TKZ2025: FURSA ZA AJIRA

TKZ2025: FURSA ZA AJIRA

Tukuza hospitality

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2022
Posts
325
Reaction score
704
Kampuni ya TUKUZA (Tuenzi na Kutunza Rasilimali Zetu Adimu), inahusika na uchakataji na usambazaji wa bidhaa mbalimbali za chakula, vipodozi asili, na kuendesha MAFUNZO mbalimbali. Kampuni imefanya kazi hizi toka mwaka 2014 hapa nchini Tanzania. Bidhaa zetu zina ubora wa hali juu na zinafanya vizuri sokoni, katika sehemu mbalimbali hapa nchini.

Kampuni inapenda kuwashirikisha watanzania (wanaume kwa wanawake) wenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea, katika kazi zake, kwa kutoa fursa za kujiajiri.

Kampuni inatoa fursa za kujiajiri kupitia mauzo ya bidhaa zake mbalimbali katika maeneo yatakayoainishwa. Kuna Nafasi 123 kwa nchi nzima katika maeneo mbalimbali kama ilivyoainishwa hapa chini.
Kwa wale watakaobahatika kupata fursa hii, watapewa mafunzo yatakayowafanikisha katika kazi zao, BURE! Pia wanaweza kuanza na kianzio kidogo na kupata mapato makubwa; kwa mfano, ukianza na bidhaa za sh 50,000, unaweza kupata faida kati ya sh 30,000 na 45,000 kwa wiki.

Aidha, kampuni itaendelea kuendesha MAFUNZO ya mara kwa mara yatakayomwezesha mlengwa, mwenye bidii na maono, kuja kusimama mwenyewe kama mjasiriamali mkubwa.

Maeneo ya kazi na idadi ya nafasi.

1. Dar es Salaam
i. Gongolamboto/Ulongoni: Nafasi 4
ii. Chanika: Nafasi 2
iii. Kinyerezi/Segerea: Nafasi 2
iv. Tabata: Nafasi 2
v. Mbezi/Kimara: Nafasi 2
vi. Ubungo/Manzese: Nafasi 2
vii. Sinza/Mwenge: Nafasi 4
viii. Mbezi Beach/Tegeta/Bunju: Nafasi 2
ix. Mikocheni/Msasani/Masaki: Nafasi 2
x. Kinondoni/Mwananyamala: Nafasi 2
xi. Kigogo/Magomeni/Mabibo: Nafasi 2
xii. Banana/Karakata/Vingunguti: Nafasi 2
xiii. Buguruni/Ilala: Nafasi 2
xiv. Kariakoo: Nafasi 2
xv. Buza/Tandika: Nafasi 3
xvi. Temeke/Mtoni/Kurasini: Nafasi 2
xvii. Chang'ombe/Keko: Nafasi 2
xviii. Kijichi/Mbagala: Nafasi: 2
xix. Kitunda/Kivule: Nafasi 2
xx. Kigamboni: Nafasi 2

2. Morogoro mjini: Nafasi 2
3. Iringa: Nafasi 2
4. Njombe: Nafasi 2
5. Mbeya: Nafasi 3
6. Songwe: Nafasi 2
7. Songea: Nafasi 2
8. Dodoma: Nafasi 3
9. Singida: Nafasi 2
10. Tabora: Nafasi 4
11. Shinyanga: Nafasi 3
12. Simiyu: Nafasi 2
13. Mwanza: Nafasi 4
14. Geita: Nafasi 3
15. Kigoma: Nafasi 4
16. Kagera: Nafasi 4
17. Mara: Nafasi 4
18. Manyara: Nafasi 3
19. Arusha: Nafasi 4
20. Kilimanjaro: Nafasi 4
21. Tanga: Nafasi 4
22. Pwani: Nafasi 4
23. Lindi: Nafasi: 2
24. Mtwara: Nafasi 2
25. Rukwa: Nafasi 2
26. Katavi: Nafasi 2
27. Unguja: Nafasi 3
28. Pemba: Nafasi 2

Sifa za mwombaji:
1. Awe Mtanzania.
2. Awe anajua kusoma, kuandika, na kuongea vizuri kwa lugha ya Kiswahili na/au Kiingereza.
3. Awe anajua hesabu, hasa ya fedha.
4. Awe na ujuzi/uzoefu wa biashara
5. Awe na nidhamu ya kufanya kazi
6. Awe na lugha nzuri kwa wateja.
7. Awe na afya njema.
8. Awe mbunifu na tayari kujifunza mambo mapya kila wakati.
9. Awe tayari kukua na kampuni.
10. Awe msafi na mtanashati wakati wote.
11. Awe mwadilifu na mwaminifu kwa kampuni na wateja wake.
12. Awe tayari kusikiliza na kutekeleza maelekezo ya viongozi wa kampuni.
13. Awe na mtaji, kuanzia shilingi za kitanzania, Elfu hamsini.

Utaratibu kutuma maombi.

Tuma barua ya maombi, pamoja na wasifu wako, pamoja namba ya simu kwa Meneja Uzalishaji na Ubunifu - TUKUZA kupitia barua pepe: tukuzahc@gmail.com

Mwisho wa kupokea maombi ni Tarehe 30/04/2025.

NB: Maombi yatakayotumwa kwa njia nyingine hayatafanyiwa kazi.
 
Back
Top Bottom