Timiza ya Airtel wizi mtupu!

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,486
Ni wizi maana wanatoza riba kubwa kuliko hata mabenki na matangazo yao yanasheheresha huo wizi.

Ukitaka kukopa tshs 6,000/= utakatwa kamaifuatavyo; kopa tshs 500, lipa tsh 565
kopa tsh 1,000 lipa 1,135
kopa tsh 2,000 lipa 2,270
kopa tsh 5,000 lipa 5,675
kopa tsh 6,000 lipa 6,810
rates hizi ni chini ya wiki 1.

Jumlisha riba zote; 65+135+270+675+810=1,955

1,955/6,000=30% per week, 120% kwa mwezi.

Hakuna anaekulazimisha kukopa ILA uhamasishaji wa kukopa ni mkubwa na viwango vya ukopaji na riba zake havijawekwa wazi. Mfano ukitaka kukopa tsh 20,000/= ni lazima uanzie kiwango cha chini cha tshs 500 na ufuate mtiririko wao hadi ukute kiwango unachotaka. HUU NI ZAIDI YA UPATU!
 
Cjui TRA inawatoza bei gani kwa mikopo yao ya kitapeli hawa Airtel??????
 
Mziki wa M-PAWA umewachanganya aisee, hizo riba za timiza ni "upatu" msemo wako mtoa mada, na mikopo yao ni ya wiki moja au mbili..
 
kiwango cha riba cha mikopo kweoye simu ni hatari. hakuna udhibiti. ni wazi mtupu.
 
Back
Top Bottom