Kesi ya Mauaji ya Mkuu wa Gereza la Liwale na wenzake yasikilizwa Mahakamani, yaahirishwa leo Julai 6, 2022

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,801
11,961
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Lindi imeahirisha kesi ya mauaji ya mfungwa Abdallah Ngalumbale inayowakabili maafisa watatu wa Magereza Mkoani Lindi kutokana na upelelezi kutokamilika.

Watuhumiwa hao ambao ni ACP Girbert Sindani ambaye ni Mkuu wa Gereza la Liwale, Sajenti Yusuph Selemani pamoja na Coplo Fadhil Mafwad wanashtakiwa kwa tuhuma za kumuua mfungwa huyo aliyekuwa akitumikia kifungo chake katika Gereza la Wilaya ya Liwale.

Kwa mara ya kwanza Watuhumiwa hao wamefikishwa Mahakamani hapo Juni 23, 2022 na leo Julai 6, 2022 wamefikishwa Mahakamani hapo lakini kesi yao imeahirishwa hadi Julai 20, 2022 kutokana na upelelezi kutokamilika na hivyo watuhumiwa hao kuendelea kusalia rumande.

Source: Mashujaa Radio

Pia soma: Mkuu wa Gereza la Wilaya ya Liwale kortini kwa mauaji
 
Kiukweli ACP Sindani amezingua sana. Hata kama hao askari na wafungwa walishirikiana kuiba hayo mahindi, bado alitakiwa kutumia njia rahisi ya kukusanya ushahidi.

Hii njia aliyotumia haikubaliki hata kidogo. Hivyo sheria iendelee tu kuchukua mkondo wake. Maana hakuna namna.
 
Uyu ikibainika aliua kwa kusudia auwawe na yeye ili familia zilie kilio kimoja
 
Back
Top Bottom