upupu255
JF-Expert Member
- Sep 4, 2024
- 356
- 491
Katika kuadhimisha Wiki ya Mama, Timu ya Kampeni ya Mama Asemewe imefanya ziara katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, ambapo wameeleza umuhimu wa kuchagua viongozi bora kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 pamoja na kuonyesha kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Timu hiyo, ikiongozwa na Bw. John Danda Katibu mkuu wa Samia for Us, Makamu Mwenyekiti wa Kampeni ya Mama Asemewe Bi. Verynance Mrema na Anna Kivuyo, Naibu Katibu Mkuu wa Samia for Us, imewahamasisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura na kuwalekeza juu ya mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais Samia katika kipindi cha miaka minne madarakani.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Katika ziara hiyo iliyofanyika tarehe 20 Machi 2025, wananchi walielezwa kuhusu miradi ya maendeleo, juhudi za kuboresha huduma za jamii, na mchango mkubwa wa Rais Samia katika kukuza uchumi wa nchi.
Aidha, wananchi walieleza kuridhika kwao na mafanikio yaliyopatikana katika nyanja mbalimbali, kama vile elimu, afya, miundombinu, na uchumi, katika kipindi cha miaka minne chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Wananchi wameonesha shukrani zao kwa Serikali kwa hatua zinazochukuliwa katika kuboresha maisha yao na ustawi wa taifa.
Aidha Ziara hiyo imejikita katika kuhamasisha wananchi kuwa na uelewa mkubwa kuhusu kuchagua ongozi bora na umuhimu wa kuendelea kushirikiana na Serikali katika kukuza maendeleo ya taifa.