Kazi ya halmashauri ni kutoa huduma za jamii ikiwemo usafi wa miji husika! Ni wajibu wa halmashauri wanapoona eneo la biashara fulani ni chafu basi walisafishe na si kuwafukuza watumiaji wa eneo husika. Jiji la mbeya walitakiwa kuboresha maeneo ya hayohayo waliopo wamachinga kwa kujenga miundombinu bora ya biashara!! jiji wana wahandisi, wabunifu majengo na watalaam wengine, kwa nini wasibuni structures hata za muda na zenye kuwa na muonekano wa usafi badala ya kubomoa? Maana Kama ni uchafu basi hata soko la SIDO hapo hapo Mbeya ni Chafu kwani vibanda vimejengwa ki-uchafu uchafu! likewise masoko mengine kama mbalizi, Mkuyuni mwanza, Tandale Dar, Sinza makaburini, Kimara mwisho, na mengine mengi!!
Ifike wakti serikali inapoona raia wake wameanzisha jambo fulani kwa maendeleo yao basi iweke mkono wa support badala ya mkono wa discauragement!!! iweke ubunifu wa kitalaam wenye kuwahamasisha raia kuongeza uzalishaji badala ya kuwakatisha tamaa!!