Tisa kizimbani mauaji ya Musoma

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
JESHI la Polisi mkoani Mara limewafikisha mahakamani watu tisa kwa madai ya kuhusika na mauaji ya watu 17 wa ukoo mmoja yaliyotokea mkoani humo mwezi uliopita.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Robert Boaz, alisema hayo jana wakati akizungumza na gazeti hili na kuongeza kuwa watuhumiwa hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani humo.

Alisema licha ya kuwafikisha mahakamani, lakini upelelezi bado unaendelea. Aliwataja waliokamatwa kuwa ni Matiko Mugasa (42), Juma Mgaya ama Jumanne Maselele (29), Juma Kinoko au Butenge Nyasoro (20), Daud Mahiki (50), Aloyce Nyakumu (43), Bahati Maryambo (34), Nyakangara Biraso (32), Marwa Mugaya (16) na Nyakaranga Mgaya.

Kamanda Boaz alisema upelelezi bado unaendelea, huku akiwashukuru wananchi wote walioshirikiana na Jeshi hilo kuhakikisha watuhumiwa hao wanakamatwa.

Watu hao wa familia moja walikufa baada ya watu ambao hawakujulikana kuvunja milango ya wakazi hao na kuwashambulia kwa silaha zikiwamo zenye ncha kali kama vile mapanga.

Miili ya wanafamilia hao ilizikwa katika kijiji cha Mgaranjabo nje kidogo ya mji wa Musoma.
 
Back
Top Bottom