Tizeba na Mwijage mnamuangusha Rais

Tizeba na Mwijage mnamuangusha Rais

kabombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2011
Posts
26,151
Reaction score
18,751
Mpango wa Rais Magufuli kuharakisha ujenzi wa viwanda ili kuinua uchumi wa nchi,kuzalisha ajira na vipato kwa masikini,unahitaji kuungwa mkono kwa kasi kubwa sana toka kwa mawaziri hawa wawili.

Waziri Mwijage anaonesha amekariri kuwa viwanda ni lazima watu watoke nje ya nchi waje na mitaji yao waanzishe viwanda.

Waziri Mwijage amekariri kiwanda ni eneo kubwa la ardhi ambalo linahitaji mchakato ili uanze kuzalisha.

Mwijage ameshindwa kabisa,kuiamsha SIDO,itengeneze mashine ndogo ambazo watakopeshwa wajasiriamali,tayari kuzalisha bidhaa kamili au malighafi kwa ajili ya kutumika kwenye viwanda vikubwa nchini.Hiyo ndio kazi ya SIDO.

SIDO imelala,wamemuachia Rais peke yake kuhangaika na kauli mbiu yake ya viwanda,wao wanakunywa mvinyo tu business as usual

Tizeba,wizara yake inahusika na ushirika,nitaomba radhi kama hahusiki na vyama vya ushirika

Tizeba ameshindwa kuumua ari ya wananchi kuanzisha ushirika wa uzalishaji mali,ili waweze kukopeshwa na SIDO mashine ambazo watazalisha mali.

Tizeba ameacha vyama vya ushirika viendelee na utamaduni wa kukopa mabenki na kununua mazao toka kwa wakulima,ambapo kwa utaratibu huu,mazao yetu yataendelea kukosa thamani kwa kuwa yatauzwa yakiwa ghafi.

Kwa mfano mashine ya kubangua korosho yenye uwezo wa kuchukua tani 4,korosho ghafi na kutoa tani 1 moja ya korosho iliobanguliwa kwa masaa 8,inauzwa china dola elfu 8
na kwa mashine hiyo utahitaji vijana au wakinamama kama 20 katika kazi nzima kuzunguka mashine

Tizeba na Mwijage,huu ni msimu wa korosho,mmeshindwa kumwagia hizo mashine vyama vya msingi kote ilimwapo korosho ili wabangue korosho yetu na kuiuza kwa thamani ya juu?

Ikumbukwe kwamba mfumo wa stakabadhi ghalani unaruhusu kukopea,kweli mmeshindwa kutengeneza mfumo ambao utamwaga hivyo vimashine vya dola 8,000 kusini yote na pwani.

Ifikie wakati sio kila jambo ahamasishe Rais,uanzishwaji wa viwanda unatakiwa uanze kwetu sisi,tena viwanda vidogo vitaokoa maisha ya wengi sana kwa njia ya ushirika kwa kua gharama za uendeshaji ni ndogo.

Tizeba na Mwijage,sera ya viwanda sio lele mama,kujenga kiwanda kimoja ni miaka miwili hadi mitatu,itafika 2020,tutakimbiana jamani,anzeni basi walau na viwanda vidogo,matunda yanaoza Handeni au mnasubiri Bakhressa apeleke kiwanda?waewezesheni wakulima kwa mashine ndogo za kukamua uji tu wa matunda ambao una soko kwa wenye viwanda vikubwa.

Tanzania ya viwanda inawezekana,tusimuache Rais peke yake
 
Nasikia Tizeba amevunja bodi ya korosho?
 
aliwaweka si kwa uwezo wao katika kufanya kazi bali kwa ukanda, acha wamwangushe
 
Tuanze na viwanda tunavyohitaji zaidi mf. Dawa za binadamu,mifugo na mimea pia kemikali za kuhifadhia vyakula .
Nguo na bidhaa za ngozi ni aibu maana ng'ombe tumewajaza tele.
Vyakula vya kusindika kwenye makopo.
Furniture na bidhaa za plastiki ambapo utengenezaji wake huwa ni rahisi.
Walau tuunde task force itayohakikisha kila baada ya mwaka kuna viwanda kadhaa hasa vya wazawa vimeanzishwa. Ikibidi tupeleke watu nje ya nchi kusomea technolojia mbalimbali kwa makusudio maalum badala ya kusomesha nje wanasiasa kama kina Nap..Naye. Bila mpango wa makusudi tutaendelea kununua dawa Kenya na baadae hata nguo tutanunua kwao kwakuwa tunashindwa kutengeneza mpango kazi wamaana
 
Back
Top Bottom