Kupima mwaweza kujiorganise na mkatafuta any registered surveyor/mpima akawapimia maeneo yenu kwa gharama mtakayokubaliana naye,ila kumilikishwa kwa maana ya kupata hati utatakiwa kwenda halmashauri husika idara ya ardhi ambamo kiwanja chako kipo,utapeleka barua ya maombi ya kupimiwa,survey map kutoka kwa surveyor na TP drawing /ramani ya mipangomiji kilipo kiwanja chako,utalipa gharama za kumilikishwa kama uandaaji wa hati,usajili wake,kodi ya ardhi na stamp duty then utaandaliwa hati yako ,utakwenda kuisaini mbele ya hakimu,wakili nk baada ya hapo hati yako itapelekwa kwa kamishna wa ardhi kwa kusainiwa na kusajiliwa na msajili wa hati ili iweze kuoperate kama kuikopea bank ,kuweka dhamana nk