TLS: Hatuwezi kuwazuia wanachama wetu kujihusisha na siasa

Azim Sokoine

JF-Expert Member
Aug 20, 2014
1,431
2,627
Habari wakuu,

Mwenyekiti wa kamati ya uchaguz wa TLS dk. Kibuta amesema chama chao si chama cha siasa ila hawawez mzuia mwanachama wao yoyote kujihusisha na siasa.

Ameendelea kusema msikitini au kanisani hakuna siasa ila waumini na hata mapadri na mashehe kuna vyama vyao vya siasa wanavyovipenda hivyo chama chao kwa mujibu wa kanuni zao hawamkatazi mwanachama wao yeyote kujihusisha na siasa.

Amesema mpaka sasa waliojitokeza kugombea nafasi ya urais kwenye chama chao wamefikia wagombea watano.

Chanzo: Azam tv habari
 
Amiri jeshi huwa na nguvu pale jeshi linapomuunga mkono, ila jeshi likiamua kuwa kinyume naye, nguvu zote humwisha. Hii ni pamoja na flame/Mfalme.

Nahisi kuna kitu hakipo sawa, na huu ni moshi tu moto utaonekana baadae.
Moshi wa kijivu au upi uliokusudia mkuu?
 
Nimebahatika kumsikiliza hapa kuna swali aliulizwa kama anaweza kutaja majina ya wagombea. Akajibu kuwa wapo 5 ila hawezi kuwakumbuka wote na kama hawezi kuwakumbuka wote kwa majina basi sio lazima kuwataja wachache ambao anawakumbuka.
 
Amefanya jambo la maana kujaribu walau kutoa ufafanuzi wa hili swala manaake lilikuwa limeachwa njia panda.

Moja ya sifa nzuri na ambayo humfanya mtu kuacha LEGACY hata baada ya kuondoka duniani ni kusimamia ukweli kwa jinsi ulivyo.

Dr. Kibuta walau amethubutu. Kama katiba inaruhusu basi na ifatwe. Kwa nini iwe nongwa...!?
 
Nailed!

Back
Top Bottom