Timu ya taifa ya Zanzibar (N'debwedo) yafungiwa maisha

Timu ya taifa ya Zanzibar (N'debwedo) yafungiwa maisha

norbit

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2007
Posts
900
Reaction score
768
ndebwedo.jpg
CANNAVARO, CHOLLO, SELEMBE, AGGREY MORRIS NA MCHA VIALLI WAFUNGIWA KUCHEZA POPOTE DUNIANI

NAHODHA wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ni miongoni mwa wachezaji 16, waliofungiwa kwa muda usiojulikana kucheza soka popote duniani na Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), ambacho pia kimeivunja rasmi timu ya taifa, Zanzibar Heroes kwa tuhuma ya utovu wa nidhamu.

Akitangaza maamuzi ya kikao cha Kamati Utendaji ya ZFA kilichofanyika leo mchana ofisi za chama hicho zilizopo Kiembe Samaki, nje kidogo ya mji wa Zanzibar, Makamu wa Rais wa ZFA Unguja, Alhaj Haji Ameir, alisema Wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji waliohudhuria kikao wameunga mkono hatua hiyo, ili iwe fundisho kwa wachezaji wengine.

Kikao hicho cha dharura kimekuja kufuatia sakata la wachezaji wa Zanzibar Heroes kuamua kugawana kiasi cha dola za Kimarekani 10,000 walizopata baada ya kushika nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge iliyomalizika wiki iliyopita mjini Kampala, Uganda, kufuatia kuifunga Bara, Kilimanjaro Stars kwa penalti 6-5, baada ya sare ya 1-1.
Inadaiwa kuwa wachezaji hao waliamua kugawana fedha hizo kwa madai kuwa wamekuwa wakidhulumiwa fedha zao na ZFA.

Hata hivyo katika ufafanuzi uliotolewa leo na Katibu Mkuu wa ZFA Taifa, Kassim Haji Salum, amesema haijawahi kutokea wachezaji wa timu hiyo kudhulumiwa haki yao akikumbushia fedha za zawadi walizopata mwaka 1995 katika mashindano kama haya yaliyofanyika nchini Uganda na Zanzibar ikafanikiwa kutwaa ubingwa na mwaka 2009 waliposhika nafasi ya tatu na mara zote walipewa stahili zao.

Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa Zanzibar, Salum Bausi ambaye jana alitangaza rasmi kujiuzulu kuifundisha timu hiyo, amesema hatua hiyu ni sahihi kabisa kwa sababu kitendo hicho kimewafedhehesha wadau wa soka na Wazanzibari kwa ujumla.

Tayari ZFA Taifa walikwishatuma barua rasmi kwa TFF juu ya hatua hiyo huku nakala ya barua hizo zikitarajiwa kusambazwa kwa vilabu wanavyochezea wachezaji hao.

Wachezaji wanne walionusurika na adhabu hiyo ni wale walioamua kuzirejesha fedha hizo ambao majina yao hayakutatwa kwa sababu maalum, hata hivyo taarifa zilizopo ni kuwa wachezaji hao wanatoka katika klabu ya Kipanga timu inayomilikiwa na JWTZ, Jamhuri, Zimamoto na KMKM.

Kikosi cha Zanzibar kilichokwenda Challenge ni makipa; Mwadini Ali (Azam), Suleiman Hamad (Black Sella), Abdalla Juma (Kipanga), mabeki; Nassor Masoud ‘Chollo’ (Simba), Samir Haji Nuhu (Azam), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub Ali ‘Canavaro’ (Yanga), Aziz Said Ali (Kmkm), Mohammed Juma Azan (JKU) na Ali Mohammed Seif (Mtende Rangers).

Viungo ni; Hamad Mshamata (Chuoni), Ali Bakar (Mtende Rangers), Is-haka Mohammed (JKU), Twaha Mohammed(Mtibwa Sugar), Suleiman Kassim ‘Selembe’ (Coastal Union), Saad Ali Makame (Zanzibar All Stars), Makame Gozi (Zimamoto), Issa Othman Ali (Miembeni), Aleyuu Saleh (Black Sella), Khamis Mcha Khamis ‘Viali’ (Azam) na washambuliaji; Amir Hamad (JKT Oljoro), Jaku Juma Jaku (Mafunzo), Abdallah Othman (Jamhuri), Nassor Juma (JKU) na Faki Mwalim (Chipukizi).
 
hizo ni hasira tu; dola elfu10 siyo za kufungia wachezaji kucheza mpira maali popote; itafutwe adhabu nyingine iliyoko kwenye kanuni za ZFA na kutambuliwa na CAF pamoja na FIFA lakini siyo hii iliyotolewa
 
Kosa lililofanyika halilingani na adhabu waliyopewa, wafikirie upya
 
Nchi ya Tanganyika ilifungwa ngapi vile na nchi Zanzibar?

Wazenj nouma😀

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk 2
 
Inauma sana jamani dolale wamechukua waliocheza maumivu wanapata viongozi ha ha ha ha kweli kazi ipo.
 
Mbele ya CAF na FIFA, ZFA haitambuliki kwa sababu si mwanachama, hivyo adhabu hiyo inaishia Nungwi tu. TFF ndio wenye mamlaka hayo kama wataidhinisha hiyo adhabu. Lakini ni kweli viongozi wengi wa mpira wanawanyonya wachezaji kama unakumbuka yaliyowapata watoto wa Simba baada ya michuano ya BANC ABC
 
Kitu kimoja tu najua,ZFA haitambuliki na FIFA hivyo sidhani kama ina mamlaka kutoa instructions zinazoweza kuheshimiwa na FIFA wala mwanachama yeyote wa FIFA.Ngoja tuone
 
Kwa jitihada walizoonyesha wachezaji wa Zanzibar katika mashindano hayo kuwafungia maisha si suluhu kwani bado tunahitaji vipaji vyao katika kuboresha soka letu Tanzania kwa ujumla.

Kuna vijana wengi waochipukia wanahitaji kujifunza kutoka kwao.

Mimi naona kuna tatizo la kimfumo hasa linapokuja suala la makabidhiano ya zawadi, hii maneno ya kukabidhiana cash kwa kweli haijatulia maana achilia mbali watu kuingia nazo mitini lakini hata kiusalama tu haiko sawa.

Wafikirie adhabu nyingine ikiwemo kuwakata katika mapato yao yeyote yali kufidia hiyo pesa lakini sio kuwafungia maisha. Hapo watakuwa hawajengi zaidi ya kubomoa.
 
Unamfungia maisha Kwa kuchukua dollari 500 yake!! Sasa mgewalipa ngapi wangerejesha?
10000/20 =500.wachezaji 4 wameerejesha = 2000.jamaa wamechukua 8000 tu
 
....

Wafikirie adhabu nyingine ikiwemo kuwakata katika mapato yao yeyote yali kufidia hiyo pesa lakini sio kuwafungia maisha. Hapo watakuwa hawajengi zaidi ya kubomoa.

Kama hakuna utaratibu ulio rasmi ndani ya katiba ya ZFA juu ya mgawanyo wa fedha za Zawadi kwa timu ya Zanzibar Hero, hakuna kuwakata hata senti moja kama ipo. Wanaotakiwa kulalamikia Mgawo ni benchi la ufundi na kocha wa Zanzibar Heros waliokuwa na timu kama wachezaji waliwatosa katika mgawo.
 
hizo ni hasira tu; dola elfu10 siyo za kufungia wachezaji kucheza mpira maali popote; itafutwe adhabu nyingine iliyoko kwenye kanuni za ZFA na kutambuliwa na CAF pamoja na FIFA lakini siyo hii iliyotolewa
kaka hizo hasira zinaonesha chuki kubwa sana maana naona watu walishaandaa viwanja vipya sasa wachezaji wametibua dili na ilikuwaje wachezaji wakapokea pesa.
 
Inauma sana jamani dolale wamechukua waliocheza maumivu wanapata viongozi ha ha ha ha kweli kazi ipo.
kaka ulishaona mwizi anakasirika kwa kushindwa kumwibia mwenye mali kweli wizi nikipaji.
 
kaka ulishaona mwizi anakasirika kwa kushindwa kumwibia mwenye mali kweli wizi nikipaji.
Wapo wanaokasirika ikiwa kile walichopanga kuiba hakijafanikiwa mkuu taamu.
 
Back
Top Bottom