barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,865
Kwa sasa neno njaa sio uchochezi tena,serikali kupitia waziri wa kilimo Dr Tizeba imetangaza kuwepo kwa upungufu wa chakula (Njaa) kwa takribani tani 35,491 zinazohitajika kati ya mwezi Feb na April 2017.
Huku watu 1,186,028 wakiwa katika hali ya ukosefu mkubwa wa CHAKULA katka Halmashauri 55 Nchini.
Aidha watu 118,603 hawana uwezo kabisa wakupata chakula na mahitaji yao ni tani 3,549.
Mpango wa serikali ni kuwapelekea chakula kwa bei nafuu.
Hakika ni dhahiri kuwa njaa haifichiki.Ni uhakika sasa tuna upungufu wa chakula nchini,ambapo kwa kiswahili kifupi ni kuwa "Tuna Njaa ndani ya nchi" katika maeneo mengi ambapo watu wanashindia maembe na mizizi.
===================
Taarifa kutoka vyanzo vingine
===================
Serikali imesema matarajio ya ukuaji wa pato la taifa kwa wastani wa asilimia 7.0 uliotegemewa uenda usifikiwe kutokana na mwenendo wa uchumi katika kipindi cha miezi tisa ya mwanzo katika sekta zinazoajiri watu wengi na zenye mchango mkubwa katika uchumi kutokuwa katika kasi inayotarajiwa.
Akitoa kauli ya serikali bungeni kuhusu mwenendo wa hali ya uchumi waziri wa fedha na mipango mhe dkt phillip mpango amesema sekta ya kilimo ilitarajiwa kukuwa kwa asilimia 2.6 lakini ilikuwa kwa asilimia 2.1, biashara matarajio ni asilimia 7.6 ilikuwa kwa asilimia 5.6.
Kuhusu hali ya chakula nchini, Waziri wa Kilimo, Mifugo na uvuvi, Dkt Charles Tizeba amesema Tanzania haina njaa, bali ni uhaba wa chakula katika baadhi ya maeneo na serikali inahifadhi ya chakula ya kutosha na kuwaomba wananchi kutumia hifadhi ya chakula walionayo kwa uangalifu mkubwa.
Wakizungumza kuhusu kauli za serikali baadhi ya wabunge wameitaka serikali kufanya tathimini ya kina kuhusu hali ya chakula kutokana na maeneo mengi kuwa na uhaba wa vyakula, huku wengine wakitaka serikali kuharakisha kutoa chakula cha msaada katika maeneo hayo.
Katika kikao cha kwanza cha mkutano wa sita wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wabunge wanne wameweza kuapa kiapo cha uamifu wakiwemo watatu walioteuliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli na mmoja Mbunge wa jimbo kutoka Zanzibar.
Chanzo: ITV
=========
Mada hii ilisomwa kwenye JamiiLeo ya JamiiForums; Kuona mada nyingine zilizosomwa angalia video hii hapa chini:-