KUNDI linalomuunga mkono Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, katika harakati zake za kuingia Ikulu Oktoba, mwaka huu, linalojulikana kama ‘Friends of Lowassa', limeandaa tukio kubwa la kihistoria wiki hii.
Kwa mujibu wa taarifa za ndani ya kundi hilo zilizolifikia gazeti hili mwishoni mwa wiki, wakati wowote wiki hii, makada wastaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), watakusanyika jijini Arusha kutoa tamko la ‘kumshawishi' Lowassa kutangaza nia ya kugombea urais.
Katika wiki chache zilizopita, waratibu wa shughuli za kampeni za Lowassa walibadili mbinu za kumshawishi kada huyo mkongwe agombee urais; na sasa badala ya ‘mashabiki' wao kufunga safari kumfuata aliko, huita vyombo vya habari, hususan TV, na kutangaza kumuunga mkono wakiwa huko huko waliko.
"Sasa hivi mipango inaendelea ili kundi kubwa la Watanzania litakalojumuisha wazee wa kimila wa Kimasai kutoka kila kona ya Arusha, siyo wa Monduli peke yao, pamoja na wenyeviti na makatibu wastaafu wa CCM wa mikoa ya Kanda ya Kaskazini wakusanyike hapa Arusha mjini kumuomba mzee atangaze haraka nia ya kugombea urais.
"Hii ya Arusha si mchezo, maandalizi yake ni makubwa mno kwa kuwa ndipo anapotoka mzee. Tukio hili litakuwa kubwa na baada ya hapo, basi! Hakutakuwa na makundi mengine tena yatakayotoa matamko kumshawishi mzee," alisema mmoja wa waratibu ndani ya Friends of Lowassa ambaye hatuwezi kumtaja gazetini kwa sababu za wazi kabisa.
Raia Tanzania linafahamu kuwa mipango yote kuhusu kufanyika kwa mkutano huo imekamilika na kwamba tukio hilo awali lilipangwa kufanyika wakati wa Sikukuu ya Pasaka, lakini likaahirishwa kutokana na wadau muhimu kuwa katika shughuli za mazishi ya mfanyabiashara mmoja wa Tanzanite aliyeuawa wiki iliyopita.
Majina ya baadhi ya wazee wa kimila na makada wastaafu wa CCM waliopewa taarifa za mkutano huo tunayo.
"Mbali na makada hao, pia wapo wazee maarufu wa Arusha na wazee kutoka vyama vya upinzani (hakutaja majina). Hii shughuli itakuwa kubwa kuliko zote zilizowahi kufanyika," alisema mtoa taarifa wetu.
Alisema mkutano huo mkubwa jijini Arusha utatumika pia kuujulisha umma wa Watanzania kwamba ingawa Arusha ni ngome ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Lowassa anakubalika kugombea nafasi ya urais.
Taarifa zaidi zinadai kuwa baada ya mkutano huo, mambo yatasitishwa kusubiri Lowassa atangaze nia yake; na kwamba mbunge huyo wa Monduli anatarajiwa kufanya hivyo ndani ya wiki mbili zijazo.
Mipango ya Lowassa kuweka hadharani nia yake hiyo imekuwa ikiahirishwa kwa zaidi ya mara nne sasa kutokana na sababu mbalimbali za kimkakati, kubwa ikiwa ni Lowassa kuwa katika uangalizi wa Kamati Ndogo ya Maadili ya Kamati Kuu ya CCM kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, baadhi ya wadau wa siasa mkoani Arusha walisema harakati zinazofanywa na Friends of Lowassa ni dalili ya woga na kutojiamini hasa kukubalika kwa wanayempigani miongoni mwa Watanzania.
Mkazi wa Sakina jijini hapa, Haji Mseleka, alisema kwa Watanzania kulazimishiwa mtu kuwa Rais (kama wanavyofanya Friends of Lowassa) si sahihi na badala yake Watanzania waachwe wachague wenyewe muda ukifika.
"Kufanya kampeni si vibaya, lakini wanazofanya si kampeni bali ni kuwahadaa Watanzania na kuwalazimisha kuchagua chaguo la wachache; lakini ngoja tuone," alisema Msekela.
Hivi karibuni wanodaiwa kuwa ni Masheikh wa mkoa wa mwanza walitoa kauli kumtaka Lowassa kutangaza nia huku pia wakimpa fedha za kuchukulia fomu za kugombea urais mlango utakapofunguliwa rasmi.
Chanzo: Raia Tanzania