mshumbusi
JF-Expert Member
- Oct 24, 2011
- 457
- 231
wadau ni matumaini yangu mpo salama
ni jambo lililo wazi kwamba mbio za urais zimefikia hatua kali sana hata wengine kudiriki kutumia makanisa kwa manufaa yao. Bila kificho timu ya kampeni ya mheshimiwa mizengo pinda (maarufu kama mzee wa kulia lia), wamesambaza waraka katika makanisa kuwa rais ajaye lazima awe ni mkatoliki (kitendo ambacho kimeshangaza watu wengi sana). Mwalimu nyerere katika uhai wake alilikemea jambo hili kwa nguvu zake zote na kwa ukali kabisa naomba kunukuu maneno ya nyerere "siyo sahihi kumchagua mtu kwa sababu ya dini yeka au dhehebu lake na vile vile siyo sahihi kutomchagua mtu kwa sababu ya dini yake au dhehebu lake, akitokea mtu wa namna hiyo hatufai hata kidogo".
waraka huu umeanza kusambazwa katika makanisa ya mikoa ya kaskazini mwa tanzania (mikoa ya kilimanjaro, arusha na manyara), na mimi kama muumini wa kanisa hili nilishangazwa sana jumapili hii iliyopita ya tarehe 26/10/2014, waraka huu uliposomwa kwa mara ya kwanza katika kanisa langu hapa manyara. Waratibu wa huu mkakati ni mdogo wake mkuu wa mkoa wa mwanza ambaye ni padri katika kanisa la katoliki na ni maarufu kwa jina la paroko (jina kamili ni emmanuel ndikilo) wakishirikiana na mpambe mkubwa wa pinda anayeitwa mwalimu m. Shilatu..
Katika hatua nyingine ya kuonyesha hali ya kisiasa ndani ya ccm imekuwa mbaya sana, mheshimiwa mizengo pinda kwa kujiimarisha kifedha amekuwa akiratibu michango mbali mbali kutoka kwa wakurugenzi wa mikoa na wilaya, na mratibu mkuu wa hili jambo ni dr.masaburi akishirikiana na wakurugenzi 5 wakiwa kama timu. Dr. Masaburi kapewa huu uratibu kutokana na nafasi aliyonayo kwenye alat (so unaweza kucconect the dots); nakumbuka hili swala la wakurugenzi kufungua account maalumu kwa ajili ya kampeni za pinda lilishawai kuletwa humu ndani na mdau mmoja ocampo four na kueleza jinsi wakurugenzi wanavyochangisha ela za umma kwa ajili ya kampeni.,jina maarufu ya hiyo account ni "akaunti ya nyau" au "akaunti ya simba"
nb: Jf ni chanzo kizuri cha habari hivyo, tunaomba serikali iiangalie hilo swala la wakurugenzi kuchangishwa fedha
kwa ajili ya kampeni, na ikibidi hatua zichukuliwe, mutambue wananchi wanajua hili jambo na wanapokosa huduma za kijamii kama madawa, maji, chakula nk wanaumia sana sana.
2). Uongozii wa juu wa katoliki tafadhali waraka kama hizo zisisambazwe tena na tena, zitaleta hisia za kidini.
Naomba kuwasilisha
ukipewa walaka usambaze na ukashindwa kusambaza ....:utapigwatu...na mimi na sema wewekama utaki kusikiza walaka utapigwa .maana hakuna namna