini kuwa barua inayoonekana katika grafiki hiyo haikutolewa wala kuchapishwa na Tanganyika law society.

Ufuatiliaji umebaini kuwa hadi wakati ripoti hii inaandaliwa Mei 16, 2025, taarifa ya mwisho kuchapishwa katika kurasa rasmi za TLS ilikuwa ni Taarifa kwa Umma kuhusiana na vitisho dhidi ya Boniface Mwabukusi. Taarifa hiyo kwa Umma ilitolewa Mei 13, 2025 kwa lugha ya kiswahili na kiingereza. Tazama hapa na hapa.

Aidha ufuatiliaji kwa kutumia maneno muhimu (keyword search) JamiiCheck imebaini kuwa hakuna taarifa inayofanana na hiyo kutoka katika kurasa rasmi za miandao ya kijamii ya Jambo TV hivyo hata grafiki hiyo ni ya kughushi.
Mbona kumeibuka sana matamko feki mitandaoni? Naona John Mrema TWITI zake zinafekiwa sana.
 
Back
Top Bottom