Taarifa za uhakika zilizotoka kwa vyanzo ndani ya NSSf zinasema shirika hilo tangu mwezi Desemba mwaka 2015 limewatimua wafanyakazi kadhaa kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya kutungwa. Hadi sasa zoezi hilo la kutimuatimua hovyo wafanyakazi bila kuzingatia sheria linaendelea.
Mtakumbuka mpaka sasa wakurugenzi kadhaa wa shirika hilo wanaendelea kupokea mishahara yao bila kuifanyia kazi tangu mwezi julai waliposimishwa kupitisha uchunguzi usiokuwa na kikomo lakini wafanyakazi wa chini wanatimuliwa kama vibaka licha ya wengi wao kulitumikia shirika hilo toka enzi za akiba
Tayari wafanyakazi kadhaa wamekwisha fungua kesi mahakamani na wameshinda na hivyo shirika kudaiwa mamilioni ya shilingi kama fidia ya kutimua bila kuzingatia sheria.