Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,437
- 5,234
Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kwa kushirikiana na mashirika ya haki za binadamu nchini, yakiwemo Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kinapenda kuutangazia umma kuwa kitatoa msaada wa kisheria bure kwa watuhumiwa wote waliopo katika vituo vya polisi na wale ambao tayari wameshafunguliwa mashtaka ya uhaini au makosa mengineyo yanayohusiana na kukamatwa kwao wakati wa kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Msaada huu utatolewa kutokana na maombi ya familia za watuhumiwa ambayo wamewasilisha TLS na msaada huu una lengo la kuhakikisha kuwa haki za watuhumiwa hawa zinalindwa na kwamba wanapata uwakilishi wa kisheria, kama inavyohitajika kwa mujibu wa Ibara ya 13(6)(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kwa mujibu wa Sheria ya Msaada wa Kisheria ya Mwaka 2017. Lakini pia msaada huo wa kisheria unatolewa kwasababu watuhumiwa wengi wanatoka familia zenye kipato cha chini
zisizokuwa na uwezo wa kulipa gharama za mawakili. Haki ya kila mtu kupata uwakilishi wa
kisheria ni ya msingi na ni haki ya kikatiba.
Kama chama cha kitaaluma cha wanasheria, TLS ina wajibu wa kuhakikisha kuwa watuhumiwa wanapata huduma ya kisheria inayostahili, na kwa mujibu wa kifungu cha 4 cha Sheria ya Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), TLS inawajibika kutoa msaada wa kisheria kwa umma. Hii ni sehemu ya jukumu letu la kuwatumikia wananchi na kuhakikisha kuwa haki za binadamu.
Kusoma Zaidi